Inatia kinyaa na hasira: Abdi Banda adai Simba inamtaka

Inatia kinyaa na hasira: Abdi Banda adai Simba inamtaka

nzagambadume

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2018
Posts
2,430
Reaction score
5,779
Kama ni kweli Simba wanambembeleza yule, i will dedicate my time kuitukana simba na kuhamia utopolo kwa mkopo, this is absurd.

Yani huyu mtu aliyeondoka simba kwa matusi akafanya interview huko South Africa na kusema Simba inashirikiana na serikali ya Tanzania ku-fake vipimo vya corona, Simba inahonga marefa na akaipa Kaizer Chiefs mbinu za ushindi.

Who knows hata huko South Africa kuna mambo alifanya nyuma ya pazia tukapigwa goals nne? Are we that desperate? CEO wa Simba na nyie kina magori kama ni kweli basi subirini show tamu sana maana naona mmekosa mikikimikiki kwa muda mrefu.

========

More by this Author

MWANASPOTI limefanya exclusive na beki huru Abdi Banda kujua ukimya wake unatawaliwa na nini baada ya kuachana na Baroka ya Afrika Kusini aliyoichezea tangu mwaka 2017-19.

Banda anafunguka mambo mengi, ikiwemo tetesi zilizokuwa zimeenea za kugombana na aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike pia namna alivyoweza kuyafikia malengo yake ambayo alijipangia akiwa mtoto.

Banda alikwenda kucheza Afrika Kusini akitokea Simba aliyojiunga nayo msimu wa 2014-17, iliyomsajili kutoka Coastal Union ya Tanga, anasimulia mambo mbalimbali kama ifuatavyo.

ISHU YAKE YA USAJILI SIMBA
Banda anasema waajiri wake wa zamani ni miongoni mwa klabu ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili kwa kuongea na wakala wake ambaye ni raia wa Uingereza anaishi huko Bondeni, Afrika Kusini, “Amenigusia kwamba walimpigia simu.

“Baada ya kunieleza kila kitu kilivyokuwa kwenye mazungumzo, aliniuliza unasemaje kwenye hilo? nilimwambia tuendelee kuwasikilia maana haikuwa klabu pekee ambayo imeonyesha nia ya kutaka kunisajili,” anasema beki huyo.

Vipi kama watafika dau? Banda anasema maisha ya mpira yana mwisho hivyo hatakuwa na chaguo jingine zaidi ya kuchangamkia ofa yao, “Tunacheza mpira ikiwa ni sehemu ya utafutaji, ndio maana ikitokea ofa huwa zinawekwa mezani halafu unafanyika mchanganuo ndio uamuzi wa mwisho unafanyika,”

“Naweza kurudi nyumbani na kucheza soka ikiwa kutakuwa na maslahi makubwa zaidi ya huko nje ambako ndio shabaha yangu kubwa,” anasema.

HAIKUWA RAHISI KUONDOKA SIMBA
Wakati wa mashindano ya COSAFA, 2017 nchini Afrika Kusini ndio kipindi ambacho Banda alifanya uamuzi wa kujiunga na Baroka FC, ilikuwaje? Banda anasema iliwezekana kukamilika kwa uhamisho wake huo kutokana na malengo aliyojiwekea.

“Nakumbuka Mo alitaka niongeze mkataba lakini ilibidi nimzungushe kwa sababu nilikuwa na mipango yangu mingine, msimu huo ulikuwa mzuri kwangu licha ya kwanza maisha yangu ndani ya Simba mwanzoni yalikuwa na changamoto nyingi.

“Kipindi ambacho Mo alitaka niongeze mkataba ilikuwa kabla ya COSAFA, nilikuwa nikimkwepa kwa kumwambia ajenti wangu hayupo hivyo nisingeweza kuongeza mkataba mwenyewe, ni kweli hakuwepo lakini tulikuwa na makubaliano ya kwamba nisiongeze mkataba kwa sababu kulikuwa na dili nyingine kubwa sana Afrika Kusini.

“Sikuondoka kwa ubaya nadhani viongozi wanatambua maisha ya mpira yalivyo nikiwa Afrika Kusini kwenye mashindano ya COSAFA, nilionana na ajenti wangu tukiwa hotelini sehemu ambayo alinielekeza na nikasaini mkataba wangu wa kwanza wa kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, ilikuwa ni furaha kubwa sana kwangu,” anasema.

