Inapendeza zaidi kama...

...wasichana waache kupokea hela na zawadi za wanaume iwapo hawawapendi!! nani kasema? "Baniani mbaya, kiatu chake dawa"
 


Mkuu, kuombaomba hakuna heshima...

Tukija kwenye hili jambo la hawa wenzetu ni tabia ambayo inatokana zaidi na mental slavery ambayo marehemu Bob Marley alitaka watu waondokane nayo ..alivyoimba "emancipate urself from mental slavery..." katka wimbo wake wa the redemption song....

Nakubaliana nawe kuwa inatokana na maisha yenye kuegemea uchumi tegemezi.... kuanzia ngazi ya taifa..... kuomba kumekuwa kama ndio chanzo cha mapato badala ya kutumia rasilimali tele tulizojaaliwa ikiwa ni pamoja na nguvu kazi yetu

Hebu turudi nyuma enzi zileeeeeee tuangalie je kule vijijini watu walikuwa waombaomba? nijuavyo mimi waliokuwa na tabia hizi walionekana wavivu na walidharauliwa sana. Likewise kama tutawaendekeza hawa na kuwatetea.... hatutakuwa tunawasaidia... ndio maana wahenga walisema " mtumai cha ndugu hufa maskini..."
Kuabika ni kama hivi mtu na mdogo wake wamejikuta wakihudumiwa na mwanaume mmoja kama vile wao ndio kipande cha mwisho cha nyama kilichobaki hapa duniani!
 
Khaa jamni wasichana tubadilike jamni, hii yote tamaa ndo maana wanapokea vocha za huyo kaka,
Inapendeza zaidi mtu ukijikubali ulivyo!!
...week end hii umepatwa masahibu gani MR, sijaona vijimambo
 
Kama kina mama wengi wanakuwa na attitude hii ya kutafuta wenyewe na kujitegemea, basi tutafika mbali. Wengi wanachukulia wanaume ndio ngazi za kupanda wafike wanakotaka kufika halafu inakuwa balaa
 
Kama kina mama wengi wanakuwa na attitude hii ya kutafuta wenyewe na kujitegemea, basi tutafika mbali. Wengi wanachukulia wanaume ndio ngazi za kupanda wafike wanakotaka kufika halafu inakuwa balaa

Yaani!
Kwa sababu mmepinda migongo na kuwaruhusu wawapandie wafike watakako.
Mkiwawekea No basi watakomaa na kujipinda wenyewe.
 
Yaani!
Kwa sababu mmepinda migongo na kuwaruhusu wawapandie wafike watakako.
Mkiwawekea No basi watakomaa na kujipinda wenyewe.
Kwa elimu kama hizi tunajifunza. Inshallah tutaacha kujiingiza kwenye relationships basing on money as if money could buy someone's feelings.
Kwani kuna trick gani nyingine za kumpata dada wa kileo bila kuazima gari la mtu ili kumpeleka disco na kukopa pesa za kumzungusha viwanja mpaka aseme imetosha?
Maana haya matatizo tunakabiliana nayo waume wengi, tuliozaliwa vijijini na kukulia huko na hata wa mjini. Zamani walisema wanaume wakuja ndio tabia zao.
 
Sasa Mkuu... huyo dada wa kileo ukikuta analo gari lake je? na viwanja anavijua utatumia njia gani? Tatizo pia hutokana na kuvamia wasichana ambao hayo mambo ni mageni sana kwao....
I cant imagine umeazima gari la mtu likapata ajali ( gharama ya kutengeneza? kwako) umekopa pesa kisa umzungushe mtu viwanja.. mwisho wa siku imekula kwako..deni lazima ulipe... what do u get at the end of the day ambacho kinalingana na hasara ulizopata?
 
Yaani!
Kwa sababu mmepinda migongo na kuwaruhusu wawapandie wafike watakako.
Mkiwawekea No basi watakomaa na kujipinda wenyewe.

jamani ours is also a society, society haiwezi kurndeshwa kwa maoni kama mnayotoa hapa........, kumbukeni hata hizo vocha moyoni mwa huyo kaka hutoka kama zawadi tu na imression ya kuhonga imo moyoni mwa huyo anayependa vya dezo.......... sasa nipeni mfano wa jamii iliyoelimika kiasi cha kuomesha hata kupeana zawadi............. vinginevyo tunajilisha upepo tu........

siku zote niliamini huogopi hoja ila leo naona umekwepa kujibu hoja niliyoitoa................. hahahaaaaaaa.............
 

