Inauma sana: Kansa ya ngozi yamharibu mtoto wa miaka 7....baba amwaga machozi akiomba msaada

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
INAUMA SANA: KANSA YA NGOZI YAMHARIBU MTOTO WA MIAKA 7....BABA AMWAGA MACHOZI AKIOMBA MSAADA




MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.

Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.


“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.

“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 na 0715 424697 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi.
 
hii picha inasikitisha sana. Kweli binadamu kabla hujafa hujaumbika.
Inawezekana katika Mungu huyu tumwitaye Yesu. Kama anaweza kumpeleka kwenye maombi Yesu yuko tayari kumponya. Ameshaponya magonjwa mengi zaidi ya haya.
Kwake yeye hakuna linaloshindikana.
John 3:36 "He that believeth on the Son hath everlasting life:"
Luke 1:37 "For with God nothing shall be impossible.''
 
Inauma kweli. Naam rais wetu anayependa kusaidia wabugiaji unga, huyu mwanetu naye anahitaji msaada wa haraka unasemaje?
 
La Haula wala Kuwata ila Billahi LlaAdhiym.
 
Kaka jaribu kuwaona Serikali sikivu ya CCM huenda wakawa na huruma wakasaidia angalau nauli, kama ingewezekana ukaenda kwa TB Joshua wa Emmanuel TV Lagos nadhani maombi yangesaidia sana. Nimewahi kuina watu wenye case kama hiyo wakapata kupona. Mungu akujalie na kukufungulia mlango kila utakapokwenda ili ufanikiwe kumponya binti yetu
 

Ammmeeen ... kwa utukukufu na mamlaka ya mistari tajwa ... ninaenda kutoa tamko toka kwa Bwana kuwa n three weeks time Mtoto atapona na jina la Bwana lisifiwe na kuhimidiwa.
 
In jesus name he will be healed na mungu amrehemu.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Naliombea hili taifa siku moja tutakuwa na
1. madaktari willing na wenye nia ya dhati katika kufanya uchunguzi wa kina wagonjwa wao
2. Vifaa na vitendea kazi muhimu kwenye mahospitali ya umma.

Nina hakika kama haya yangekuweko this little angel asingekuwa amefika stage aliyofikia this is very sad.
 
Maskini mtoto Ashura....Kile kitengo cha Wizara ya Afya kinacho-approve safari za matibabu si wangeweza kusaidia hali kama hizi? Ila stage 4, si ni critical? Au?
 
rabbannaa lammaa jaa atnaal,,...rabbanaaa af-rig alay-naa sabranw-wa....,,ta waffanaa muslimiin................!!!!!!!!!!!
 
Ammmeeen ... kwa utukukufu na mamlaka ya mistari tajwa ... ninaenda kutoa tamko toka kwa Bwana kuwa n three weeks time Mtoto atapona na jina la Bwana lisifiwe na kuhimidiwa.

May our prayers meet in the spiritual realm.
And let it be done unto her as thou hast believed in faith.
Amina.
 

It is my prayer that your prayers be heard and granted as quick as the speed of light
 
Mwenyezi Mungu tunaomba umponye mtoto wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…