ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Nchi ipo katika kipindi cha maandalizi ya mipango na bajeti ya 2020/2021. Utaratibu unataka taasisi za serikali na mawakala kuanza mchakato wa maandalizi wa mipango na bajeti zao mara baada ya Wizara ya Fedha na Mipango kutoa mwongozo wa uandaaji wa bajeti kwa mwaka husika, mwongozo wa maandalizi nadhani ulishatolewa.
Turudi kwenye mada, Halmashauri nyingi zimeshusha makadirio ya makusanyo ya mapato ya ndani (own source) kwa zaidi ya 25%. Wako wakurugenzi wajanja walioshusha mapato ya ndani halisi (proper) na kuongeza mapato ya ndani fungwa (protected), na kundi la pili wameshusha mapato halisi (own source proper) wameongeza nguvu za wananchi (community contribution).
Tukianza na kundi la kwanza ni kundi ambalo wakurugenzi wake wamejaribu kuwahadaa wananchi. Hawa ni wale wakurugenzi ambao hawapendi stress ya kupigiwa kelele kila siku na waziri wao kwamba wanakusanya chini ya wastani, pamoja na kundi la pili pia.
Sasa TUNAOMBA wachumi na watalaamu wa masuala ya bajeti waje watuambie halmashauri kushusha bajeti zao za makusanyo ya mapato ya ndani ni ishara kwamba uchumi wa wananchi wao na vipato vyao vimeshuka? Lakini pia waje watuelekeze uhusiano uliopo kati bajeti na ukuaji wa uchumi.
Tunachokizungumzia ni mapato ya ndani halisi (own source proper) kwa sababu mapato haya ndio makusanyo yake yanakwenda moja kwa moja kuhudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya mashule, zahanati na hata kuhudumia vikundi vya wajasiriamali wadogo wadogo vya wanawake, walemavu na vijana. Athari zake ukishusha own source proper unaenda kuathiri moja kwa moja shughuli zinazogusa maisha ya wanyonge walio wengi.
Labda TAMISEMI wangetusaidia kutuainishia sisi wananchi kwa kila Halmashauri mapato ya ndani halisi (proper) mwaka 2019/20 ilikuwa ngapi na 202/21 ilikuwa ngapi kwa sababu sisi wananchi wa kawaida tukiuliza kwa fedha za vikundi na miradi imeshuka tunapewa majibu mepesi sana huku kwamba vitambulisho vya Rais Magufuli vimechukua baadhi ya vyanzo.
He ni kweli au ni uzembe tu au wanataka kutugombanisha sisi wananchi wa kawaida na serikali yetu.