Inaniuma!

Smart lady

Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
60
Reaction score
28
Wana JF.Naomba ushauri wenu.Nilikuwa na ex boyfriend ambaye tulikuwa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.Nilimpenda sana huyu kijana.Nilijitolea muda wangu na nilifanya kila mbinu aweze kufanikiwa katika maisha yake nikiamini ni mume.Nilimkuta na chumba kimoja lakini ndani ya kipindi tulichokaa, aliweza kufungua biashara, kununua gari na kuhamia nyumba ya self container. Alikuwa muwazi sana kwangu na alinieleza aliwahi kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine lakini kutokana na tabia za yule mwanamke aliamua kuachana nae.
Kadiri muda ulipokuwa unakipimbia, nilihitaji tuwe wawazi kwa wazazi lakini yeye aliniambia bado sijajipanga.Nilimvumilia na nikaendelea kuwa nae.Baada ya muda, jumapili nimekaa home napokea simu yake.Nilijua natolewa out kumbe masikini ya Mungu nataarifiwa kuwa mwenzio nataka kuoa hivi karibuni hivyo nimeona ni vizuri kukufahamisha.Kwa kweli niliumia sana kiasi ambacho siwezi kusimulia.
Ilikuwa ni ngumu kuamini anayoongea lakini baada ya muda na uchunguzi nikagundua ni kweli na aliyemuoa ni yule girl friend wake wa kwanza.Marafiki zake hawakuamini, na wengine wamemkimbia kabisa.Cha ajabu na cha kushangaza ni kwamba ameoa lakini kila siku ananipigia simu na kunitumia e mail.Kwa kweli inanikera sana.Nimebadilisha line lakini wapi.Sijui aliipata wapi line yangu mpya.Nimfanyaje?
 
forget him huyo hakufai kwa ufupi huyo ni playboy,em jaribu kuwa smart kama jina lako Smart lady,mpotezee kabisa angalia mbele utampata mwingine aliye serious na life....
 
Last edited by a moderator:
chezea wanaume nini.....hao ndio vidume vya kweli!!! na nyie dada zetu janjarukeni kila leo nyie mwaliwa papuchi tuu na kuolewa msiolewe. hesabu hasara na huyo anataka awe anakugegeda tuu. piga chini
 
Pole hny me nakushauri ujitahidi kuwa bize kujenga maisha yako na Mwenyezi Mungu atakupa mwingne atakayekupenda na anayejua thamani yako
 
Pole sana mkuu. When you love someone, don't expect something in return. Wewe achana naye kabisa hafai huyo. Kama unatumia smartphone nakushauri uiInstall software ya kuBlock calls ili uBlock calls na SMS zake.

Pole sana na ni muda pekee ndo utakaokuponya. Utaumia sasa hivi ila baada ya muda kupita maumivu yataisha. Just let it flow, let it go.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
smartlady sikuiti ila ndivyo ulivyo my dear.
ulikuwa very smartlady ulipoamua kumwachia aondoke kwenye maisha yako ingawa kwa hali iliyokuumiza sana. sasa asikutie shombo kabisaa mwambie wewe ni zaid ya anavyofikiri and tell him straight Mungu alionA he is not a good hubby for you akatafuta njia ya wewe kupona sasa asikusumbue kwani Mungu ameamua kukupumzisha

do you know what, Mungu hujua mahitaj ya mioyo yetu and always he is good sasa usishangae sana anajua amekosea ila usimpe nafasi tena kwenye maisha yako. carry on aliyekusudiwa kwaajili yako atakuja very soon and hapo utauona wema wa Mungu kwako.
waswahili husema LIKUKWEPALO LINA HERI na pia husema HERI NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI na wenye akili zaid wakamalizia HERI KENDA NENDA KULIKO KUMI NENDA RUDI
 
Last edited by a moderator:
Nina hasira sana kwenye tabia za hovyo namna hii.Kama unajipenda achana na huyo jamaa,angalia maisha yako.
"
Watu wengine wanakera sana!
 
forget him huyo hakufai kwa ufupi huyo ni playboy,em jaribu kuwa smart kama jina lako Smart lady,mpotezee kabisa angalia mbele utampata mwingine aliye serious na life....

Hivi wewe unakumbuka ile miadi yetu?

Nimekumisi ujue......
 
Last edited by a moderator:
Dawa ya moto ni moto. Kama unampenda na anakutafuta mkubalie ubinjuke kwa raha zako. Hakikisha mpaka mkewe anajua ili ampige chini. Akishapigwa chini na mkewe nawe unampiga chini.

Nlishamfanyiaga shori mmoja enzi hizo aliponifanyia unaa kama huu.
 
kama wewe ni fulani, nakumbuka ulivyoumia hadi kwenda Ghana kuombewa, pole sana kama ni wewe.

Ila usiwe 'desparate' na ndoa, watakugonga tu.

Pole
 
Hivi wewe unakumbuka ile miadi yetu?

Nimekumisi ujue......

Mkuu Asprin, it seems like hiyo ni private issue baina yenu so ungemPM ingekuwa jambo jema zaidi. Jaribu kufikiria kila mtu aanze kuongea na mwenzie kuhusu private issues zao kwenye hii thread itakuwaje?

It's so irritating wakati ambapo mtu anamatatizo anaomba ushauri, anapitia asome ushauri anakuta watu wanaongea mambo ambayo hayahusiani. Inamaana hii thread isingeazishwa usingemuulizia hiyo miadi yenu?

Nyie wakongwe ndiyo mnaotakiwa mtufundishe sisi wageni jinsi ya kuBehave humu ili tujifunze kutoka kwenu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
You are too smart for him; yuko attracted kwa drama girl wait till wakorofishane tena, atarudi huku dick yake ameifyata kama mkia wa mbwa!

Good riddance!
 

acha kuingiza Mungu ambapo hastaili....poor decision yake ndio prince anayo pay!!!
 

Hayatuhusu. Pelekea umbeya wako kwenye majukwaa mengine. siyo humu ndani. Kama huna cha kuandika, tulia kimya, nyamaza kabisa kabisa. Soma michango ya watu wengine. Unajiabisha tu hapa ndani.
 
labda unywe maziwa jirani?

Kwani mtaani wapya wanafundishwa kila kitu na wakongwe?

 
hata kugegedana raha, ndoa matokeo tu.

chezea wanaume nini.....hao ndio vidume vya kweli!!! na nyie dada zetu janjarukeni kila leo nyie mwaliwa papuchi tuu na kuolewa msiolewe. hesabu hasara na huyo anataka awe anakugegeda tuu. piga chini
 
hata kugegedana raha, ndoa matokeo tu.

hahaha ndoa ingekuwa matokeo tuu msingekuwa mlalamika pale ambapo wanaume wana wagegeda na kusepa. the mere fact kwamba mnalalamika inaonyesha kuwa ndoa ni kitu ambacho deep down mna expect na mngependa uhusiano na mwanaume uishie huko....so dnt try trivialize the importance of marriage especially from a female perspective.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…