Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
pole sana mtanzania mwenzangu na mwana jamii mwenzangu,,,,ninachoweza kukushauri ni kwamba jikaze uonane naye ila iwe sehemu ya wazi na uambatane na rafiki zako kama watatu au wanne,,pia usisahau kumwomba mungu juu ya hilo ili akulinde kwa kila jambo.
Loooo jamani haina maana ya kuonana na mtu ambaye hakuona thamani yako kama mtoto wake, sasa hivi ndio ataonaje umuhimu wako, endelea na maisha yako achana naye, hata Mungu hatakuhukumu kwa hilo
pole sana ezam ninachoweza kukwambia sasa kwa sababu wewe ni mtu mzima 34 years unajua jema na baya,
kama una nia ya kumuona baba yako wewe panga nae mkutane ,ila sehemu yenyewe iwe ya wazi na mazingira yaliyo na watu kabisa ama unamwambia hata rafiki yako anakuwa katika mazingira utakayokuwepo,
inawezekana sasa baba yako alishagundua alilotaka kufanya halikuwa sahihi na moyo wake unamsuta
anaweza kuwa anakutafuta akuombe samahani..jipe moyo wa kiume na ukubali wito,ili angalau moyo wako uwe free na uweze kumjua baba yako.
pole sana ezam ninachoweza kukwambia sasa kwa sababu wewe ni mtu mzima 34 years unajua jema na baya,
kama una nia ya kumuona baba yako wewe panga nae mkutane ,ila sehemu yenyewe iwe ya wazi na mazingira yaliyo na watu kabisa ama unamwambia hata rafiki yako anakuwa katika mazingira utakayokuwepo,
inawezekana sasa baba yako alishagundua alilotaka kufanya halikuwa sahihi na moyo wake unamsuta
anaweza kuwa anakutafuta akuombe samahani..jipe moyo wa kiume na ukubali wito,ili angalau moyo wako uwe free na uweze kumjua baba yako.
riwaya...................!!!!![font=&]wana jamvi mimi siyo mwandishi mzuri, wa story ndefu ila nataka kushea kidogo changamoto/tatizo nililo nalo na kunisaidia mawazo nini nifanye kwasababu hapa nilipo nimejawa na hasira lakini pia natamani kumuona kwa macho yangu baba yangu mzazi.[/font]
[font=&]wadau mwenzenu mpaka sasa nina umri wa miaka 34 nimelelewa na mama yangu toka mdogo mpaka nilipofika form three, nikiwa form three ndipo mama yangu alifariki dunia, wakati wa uhai wake nilishawahi kumuuliza mara mbili kuhusiana na yu wapi baba yangu, mara ya kwanza nilimuuliza nikiwa form one alinijibu kwamba baba yangu yupo mbali sana(kwa maana ya nje ya nchi) ipo siku nitamuona, nilipomuuliza tena nikiwa form two kwamba baba yangu atakuja lini na mbona hata haandiki wala barua? Akanijibu kwa hasira kwamba baba yangu yupo tanzania ila nimsahau nijikite zaidi katika masomo nikisha kuwa mtu mzima atanipa full story basi sikumuuliza tena.[/font]
[font=&]baada ya kifo cha mama nikachukuliwa na kulelewa na mjomba wangu ambaye amenisomesha mpaka nilipofikia kujitegemea naye alifariki mda mfupi baada ya mimi kuanza kazi. Wakati wa uhai wake mjomba nilimuhadithia kwamba mpaka mama anafariki dunia hajanionyesha baba yangu japo alidai yupo hapa nchini, mjomba alinijibu kwamba yeye anamfahamu tena hata mama akiwa hai baba yangu alikwenda nyumbani kwake mara kadhaa kuomba radhi na kutaka anichukue akanilee lakini akadai wao walikataa kata kata kutokana na kwamba baba yangu siyo mtu mzuri na ilikuwa ni hatari sana kwa mimi kuishi naye nikiwa bado mdogo ila na yeye pia aliniahidi kwamba nikisha kuwa mtu mzima na familia yangu atanipa full story.[/font]
[font=&]mara kadhaa nimekuwa namuomba mama mdogo anipe story kuhusiana na baba yangu kwani hata yeye anamfahamu na ndiye mtu pekee aliyebaki mtu mzima katika familia yao anayeweza kufahamu hili, lakini huwa ananigomea anadai hiyo ni ishu kubwa sana hawezi yeye akaniambia kwasababu naweza ku-react nikafanya maamuzi ya kutisha then yeye hataeleweka katika jamii, sana sana huwa ananisihi nimpotezee tu niendelee na ishu zangu.[/font]
[font=&]hivi karibuni nilienda mkoani kwetu nikafika kijijini wanakotoka marehemu bibi na babu yangu nilikutana na bibi mmoja(niliambiwa alikuwa rafiki yake na marehemu bibi) mama mdogo akanitambulisha kwa huyo bibi, yule bibi akastuka na kuonyesha kanikumbuka then akaanza kulia. Kuna watu wazima wawili wakamchukua pembeni sijui walikuwa wanaongea naye nini kimyakimya, baadaye akarudi akiwa halii tena ila kuna kila dalili kwamba alikuwa anajizuia kufanya hivyo na kuna jambo baya sana amekumbuka. [/font] [font=&]
majuzi nimepigiwa simu na mtu mzima mmoja anadai anaomba nitafute siku tukutane popote pale ana mazungumzo na mimi ya mda mrefu sana, nilipomuomba aniambie yeye ni nani akajibu yee ni baba yangu, nikastuka sana ila nikajikaza kiume nikamwambia mimi simfahamu baba yangu, akanijibu una haki ya kusema hivyo ila ni habari ndefu sana nijitahidi nifanye tuonane tuzungumze, nikamuahidi nitampigia nikipata mda, bila kuchelewa nikampigia simu mama mdogo na kumtaarifu hili suala, yeye akastuka na akanijibu kwa kuhamaki kwa kifupi tuu kwamba niwe makini na huyo mtu siyo mtu mzuri, akanipa story ndefu ya kutisha kwa kifupi ni kwamba baba yangu alifanya jaribio la kunitoa kafara nilipokuwa mchanga kwa ajili ya biashara zake kwasababu yeye ni miongoni watu wenye imani za hivyo, sitaweka kila kitu hapa natakiwa niandike kitabu. Ila mama mdogo kanishauri kwasababu nimekuwa mtu mzima nichanganue mwenyewe.
Hii imenistua naogopa sana kuonana na huyu mtu.[/font]
[font=&]nisaidieni wanajamvi hili suala nili handle vipi?[/font]