Inasemekana bifu zito kati ya Mtendaji wa Shirikisho na Mmiliki wa Tabora United ndio sababu ya kucheza pungufu

Inasemekana bifu zito kati ya Mtendaji wa Shirikisho na Mmiliki wa Tabora United ndio sababu ya kucheza pungufu

Kanuni zipo ila ni za hovyo. Kama timu haijaingia uwanjani huwa inapigwa faini kubwa na kuzuiwa kushiriki hiyo ligi au mashindano.
Sasa kuruhusu mechi kuchezwa kwa timu moja kuwa na wachezaji 8 halafu bila faini au adhabu nyingine kwa hiyo timu hapo chama cha mpira kinafikiria nini? Vipi hiyo klabu ikiamua kwenda na mwendo huo huo wa kupeleka wachezaji pungufu na kusingizia wengine wanaumwa hiyo itakuwa na faida gani kwa ligi hata kama kanuni zinaruhusu?
Umejuaje kama kamati haitakuja na adhabu kwa Kitayoce kwa uzembe walioufanya?
 
Tff walikua wanalijua hili mapema walishindwa nn kuhairisha Mechi kwa kutumia busara tu,
Yaani TFF wakimbilie tu kuahirisha mechi wakati timu husika zipo tayari kuingiza vikosi na kucheza? Mbona mnajidai mnajua zaidi wakati mpo weupe kichwani? Unadhani Kitayosce walikuwa hawajui taratibu za kuahirisha mechi? Mbona mnawasemea wakati wao wanaona njia waliyotumia ni nzuri zaidi kuliko zote, na wala hawalalamiki?
 
Kwa issue ya jana karia amejivua nguo,
WAMEONEWA TU🙏

"Kuna team wachezaji wake 16 walipata mafua mechi ikaahirishwa wakati walikua na wachezaji 25 ukitoa 16 wanabaki 9 leo wachezaji 8 wameweza kucheza mechi ila 9 haiwezekani hii ndio TFF YA KARIA ligi yetu kivyetu vyetu"

NB: na bila aibu walikuwa wameendaa na watu wao wa kuongea kwenye media mchezo ukishindwa kumalizika 😅
 
TFF sijui wanafikiri vipi. Ilitakiwa mechi kuahirishwa bila kujali Tabora utd wamefungiwa na FIFA.
Yaani katika posts zote ya kwako ndio Ina mantiki kweli kweli. Wengine hawajui hata kosa ni nini wanailaumu TFF. Hawajui kuwa kosa ni Kitayose FC kushindwa kuwalipa wachezaji wake Asante Kwasi na mwenzake licha ya kupewa miezi minne wawe wamelipa. Na adhabu ya FIFA kwa kosa Hilo ni kufungwa usajili. Period!

Tunachoweza kuwalaumu TFF kama ulivyosema ni kwanini hawakuahirisha hiyo mechi?
 
Kanuni zipo ila ni za hovyo. Kama timu haijaingia uwanjani huwa inapigwa faini kubwa na kuzuiwa kushiriki hiyo ligi au mashindano.
Sasa kuruhusu mechi kuchezwa kwa timu moja kuwa na wachezaji 8 halafu bila faini au adhabu nyingine kwa hiyo timu hapo chama cha mpira kinafikiria nini? Vipi hiyo klabu ikiamua kwenda na mwendo huo huo wa kupeleka wachezaji pungufu na kusingizia wengine wanaumwa hiyo itakuwa na faida gani kwa ligi hata kama kanuni zinaruhusu?
Maana ake ziboreshwe zaidi
 
Kwa tukio lililotokea jana kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Azam FC Vs Tabora United NIMEUMIA sana nisiwe mnafki

Sio mm tu jamii yote ya Wapenda Soka imeumia kwa Utoto waliofanya Tabora United kuichafua ligi yetu, Ligi namba 5 kwa Ukubwa Afrika Mechi inachezwa kwa Dk 15 Aibu sana

TFF ni Baba wa Mpira wetu, na hivi Vilabu vyote ni watoto wake, Hivi mtoto akiunyea mkono unaukata? Tabora wameonesha utoto Tff walikua wanalijua hili mapema walishindwa nn kuhairisha Mechi kwa kutumia busara tu, Mbona kwa hizi Team kubwa busara hutumika sana au kwasababu Tabora United ni team ndogo?

Rejea tukio lililowakuta Simba Miaka miwili nyuma waliposafiri kwenda Kagera Wachezaji 12 kati ya 22 wakapata Mafua walibaki 10 wazima lakini Mechi ilihairishwa busara ilitumika!!! Why kwa jana imeshindikana??

Mchezo wa Yanga Vs Simba Miaka miwili nyuma ulihairishwa Kisa Muda tu kuleta changamoto mbona busara ilitumika ukapangiwa siku nyingine au kwasababu hawa ni Wakubwa!!

TFF sio nawalaumu ila mliweza kuzuia Aibu hii kuikumba ligi yetu lakini hamjafanya hivyo, Brand ya Ligi imechafuka walioichafua ni Tabora Utd na nyie Tff[emoji119]

Hongereni Azam FC kwa Ushindi, Hongera Feisal kwa Hattrick.
Kumbe wewe ni Oscar Oscar!
 
Zipo taarifa kuwa wachezaji wa kigeni wa Tabora United wote wana vibali vya kazi, kilichokosekana ni vibali vya makazi lakini kwa sababu wana business visa, wanaruhusiwa kucheza kwa muda hadi pale vibali vyao vitakapotoka. Kwanini leo hawajaruhusiwa kucheza? Kuna tetesi kuwa kuna bifu zito kati ya Mtendaji wa Shirikisho na mmiliki wa Tabora United!

Je, ingekuwa ni Simba au Yanga wakawa na issue hii wangeachwa wacheze wakiwa nane au mechi ingeahirishwa? Sina majibu. Wacha tu niendelee kulewa.

Unadhani aliyeathirika na huu “Utoto” wa leo ni Tabora United tu kupoteza points? Hapana. Mpira wote umeumia. Imagine watu wa betting, waliosafiri kwa ajili ya mechi, kama Azam atakuwa bingwa kwa tofauti ya alama tatu mwisho wa msimu, kama Feisal atakuwa Mfungaji Bora kwa tofauti ya mabao matatu! Mpira wote umeumia!

Imagine kuna raia wa kigeni alikuwa anaitazama ligi yetu kwa mara ya kwanza, kuna mtu alikuwa anataka kutoa sponsorship kwa moja ya timu zetu. Sina nia ya kutetea tabora kwa sababu ya unyumbani, nataka tuitazame issue hii kwa ukubwa wake.

Tabora United wana utoto wao wamefanya kwenye hili lakini, utoto wao kuna namna umekuwa utoto wetu sote. Ligi yetu inaonekana bado ina mambo ya kitoto. Kuna mtu leo angeweza kushawishika kulipia king’amuzi cha mwezi, baada ya utoto wa pale Azam Complex ameghairi!

Anyway, Mfaransa mmoja wa kuitwa François-Marie Arouet aliwahi kusema common sense is not so common! Hivi mechi ingepelekwa mbele mngepata dhambi?
Mpe credit zake oscar oscar haya maneno si yako kayasema yeye

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom