MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Haya mambo ya biashara hayana kanuni inayoeleweka. Siku za karibuni kuna jamaa yangu kaanzisha biashara ya kuku wa kienyeji ila ufanyaji wake wa biashara ni wa kushangaza sana. Kwanza bei zake ni kubwa kulinganisha na bei ya soko. Pia ukienda kwake kununua kuku unamkamata mwenyewe bandani. Banda lake ni kubwa kama chumba cha square meter 18. Kuna kukimbizana na kuku kidogo. Pia anavyopost Insta na FB huandika kwa majivuno.
Kwa mfano niliona kaandika kuwa watu wasiseme kuwa wanamsapoti kwa sababu na wao pia wanaondoka na kuku wake. Kingine ni kuwa kama unataka kuku kesho usimsumbue kwa kumpigia simu leo. Yaani ni tafrani.
Ingawa jamaa ana vyanzo vyake vingine vya mapato ila hiyo biashara yake anafanya kwa style hiyo na kupata wateja kibao. Binafsi nimekulia Arusha na kujionea wafanyabiashara wengi wasiobembeleza mteja lakini ndo kila siku wanafanikiwa. Huwa ninashangaa.