Inasemekana Cloud media inataka kumshuka Diamond kimziki kwasababu alikataa ofa ya kuwa chini yao

Sasa msanii wa kimataifa anashushwaje na Radio ya Ndani?
Labda we ndo utwambie diamond ana wimbo gani ulio hot hivi sasa alafu haupigwi ndo tujilidhishe? Je umeshasikiliza na radio nyingine kuona kama wanapiga nyimbo zake mara kwa mara? Hivi kwan clouds siku hizi ina manage wasanii? Mameneja wa wasanii ni babu tale, mkubwa fela ,ustadh n.k. sijawahi kusikia Ruge au Kusaga waki-manage wasanii. THT yenyewe Ruge ni mlezi tena wanajihusisha na wasanii wachanga ukimkuta msanii mkubwa basi ujue kakulia pale.
Fiesta kampuni ya serengeti ndo inayolipa wasanii moja kwa moja. Na hapo anayepatana ni Babu Tale wala sio Diamond.

Huwapa kick wasanii wengine kama njia ya kuongeza ushindani wala sio dhambi kwan inawafanya wasanii walioko juu kujituma zaidi na zaidi.

Muhimu unachotakiwa kuelewa Diamond wimbo wake wa mwisho ku-heat ni mdogomdogo toka hapo anatoa pumba tu matokeo yake hazimalizi miezi 2 kwenye soko zishachuja.
 

nakubaliana na wewe mkuu mi ni shabiki wa diamond ila wimbo mzuri kwangu wa mwisho ni mdogo mdogo baada ya hapo huo ntampata wapi umefunikwa redioni na hadi kwenye madaladala na nyimbo za kama pacha wangu, unanimaiza ya matonya na wakina yamoto band wamemfunika sana nyimbo zao kumpigwa mtaani
 
pia ni kweli alikiba apewa promo sana na clouds mara sijui ratiba zake za kuvaa mara jingle zake n.k......ni wakati wa diamond kutoa hit song nyingine ila sio kama ntampata wapi
 
Nyimbo mpya ya ali.kiba ni kali hatari. Yani ukichukua yale mapambio yote ya diamond kuanzia mbagala, nataka kulewa, my number one na taka taka zake zoote haifikii hii ngoma, Ally kiba ni mkali

Ati mapambio :what::what:
 
Wasipompa promo clouds na kupiga nyimbo zake, wala haina shida zitapigwa trace tv, sound city, Chanel o, MTV, UK, Ghana, Kenya, Uganda, na kwingineko!!

Hili ndo jibu sahihi kwa wanafiki na wachawi wote wapenda kufitinishana. Au watwambie ana wimbo gani unaohit na haupigwi?

Ukweli ni kwamba hata maskendo ya wanawake yamechangia kumfikisha hapo alipo.
 
Msiogope kivuli cha Mfalme Kiba, tulieni dawa iwaingie vizuri na mwaka mtasingizia mengi sana.
 

Hii tetesi ni uongo mtupu maana nilitegemea uoneshe kwa ushahidi jinsi Diamond alivyo kataa hiyo unayosema ni offer! Kwa hiyo ulikuwa utaki nyimbo za wasanii wengine zipigwe au kupewa promo? Hata hivyo mbona nyimbo za Diamond zinapigwa?

Wimbo wa Kiba unapigwa sana si Clouds pekee hata radio stations nyingine na kwakuwa ni hit song na watu wanauchagua sana..mimi naona lengo lako ni kumgombanisha Diamond na Clouds jambo ambalo si jema!

Hivi kuna kosa gani mtu akifanyiwa promo? Mnapenda sana kuwasingizia Clouds hata kwenye mambo yasiyo na msingi kabisa ..hivi kweli hata kwa akili ndogo Clouds wanawez kumshusha Diamond? Ili wapate faida gani?

Kuna kipindi watu walisha lalamika kuwa Diamond anapewa promo sana na Clouds lakini sasa hivi mnageuka mnaanza kusema wana mshusha pengine unafikiri kwa kuwa Kiba anapewa promo! Hivi kwanini msifikiri wana kuza muziki?
 
Nyimbo mpya ya ali.kiba ni kali hatari. Yani ukichukua yale mapambio yote ya diamond kuanzia mbagala, nataka kulewa, my number one na taka taka zake zoote haifikii hii ngoma, Ally kiba ni mkali

Hahaha hahaha hahaha duh watu Jaman kwaio zile nyimbo zote n takataka
 
Clouds FM na Diamond wote ni wahanga wa uzushi dhidi yao ndani ya nchi hii!! Haidhuru leo tunasikia kuhusu Clouds lakini baada ya muda tutasikia hili ama lile kuhusu Diamond! Kwa mtu anayeifahamu music industry ya Tanzania anafahamu ni nyimbo ngapi radio stations wanapokea kwa siku... kwa asiyefahamu, tunazozisikia hazifiki hata robo ya zile zinazopokelewa! Tukichukulia Clouds kwa mfano, nyimbo ambazo wanapokea kwa siku zinatosha kabisa kutumika kwenye kipindi kizima cha XXL bila kuongezea na nyimbo zilizopokelewa jana yake... hii ni kuonesha jinsi gani wanavyopokea nyimbo nyingi kwa siku! Ukienda studio kurekodi, inaweza kukuchukua mwezi mzima kutokana na uwingi wa watu wanaotaka kurekodi kama wewe!

Sasa basi, katika mazingira kama hayo usitarajie kwamba nyimbo au wimbo wa msanii fulani utausikia mara kwa mara... iwe Diamond, Ali Kiba, Weusi au yeyote yule hususani ikiwa hakuna wimbo mpya uliotolewa na msanii/wasanii husika! Kwa mazingira ya Bongo Flavor, kutokana na nyimbo zinavyofyatuliwa kila siku, nyimbo iliyotoka mwezi mmoja uliopita na sifa zote za kuitwa ya zamani!
 
Clouds wapo busy na Chekecha chekecho, wanajitahidi kwa kila hali kulipaisha chekecho lao.
 
Diamond ameshashift kutoka kuwa local Artist hadi kuwa Mega Super Star kwahyo usishangae Local radios kupunguza promo kwa sababu wanajua Diamond hahitaji sana kick kutoka radioni ...

Kitu kingine ni kwamba Diamond yupo pamoja clouds media kama kawaida na nguvu yake kwenye mitandao na magazeti ni kubwa sana kuliko mtu yoyote hapa Tz... Kwahyo tuseme hata clouds radio wapige huo wimbo wa mchekecho 24/7 haitamuathiri daimond technically
 
Hivi kwa nini kila anapoongelewa diamond lazma watu wamhusishe ali kiba na akiongelewa ali kiba watu wanamhusisha diamond? Kwa nini watu wanadhani kupanda kwa kiba ni kushuka kwa diamond? Kwa nini kupewa promo kiba ionekane ni kumuonea diamond?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…