Inashangaza sana: Blagnon nje, Juma Luizio ndani

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kuna kipindi huwa nacheka tu. Pale nionapo Usajili wa kukurupuka unaofanywa na Klabu ya Simba.
Najiuliza ni nini huwa wanafikiria hasa pale wafanyapo usajili wa wachezaji wapya.

Tatizo kubwa sana ambalo wamekuwa nalo tangu Tambwe awanyooshee mkono wa kwa heri, ni nafasi ya Ushambulizi.

Ila cha ajabu zaidi ni pale wanapopata mshambuliaji mwenye ubora wa wastani na kushindwa kukaa naye kwa kipindi kirefu.

Mimi binafsi sikuona Tija ya kumuondoa Blagnon. Basi tukadhani kuwa kunafanyika usajili wa Upgrade. Yaani kuleta kilicho bora zaidi. Nilishtuka na kupigwa na butwaa baada ya kusikia Juma Luizio kutoka Zesco ndio anakuja kuchukua nafasi ya Blagnon. Kwa lugha nyingine ni kwamba yeye ni bora kuliko Blagnon.
Tukiwa tunasema pengine ukawa ni usajili mzuri, tukumbuke kuwa Juma Luizio si mshambuliaji na haijawahi kuwa mshambulizi wa kutegemewa huko Zesco. Alikiwa ni mchezaji wa ziada, na amepata kucheza mechi chache sana akiwa ameanza.

Je anaweza kuwa na impact zaidi ya ile ya Blagnon?

Ukisikia usajili wa Kamari/Kubahatisha ndio huu sasa.

Ninachokiona ni kwamba mzunguko wa pili Simba itafunga mabao machache sana kuliko mzunguko wa kwanza. View attachment 446316View attachment 446317

Juma Luizio amezaliwa mwaka 1997 - Ana miaka **
 
Acha umbea ww inakuhusu nini maswala ya simba
Mkuu... Huo ndio ukweli. hata kama hutopenda kuusikia lakini hamna namna
.
.
Hutoweza kubeba ndoo ukiwa na Juma Luizio mbele.... Akisaidiana na Atanasi..

Ukizingatiza Mavugo hali yake unaijua. [emoji23]
 
Wanamrudisha Danny Serunkuma. Kipa wao ndiyo alikuwa bora kitakwimu mzunguko wa kwanza lakini katemwa. Hadi huyu mpya akae sawa, watakuwa nafasi yao ya kawaida - ya tatu au nne!
 
Kwa kweli Hanz popo ni kama amechanganyikiwa hivi au ana iq ndogo kinoma, eti anahoji ni kwa nini blagon alalishindwa kuifunga yanga dakika za lalasalama akiwa yeye na dida
Eti na wewe kipa ni kwa nini Prison wamekufunga goli 2 za krosi 'utufahi!!!'
 
Mkuu... Huo ndio ukweli. hata kama hutopenda kuusikia lakini hamna namna
.
.
Hutoweza kubeba ndoo ukiwa na Juma Luizio mbele.... Akisaidiana na Atanasi..

Ukizingatiza Mavugo hali yake unaijua. [emoji23]
Mdau ulichosema ni sahihi. Ilitakiwa Simba wampe muda Blagnon. Ni aina ya washambuliaji wanaotisha akikaa namba 9. Yaani hata asipofunga yeye mwingine atafunga. Duru la pili muda utaongea wakuu.
 
Kwa Angban wamechemka, ndo kipa bora round ya kwanza, magori 2 yamemponza, anarudi kwao
 
Haya mambo ya usajili Katika hizi timu zetu hua nashindwa kuyaelewa kabisa,hua sijui ni nani hasa anaehusika na usajili WA wachezaji lakini kwa mtazamo WA kawaida tu unaona kabisa kua kuna vitu haviko Sawa!
 
Kama ni kweli nitashangaa sana, sana. Hakuna sababu ya msingi kumwacha Angban wala Blagnon ktk mzunguko huu.
 
Wenye kadi za chama wamekubaliana ww mtu baki povu la nn tulia mkuu tumekuja kuwashiiiiiika
 
Mdau ulichosema ni sahihi. Ilitakiwa Simba wampe muda Blagnon. Ni aina ya washambuliaji wanaotisha akikaa namba 9. Yaani hata asipofunga yeye mwingine atafunga. Duru la pili muda utaongea wakuu.
Jamaa alikuwa ameshaanza kuizoea ligi. Sasa wameleta hawa wapya.... Subiri pale watapo fanya vibaya kwenye mechi zao.

Wataanza kuilaumu Yanga kuwa inabebwa.. [emoji23]
 
Kwa Angban wamechemka, ndo kipa bora round ya kwanza, magori 2 yamemponza, anarudi kwao
Ngoja tuone huyu atadakaje ile mipira ya kudunda dunda kwenye viwanja vya mikoani.... [emoji23]
 
Kama ni kweli nitashangaa sana, sana. Hakuna sababu ya msingi kumwacha Angban wala Blagnon ktk mzunguko huu.
Anza kushangaa mapema ili wakati ukifika wa kushangaa usije ukazimia.. Hahahah

Viongozi wenu wamefanya panick buy. [emoji23]
 
Wenye kadi za chama wamekubaliana ww mtu baki povu la nn tulia mkuu tumekuja kuwashiiiiiika
Utamshika nani ligi hii ukiwa na athanas na Luizio?

Wakati wenzako Yanga wana Tambwe na Ngoma. [emoji23]

.
.
.
Endelea kuota Ubingwa!
 
Kuna kipindi huwa nacheka tu. Pale nionapo Usajili wa kukurupuka unaofanywa na Klabu ya Simba.
Najiuliza ni nini huwa wanafikiria hasa pale wafanyapo usajili wa wachezaji wapya.

Tatizo kubwa sana ambalo wamekuwa nalo tangu Tambwe awanyooshee mkono wa kwa heri, ni nafasi ya Ushambulizi.

Ila cha ajabu zaidi ni pale wanapopata mshambuliaji mwenye ubora wa wastani na kushindwa kukaa naye kwa kipindi kirefu.

Mimi binafsi sikuona Tija ya kumuondoa Blagnon. Basi tukadhani kuwa kunafanyika usajili wa Upgrade. Yaani kuleta kilicho bora zaidi. Nilishtuka na kupigwa na butwaa baada ya kusikia Juma Luizio kutoka Zesco ndio anakuja kuchukua nafasi ya Blagnon. Kwa lugha nyingine ni kwamba yeye ni bora kuliko Blagnon.
Tukiwa tunasema pengine ukawa ni usajili mzuri, tukumbuke kuwa Juma Luizio si mshambuliaji na haijawahi kuwa mshambulizi wa kutegemewa huko Zesco. Alikiwa ni mchezaji wa ziada, na amepata kucheza mechi chache sana akiwa ameanza.

Je anaweza kuwa na impact zaidi ya ile ya Blagnon?

Ukisikia usajili wa Kamari/Kubahatisha ndio huu sasa.

Ninachokiona ni kwamba mzunguko wa pili Simba itafunga mabao machache sana kuliko mzunguko wa kwanza. View attachment 446316View attachment 446317

Juma Luizio amezaliwa mwaka 1997 - Ana miaka **
We ngoja simba ikose ubingwa halafu uone kama patakalika pale nanihii
 
Back
Top Bottom