Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mji wa Tanga ulijengeka kwa haraka baada ya kutua mjerumani na moja ya kitu alichoacha alama kwenye mji wa Tanga ni kupanga mji kwa barabara 21. Miaka kadhaa nyuma nilifanikiwa kuishi kwenye mji huu kwa siku chache wakati huo google maps ndio inaanza kuwa maarufu nchini.
Pamoja kwamba wenyeji wa Tanga walikuwa wakarimu sana kumuelekeza mtu sehemu anayokwenda, nilipenda sana kutumia ramani ya kwenye simu, kama kitu kipo kwenye ramani hakika utafika vizuri bila kuzunguka zunguka
Miaka zaidi ya 100 sasa, pamoja na kuwa tunacho chuo cha Ardhi na kila mwaka kinatoa graduates, wengine wako nyumbani bila shughuli za kufanya wakati miji mingi mipya inaota kama uyoga nchini tena kiholela mpaka kukosekana njia za kufika.
Maeneo yanakinai kuyaona machoni hata ikitokea dharura kufika baadhi ya sehemu ni changamoto.
Yaani tunashindwa kufanya kitu wenzetu walichoweza miaka 100 iliyopita pamoja na maendeleo makubwa ya teknolojia kwenye namna na vifaa vya kufanya kazi hiyo ya kupanga mji.
Nini kimetushinda sisi waswahili kupanga miji yetu?
Mji wa Tanga