Inashangaza sana Jiji la Arusha linatoa ajira kwa watumishi wa Umma ilhali kuna watu wengi ambao hawana ajira

Inashangaza sana Jiji la Arusha linatoa ajira kwa watumishi wa Umma ilhali kuna watu wengi ambao hawana ajira

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,150
Reaction score
3,225
Huu ni utani na wananchi ambao hawana ajira. Jiji la Arusha mlifikiria hili mkiwa wazima wa afya. Enyi serikali hebu wajarini wananchi wenu kwa usawa.

Watu hawana ajira, inatokea ajira ya muda badala muwape ajira wasiokuwa na ajira mnawapa wenye ajira?Wacha tukae bila ajira Wala pesa. Tutashinda huku mitandaoni kuwasema hadi mlewe. Wabinafsi wakubwa nyie. Keki ya Taifa hamtaki kutugea na sisi wananchi.

wananchi wenzangu, nafasi za kazi hizo hapo...lakini ni kwa watumishi tu.
IMG-20240925-WA0494.jpg
 
Sehemu zote nilizosikia wanahitajika watumishi wa umma pekee.
 
Ukiharibu kazi watakupata wapi mkuu, lengo ni kazi ifanyike kwa ufanisi na watumishi wa serikali ambao wapo interested na sio kutoa kazi kwa kigezo tu kuna watu hawana ajira
 
Huu ni utani na wananchi ambao hawana ajira. Jiji la Arusha mlifikiria hili mkiwa wazima wa afya ama mlikuwa mmekunywa rubisi?? Enyi serikali hebu wajalini wananchi wenu kwa usawa. Watu hawana ajira, inatokea ajira ya muda badala muwape ajira wasiokuwa na ajira mnawapa wenye ajira??? Wacha tukae bila ajira Wala pesa. Tutashinda huku mitandaoni kuwasema hadi mlewe. Wabinafsi wakubwa nyie. Keki ya Taifa hamtaki kutugea na sisi wananchi.
WANANCHI WENZANGU, NAFASI ZA KAZI HIZO HAPO...LAKINI NI KWA WATUMISHI TU.
Kuna sifa ambazo mtumishi wa umma anakuwa nazo tayari. Ukihitaji watu walioko nje ya Utumishi wa umma, bajeti itaongezeka zaidi hasa ya recruitment na mafunzo. Bajeti hiyo ingetoka kwenye pesa za walipakodi, miradi ya maji, umeme, viwanja vya ndege, ajira mpya, barabara na kadhalika, ingeathiriwa.
 
Umemaliza, hapo bado orientation maana hiyo kazi ni "special assignment", ukimchukua mtu nje ya mfumo anajikuta hata taratibu za kawaida za utendaji kazi wa serikali anakuwa hajui vizuri
 
Ushetani uso tija. Ila Yana nwisho. Mhe. Deo Sangu NW Utumishi aliwaambia wazi kwamba suala la ajira Lina impact ya Moja Kwa Moja Kwenye usalama wa nchi alipoenda kagua panel ya usail wa afya Arusha lkn naona hao walikuwa wanamng'ong'a
 
Huu ni utani na wananchi ambao hawana ajira. Jiji la Arusha mlifikiria hili mkiwa wazima wa afya ama mlikuwa mmekunywa rubisi?? Enyi serikali hebu wajalini wananchi wenu kwa usawa. Watu hawana ajira, inatokea ajira ya muda badala muwape ajira wasiokuwa na ajira mnawapa wenye ajira??? Wacha tukae bila ajira Wala pesa. Tutashinda huku mitandaoni kuwasema hadi mlewe. Wabinafsi wakubwa nyie. Keki ya Taifa hamtaki kutugea na sisi wananchi.
WANANCHI WENZANGU, NAFASI ZA KAZI HIZO HAPO...LAKINI NI KWA WATUMISHI TU.
Ipo hivyo nchi nzima.
Hata hivyo hapakuwa na sababu ya kuwataka kutuma maombi, wangteua tu na kuwapangia vituo maana watumishi wote wa umma wana sifa!
 
Mtumishi wa umma anakuwa tayari kwa kazi kwa sababu anajua how the chain flow. Hakuna vetting itakayohutajika. Kuna matukio katika nchi yanakuwa yameungana kwa namna moja au nyingine na national security. Matukio kama usimamizi wa mitihani ya kitaifa, uandikishaji wa wapiga kura, usimamizi wa upigaji kura, hata sensa yote yanakaribiana na national security. Kwa hiyo kuchukua watu na kulipia lupus, kisa ajira, mimi binafsi naona sio sawa. Ajira zipo na karibia kila wiki sekretriat ya ajira katika Utumishi wa umma, wanatangaza nafasi za kazi za umma. Achilia mbali private sector.
 
Ipo hivyo nchi nzima.
Hata hivyo hapakuwa na sababu ya kuwataka kutuma maombi, wangteua tu na kuwapangia vituo maana watumishi wote wa umma wana sifa!
Nadhani wanafanya hivyo kujua ambao wapo interested though hoja yako ya kuteua ni nzuri kwa maana kwamba wanateua miongoni mwa hao walio-apply.
 
Labda majobless hawawaamini.
Hapo kwenye sifa "A" & "B" kwani mtumishi wa umma anaruhusiwa kujihisisha na maswala ya siasa ? Ama unaweza kuwa kada ila ujihisishi na siasa?

Yes anaruhusiwa nje ya Muda wa kazi
 
Back
Top Bottom