AK
Umenikumbusha kama miaka mitatu iliyopita kuna siku nilikuwa lumumba street nanunua vitu, nikiwa nimekaa karibu na duka moja la spea akatokea kijana mmoja ambaye alikuwa mlemavu wa miguu, akiwa anaongea kwa uhakika alikuwa anasema kuwa yeye akipata hela yoyote basi huwa anachofanya ni kutafuta mwanamke yeyote ambaye atavutiwa nae na kumtogoza na humwambia kuwa atampa hela hizo zote, nilijaribu kumdadisi kidogo na akaonyesha kuwa amesha wahi kutembea na wanawake wazuri sana kwa maneno yake, akiwapata kwenye Bar na sehemu za starehe na wote waikubali tu kuondoka nae kwenye magari yao, baada ya kuwaambia kuwa atatoa kuanzia elfu hamsini mpaka laki. Kuna jamaa alikuwa karibu yeye alithibitisha kuwa huyu bwana akiwa na hela huwa kama kichaa na anasema kuna kipindi aliwahi kukaa Sheraton kwa zama hizo karibu siku nne akiwa na mwanamke na analipia pango na chakula.

Unaweza kuona jinsi hiyo nadharia ya mkono mtupu haulambwi ilivyo...
 

wos, percentage gani ya jamii yetu imezoea haya mambo............ usijijadili wewe, jadili jamii kwa ujumla wake...............

at the nd anapata relationship ambayo asingepata kama asingefanya hivyo............ na ni kubwa sana in terms of both self and social esteem kupita kwa mbali sana hasara itakayotokea.............
 

mkuu, nashukuru angalau umeona kitu hapo........ hapa kwenye hii thread watu wengi wanignore huu ukweli........... na wengine wanajijadili wao na maisha yao kwa vile tu wameishavuka huko tunakoongelea, wamesahau kuwa wao ni sehemu ndogo sana ya jamii yetu.......... sehemu kubwa ya mabinti leo hii wasingemudu kuendesha magari mjini, au hata kubadili nguo nk. ........kam si zawadi au tuseme kuhongwa na wanaume................
 
Yes ni hasara isipokuwa hali halisi iliyopo ni kuwa kina dada mara nyingi wanakosa imani kwa kijana asiyeweza kumove fast in terms of cash na mambo mengine yanayooneka yameshika chat kwenye jamii.Na ukwei wa mambo ni kuwa bila kufuata utaratibu na kujari kupata pesa tu ni rahisi kuharibu.
Kama demand ya dada kwa mpenzi wake ni mambo yanayotaka kuwa na kipato kikubwa unafikiri itakuwaje? Labda trend imeanza kubadilika sasa maana taratibu elimu na vipato vya wanaume na wanawake vinaonekana kushabihiana.
Pengine sasa na kina kaka waanze ku explore other mens zitakazowafanya kina dada wawe more attracted na mambo ya kawaida kawaida bila kuweka mbele pesa tu.
 

Sure,,,if it works for u use it....... hapa tunajadili one aspect of life kutokana na unafiki wa mtu kujua kabisa anafanya nini halafu anakuja hapa kutafuta validation ya anachokifanya..... sikatai kuwa kuna watu hutumia pesa na vivutio mbalimbali kupata kile watakacho na siyo kwenye mapenzi tu. Rushwa kutumika kupata utakacho pia, na sidhani tunaweza kutetea kuwa maadam inakufikisha utakako basi iachwe tu.Rushwa iwe ya pesa au ya mambo mengine itakuwepo na itaongezeka viwango kama tutaacha kuikemea. Likewise pesa kununua penzi kwangu mimi naona tunahitaji kuijadili .... mwenye kuona hana jinsi ya kupendwa kama binadamu mpaka atumie pesa too bad aendelee.Ila najaribu kuwaza.. unapokaa baadae ukafikiria kuwa hujapendwa wewe bali pesa yako unajisikiaje? Imagine unatafuta mchumba uoe awe mkeo.. ukishamuoa ukasitisha kumhonga humo kwenye ndoa unadhani hatima yake itakuwa nini - BIG QUESTION! THINK ABOUT IT! Kama ni mwanamke anayejiuza hiyo ni ishu nyingine ndio maana prostitution has always been there ( kulikuwa kuna mpaka temple prostitutes ambao walihalalishwa kabisa kama namna ya kuwasaidia wanaume wenye uhitaji ili wasiwehuke kama ulivyosema kwenye bandiko lako ( japo sijui kama kuna kuwehuka)