MAISHA YAKE SAUZI
Mwaka wa kwanza (2017) aliojiunga na Baroka FC haukuwa mrahisi kwake, anaeleza aliutumia kuyazoea mazingira kama hali ya hewa ya baridi kali, vyakula na staili yao ya maisha ya kutokusaidiana tofauti na Tanzania watu wanavyoishi kijamaa.

“Afrika Kusini hawana kusaidiana, kila mtu na maisha yake iwe unaumwa unatakiwa kwenda mwenyewe hospitali bila kutegemea kuna mtu atakuja kukuona kama tulivyozoea hapa kwetu, hivyo mwaka wa kwanza ulikuwa mgumu ila sikukata tamaa;

Anaongeza kuwa, “Kwa kuwa nilikuwa na malengo yangu na nilijua kitu kilichonipeleka Afrika Kusini nilikubaliana na mazingira halisi ya nchi ile, kisha nikaendelea na majukumu yangu ya kufanya kazi,” anasema.

WASAUZI WALIVYO
Banda hashangazwi na maisha anayoishi winga wa Simba, Benard Morrison ambaye alikaa muda mrefu Afrika Kusini kwamba maisha yao hayana kufuatanafuatana, ili mradi tu anaonyesha uwezo wa hali ya juu uwanjani inakuwa imetosha.

Anasema wachezaji wa nchi hiyo, hawapendi maisha ya kambini kwasababu wanaona wanabanwa na kushindwa kupata muda wa kufanya starehe.

“Tanzania wachezaji wanajifichaficha kunywa pombe, Afrika Kusini mchezaji analewa mbele ya makocha na mabosi wake ili mradi tu awe anaonyesha kiwango cha juu uwanjani, ndio maana hawapendelei maisha ya kukaa kambini;”

Anaendelea kusimulia kwamba “Nilipewa kitambaa cha unahodha kwasababu nilikuwa najituma kwa bidii katika mazoezi na waliona sina aina yao ya maisha ya kulewa na kupenda starehe kama wao, hivyo walikuwa wananifurahia kuniona naisaidia sana timu,” anasema.

ISHU YAKE NA AMUNIKE
Wakati akiichezea Baroka FC kabla ya kwenda Highland Park, iliripotiwa kuwepo kwa tofauti baina ya Banda na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa la Tanzania ‘Taifa Stars’ na ilikuwa kipindi cha maandalizi ya mchezo wa kuwania nafasi ya kwenda kwenye fainali zilizopita za Afcon Misri dhidi ya Lesotho.

“Watu walizusha tu, kiukweli kabisa sikuwa na tatizo lolote na kocha, kuna watu walizusha maneno, ilikuwa hivi, wakati tukiwa kwenye maandalizi nilishauri tufanye mazoezi muda ambao niliona unafaa kutokana na kufahamu kwangu hali ya hewa ya Afrika Kusini.

“Kitendo hicho kilibebwa na kiongozi mmoja ambaye nadhani hakunielewa nini nililenga na ikaonekana kwamba najiona kuwa mkubwa kitu ambacho hakikuwa sawa, nilijisikia vibaya kwa yaliyokuwa yakiendelea lakini niliweka maslahi ya taifa mbele na nilikuwa mstari wa mbele kuwasapoti wenzangu na mwishowe tulienda Misri,” anasema.

KILICHOMRUDISHA TANZANIA
“Nilirudi Tanzania kuweka sawa mambo yangu huku nikisubiri dirisha la usajili Afrika Kusini lifunguliwe, naweza kurejea Sauzi siku yoyote lakini kilichosababisha nirudi ni kwa sababu timu ambayo nilikuwa nikiichezea Highland Park iliuzwa,” anasema.

MKEWE ACHOMBEZA
Kama mlidhani Banda na mkewe Zabibu Kiba, wametengana, basi habari hii inakuhusu. Wawili hao ndio kwanza penzi lao liko moto, huku wakiendelea kumlea binti yao Naifaty.

