Smart lady
Member
- Dec 7, 2012
- 60
- 28
Wana JF.Naomba ushauri wenu.Nilikuwa na ex boyfriend ambaye tulikuwa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.Nilimpenda sana huyu kijana.Nilijitolea muda wangu na nilifanya kila mbinu aweze kufanikiwa katika maisha yake nikiamini ni mume.Nilimkuta na chumba kimoja lakini ndani ya kipindi tulichokaa, aliweza kufungua biashara, kununua gari na kuhamia nyumba ya self container. Alikuwa muwazi sana kwangu na alinieleza aliwahi kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine lakini kutokana na tabia za yule mwanamke aliamua kuachana nae.
Kadiri muda ulipokuwa unakipimbia, nilihitaji tuwe wawazi kwa wazazi lakini yeye aliniambia bado sijajipanga.Nilimvumilia na nikaendelea kuwa nae.Baada ya muda, jumapili nimekaa home napokea simu yake.Nilijua natolewa out kumbe masikini ya Mungu nataarifiwa kuwa mwenzio nataka kuoa hivi karibuni hivyo nimeona ni vizuri kukufahamisha.Kwa kweli niliumia sana kiasi ambacho siwezi kusimulia.
Ilikuwa ni ngumu kuamini anayoongea lakini baada ya muda na uchunguzi nikagundua ni kweli na aliyemuoa ni yule girl friend wake wa kwanza.Marafiki zake hawakuamini, na wengine wamemkimbia kabisa.Cha ajabu na cha kushangaza ni kwamba ameoa lakini kila siku ananipigia simu na kunitumia e mail.Kwa kweli inanikera sana.Nimebadilisha line lakini wapi.Sijui aliipata wapi line yangu mpya.Nimfanyaje?