Siogopi hoja na ndio nimeshakujibu hapo juu.... ila kutokukujibu kwangu haikuwa na maana nimeogopa bali nilitaka watu wengine nao wachangie maana hii mada sijaihodhi ndugu yangu. ni free discussion.
Tofautisha zawadi na transactional " relationships" kama ni zawadi tu mbona watu wanatoa sana wanawake kwa wanaume. haina neno kabisa.


Huyu anayehonga mapato yake yote ili tu ampate mwanamke ana tatizo la self esteem na umeshaeleza vema.Akimaliza kuhonga then anarudi tena kuombaomba.... inakuwa mduara usioisha - Kuomba - kuhonga - kuomba - kuhonga..mwisho wake ni nini?
Hapo mwanamke yuko kazini - anaingiza kipato - mwanaume anateketeza kipato chake.
 

mbona toka enzi na enzi mambo yako hivyo mkuu??. mahusiano ni sehemu ya maisjha ya jamii na hua automatically,.......... jamii haiwezi kuelekezwa namna ya kuishi............ hujifunza yenyewe na hata social reconstructionists wanakiri kuwa jamii hubadilika yenyewe upon some influences...................
 

sasa unakaribia kukubali kuwa jamii ni complex kuliko ulivyotaka kui-frame......... nianze mwishoni, hata mimi napinga sana transactinal relationship ila ninazungumza kulingana na hali halisi ya jamii, sijijadili mimi binafsi, najadili jamii yangu.......... ukinielewa hapo........... basi tutaenda pamoja........hicho atoacho mwanaume huanza kutoa kama zawadi na baadaye utasikia dada akipigiwa simu baada ya salamu tu utasikia "....... dia sasa vocha leo vipi?..... hata buku basi yaani sina hata ya kubip"........ sasa hapo ndo zawadi zilizokuwa zikitolewa kwa nia njema ya zawadi tu, zinapokuwa zimegeka kuwa hongo syndrome, otherwise ilianza kama zawadi tu sio hongo.................

ukipata mchumba kwa kumhonga na kisha kumuoa, imetokea mara nyingi na hakuna utafiti uliotibitisha kuwa ukisitisha kumhonga humo kwenye ndoa kutaingia matatizo. ila ukweli ni kuwa ndani ya ndoa kuna maisha ya pamoja na hatusemi kuhonga, bali "kutoa matumizi" hilo ukisitisha huwa ndoa inachimbika hata kama mwanamke anacho kipato kizuri zaidi ya mume...............

nimesikitika kusikia hijui kama sex urge ikizgi inaweza kuleta wehu na hata kusababisha suicide!

sex urge si kitu cha kuchezea, kinazorotesha self and social esteem kiasi kwamba hushusha kiwango cha kujiamini na wakati mwingine huleta kutojithaminoi, kujichukia nk............ tote haya yakizidi, utasikia mtu kajikata uume, kabaka, kanajisi watoto, au hata kajiua............... tunahitaji utafiti wa kina sana kuweza kuelewa matatizo haya kwa kina katika jamii yetu..........
 
 
Now i know lol! Ila ni % ngapi wamewehuka, kujikata, kubaka....

ndio maana nasema tunahitaji utafiti wa kina katika suala hili.......... wengi wakisikia ubakaji nk. wanasema dunia imeisha, au mmomonyoo wa maadili nk. na kuishia kugenerarize kwa kauli kama hizo lakini ukiingia deep zaidi.............. unaweza hata kumshukuru Mungu kuwa alikuepusha na changamoto za kuwa mwaume katika dunia kama yetu................ jamii yetu inazungumzia zaidi masuala ya mwanmke na kusaidia kujenga uelewa wa kutosha upande huo, lakini mimi naamini kuwa hata uapande wa wanaume kuna mahitaji makubwa sana ya tafiti kufanyika kujua yaliyojificha humo.................
 
 
Itapendeza kama gender equality itaingia ktk vitendo zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…