Zabibu, ambaye ni dada wa supastaa wa Bongofleva, Ali Kiba, anasimulia jinsi ambavyo anamsaidia mume wake kuwa mchezaji wa kuigwa katika kuonyesha kiwango cha hali ya juu na anatamani aendelee kusaka timu za kucheza nje ya nchi kama atapata fursa.

“Mfano kipindi hiki ambacho alikuwa nyumbani kutokana na kusumbuliwa na majeraha, alikuwa anapata mawazo mengi, nilikuwa najitahidi kumjenga na kwamba atarejea tena kufanya kazi zake, ikumbukwe kwamba soka ndio ajira yake.”

Anaongeza kuwa, “Kuna wakati alikuwa anakosa amani kabisa, nilikuwa nambembeleza kwa maneno mazuri, nilijiepusha kufanya vitu vya kumkera ambavyo vingekuwa vinamuweka kwenye mudi mbaya.”

Anaulizwa je mwanao unapenda afanye kazi gani akikua? Anajibu kwamba anatamani mtoto wao aje asome isipokuwa hawezi kumchagulia kazi na kwamba angekuwa mwanaume angecheza soka kama baba yake.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Simba hatukupigwa zile goli nne kwasababu ya Banda, ni uzembe tu wa beki zetu.
ungesoma ile interview aliyoifanya kule south africa usingeongea hivyo? kama hii nchi ingekuwa serious alitakiwa awe mahakamani sasa hivi kutoa ushahidi jinsi wizara ya afya inavyoshirikiana na simba sc kuchezea vipimo vya corona vya wapinzani ,akasema pia simba inatumia hela ku influence maamuzi ya serikali na kuhonga waamuzi.
HUYO NDIYE MTU AMBAYE SIMBA WANAONA NI SAHIHI KURUDI PALE....FAKENI KABISA
 
Hata mimi nimeshangaa kama kweli wanamtaka banda ni heri Kilomoni arudi wanahangaika na mchezaji asiye na umuhimu wowote tena aliondoka Simba kwa nyodo haya yatakuwa kama mambo ya kumsajili Ajib wakati hakuwa anahitajika
 
Hata mimi nimeshangaa kama kweli wanamtaka banda ni heri Kilomoni arudi wanahangaika na mchezaji asiye na umuhimu wowote tena aliondoka Simba kwa nyodo haya yatakuwa kama mambo ya kumsajili Ajib wakati hakuwa anahitajika
wako wengi waliiondoka kwa nyodo ila huyu kijana ni level nyingine...nyosso aliondoka kwa dharau kwenda coast union iliyokuwa na hela za bin slum, Hassan kessy pia ambaye alijaribu hata kuwapeleka nkana kwa mganga wa simba ila atleast yeye alikuwa aanachezea nkana

Huyu boya kuna hata mechi ya simba vs yanga alijipatisha red card makusudi simba ikapoteza na akaondoka kwa dharau sana ila mimi kilichoniuma ni ile interview aliyofanya huko south africa...dah yaani hata kwenye comments za kaizer chiefs fans kwenye social media walikuwa wanaitumia kama reference(ETI A SIMBA FORMER PLAYER KASEMA SIMBA WANAHONGA MAREFA NA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KU TAMPER NA COVID 19 RESULTS)

WHOEVER ANAPIGIA DEBE HUYU BOYA ARUDI PALE APATE HATA AJALI YA GARI LEO AFE KABISA, USELESS DUNDERHHEAD.
 
HUYO HANA NAFASI PALE MSIMBAZI. KWANZA ATACHEZA NAMBA NGAPI?
cha kushangaza kuna majitu pale klabuni yanataka arudi....ni bora kumuamini ame ibrahim na kennedy wapewe mechi 3 za mwisho za ligi wacheze pamoja wote warefu,akishauzwa luis hiyo nafasi pamoja na kuondolewa chikwende ijazwe na moses phiri na kiungo mkbaji mrefu lenye mwili ikishindikana wamrudishe Fraga
 
ila wabongo tuachen mihemuko na tuangalie mpira wetu wa sasa.. we kabisa kwa akili ya kawaida unaona kabisa huyo banda hana namba sio tu simba hata yanga na azam hapat namba..

bado mnatokwa povu na tetesi mnasahu kuwa kupind hiki wachezaj na mawakala wana mbinu nying ili mchezaj ajiuze lazima aseme anatakiwa na team kubwa
 
ungesoma ile interview aliyoifanya kule south africa usingeongea hivyo? kama hii nchi ingekuwa serious alitakiwa awe mahakamani sasa hivi kutoa ushahidi jinsi wizara ya afya inavyoshirikiana na simba sc kuchezea vipimo vya corona vya wapinzani ,akasema pia simba inatumia hela ku influence maamuzi ya serikali na kuhonga waamuzi.
HUYO NDIYE MTU AMBAYE SIMBA WANAONA NI SAHIHI KURUDI PALE....FAKENI KABISA
Hii ndo Simba, huo ni mkakati maalum kama ule wa Ajibu. Ukisikia banda kasaini msimbazi basi deal done, ndo mwisho wa karia yake.
 
Hii ndo Simba, huo ni mkakati maalum kama ule wa Ajibu. Ukisikia banda kasaini msimbazi basi deal done, ndo mwisho wa karia yake.
Kwa hiyo mnataka kumkomoa sababu mnamuogopa sana kwa kiwango chake ama? Na kama ni hivyo basi mnaendesha timu kishamba na kiswahili sana!
 
ungesoma ile interview aliyoifanya kule south africa usingeongea hivyo? kama hii nchi ingekuwa serious alitakiwa awe mahakamani sasa hivi kutoa ushahidi jinsi wizara ya afya inavyoshirikiana na simba sc kuchezea vipimo vya corona vya wapinzani ,akasema pia simba inatumia hela ku influence maamuzi ya serikali na kuhonga waamuzi.
HUYO NDIYE MTU AMBAYE SIMBA WANAONA NI SAHIHI KURUDI PALE....FAKENI KABISA
Vipimo vililalamikiwa sana hata na timu pinzani. Kuhusu kushawishi timu hili liko wazi, hata majuzi msemaji wa Azam football club alieleza namna Simba iliishinikiza Azam wapambane kiume kwenye mechi yao na Yanga. Kwenye kutoa rushwa naamini unayakumbuka ya Ulimboka alivyokamatwa akitoa rushwa kwa Mtibwa Sugar. Kulikoni kumtukana Banda ambaye amecheza Simba na anaijua vizuri, tungejibu hoja zake kwa weledi.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Banda hawezi kupata namba kwenye Simba hii ya sasa hivi. Kipindi hiki ndio kipindi cha mavuno kwa waandishi wa habari za michezo kwa kucheza dili na mawakala ili wawapaishe wachezaji wao. Kwa umakini wa Simba kwenye usajili kwa misimu miwili iliyopita sitegemei wafanye kosa kubwa la kiufundi kama hilo. Hivi timu ina Ame, Onyango, Erasto, Kennedy, Wawa n.k. na wapo kwenye viwango vizuri halafu umlete Banda wa nini na acheze wapi. Mbaya zaidi pamoja na kiwango chake kuwa kidogo kulinganisha na mabeki wakati waliopo Simba lakini kitendo chake cha kuituhumu Simba wakati wa CL kuhusiana na rushwa na madawa kwenye vyumba vya uwanja kashfa hizo zilisambaa dunia nzima kupitia mitandao ya kijamii na kuishushia hadhi Simba na Tanzania kwa ujumla wake kinamnyima nafasi kurudi Simba.

Na hili ni funzo kwetu wote tusipende sana kuwachafua watu bila sababu kwani kesho tunaweza kujikuta tunawahitaji hao tuliowachafua kuwa msaada kwetu kwa njia moja au nyingine.
 
Hata mimi nimeshangaa kama kweli wanamtaka banda ni heri Kilomoni arudi wanahangaika na mchezaji asiye na umuhimu wowote tena aliondoka Simba kwa nyodo haya yatakuwa kama mambo ya kumsajili Ajib wakati hakuwa anahitajika
Mkuu banda anatafuta kiki ile apate dau nono na kujifanya ana umuhimu ,Simba hii imtafute banda kweli halafu aende Mtibwa ?Angalia tu usajili Simba amefanya Banda aache kutafuta kiki na mileage ya kuonekana bora.
 
Tafuta hela wewe acha kudili na mambo ya kipuuzi
 
Back
Top Bottom