Inauma sana wakuu, kijana amenikata ngwala hadharani

Kwanza naomba niwaonye wakubwa wenzangu, ili kurahisisha maisha kuna wakati tunapaswa kupuuza baadhi ya mambo ili tujifanyie wepesi.

Naomba nifupishe simulizi.

Leo nilifunga safari kwenda shule fulani kutoa discipline kwa kijana huku nikiwa nimeambatana na fungu moja la bakora (vijana wanaita mzigo wa kuni).

Kama kawaida nikifika shuleni na nikapokewa mfuko wangu nilio bebea nguo zangu, na ule mzigo mwingine kama mnakumbuka watoto pia wakauopokea huku wakishangilia na sikuuona tena (kumbe walizipeleka zile fimbo jikoni na kusema kwamba baba yake na fulani katuletea na zawadi ya kuni).

Basi nikapitiliza hadi ofisi ya mkuu pale, nilipo ingia na kijana akawa amefika tayari maana kidogo pale shule wanafunzi wapo so active kuhabarishana taarifa.

Bila kuchelewa nikaanza kutoa mashtaka yangu mbele ya mkuu pale sasa kijana alipo sikia nikamuona kama anasimama na akataka kukimbia, basi nikataka kumkata ngwala na nikakosea nika kanyaga kamba ya kiatu kumbe nilisahau kuifunga vizuri, wakuu nilikula mweleka right on front of my son.

Hapa nilisimama na nikaanza kujipangusa, basi kijana akasogea na kunipa pole, mzee nikaona usintanie badala ya kuitikia nikanyenyua teke na akalikwepa nikapita na stuli ya ugoko dahhhh.

Hapa ikabidi kijana akimbie nje, na mimi nikaona isiwe tabu maana bado sijazeeka sana, wacha nimkimbize, kijana alinikata chenga mbele ya kundi la wanafunzi katika kumkimbiza wakuu... Nilikula mweleka na nikaangukia upande wa kitambi hadi kidogo suruali ya kaunda niliovaa ikatatuka kwa nyuma kidogo.

Wakuu, kwa leo naomba niishie hapa, haya mambo ya kuwafuatilia vijana wenye damu inachemka zaidi sio sawa, kuanzia Leo nimejifunza na ninawashauri wazee wenzangu kwamba hakuna jambo jema kama mzazi kuongea na mwanae katika kila jambo pasipo kujalisha ugumu ama uzito wa situation husika, na wazazi tupunguze matumizi ya nguvu iliyopita kiasi katika kuwa nyoosha vijana wetu.

Mungu awabariki sana, mimi na familia yangu tunawatakia usiku mwema na amani tele.
Mkuu ndio ww ulienda Lalago kumpa adabu kijana kisa kaongea na wenzake lugha usiyotambua? Kama ndio wewe nilikuonya achana na hawa watoto umeshindwa kumuonya na kumfundisha nyumbani mbele ya dunia atakufunza wewe. Ila kama nakuona ulivyoshikilia ugoko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulikuonya tangia juzi kuwa; Achana na huyo kijana wako usimzingue kwa mambo yako ya kutaka kum-disipilini. Hukutusikia sasa hayo ndo mavuno ya ungangari wako.
Kwetu wana kausemi; Asosikia la wazee,,,
Dahhh....
Nikweli mkuu, ningelisikiliza ushauri wenu haya yote yasinge nisibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ndio ww ulienda Lalago kumpa adabu kijana kisa kaongea na wenzake lugha usiyotambua? Kama ndio wewe nilikuonya achana na hawa watoto umeshindwa kumuonya na kumfundisha nyumbani mbele ya dunia atakufunza wewe. Ila kama nakuona ulivyoshikilia ugoko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio mimi mkuu, ahsante kwa ushauri wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza naomba niwaonye wakubwa wenzangu, ili kurahisisha maisha kuna wakati tunapaswa kupuuza baadhi ya mambo ili tujifanyie wepesi.

Naomba nifupishe simulizi.

Leo nilifunga safari kwenda shule fulani kutoa discipline kwa kijana huku nikiwa nimeambatana na fungu moja la bakora (vijana wanaita mzigo wa kuni).

Kama kawaida nikifika shuleni na nikapokewa mfuko wangu nilio bebea nguo zangu, na ule mzigo mwingine kama mnakumbuka watoto pia wakauopokea huku wakishangilia na sikuuona tena (kumbe walizipeleka zile fimbo jikoni na kusema kwamba baba yake na fulani katuletea na zawadi ya kuni).

Basi nikapitiliza hadi ofisi ya mkuu pale, nilipo ingia na kijana akawa amefika tayari maana kidogo pale shule wanafunzi wapo so active kuhabarishana taarifa.

Bila kuchelewa nikaanza kutoa mashtaka yangu mbele ya mkuu pale sasa kijana alipo sikia nikamuona kama anasimama na akataka kukimbia, basi nikataka kumkata ngwala na nikakosea nika kanyaga kamba ya kiatu kumbe nilisahau kuifunga vizuri, wakuu nilikula mweleka right on front of my son.

Hapa nilisimama na nikaanza kujipangusa, basi kijana akasogea na kunipa pole, mzee nikaona usintanie badala ya kuitikia nikanyenyua teke na akalikwepa nikapita na stuli ya ugoko dahhhh.

Hapa ikabidi kijana akimbie nje, na mimi nikaona isiwe tabu maana bado sijazeeka sana, wacha nimkimbize, kijana alinikata chenga mbele ya kundi la wanafunzi katika kumkimbiza wakuu... Nilikula mweleka na nikaangukia upande wa kitambi hadi kidogo suruali ya kaunda niliovaa ikatatuka kwa nyuma kidogo.

Wakuu, kwa leo naomba niishie hapa, haya mambo ya kuwafuatilia vijana wenye damu inachemka zaidi sio sawa, kuanzia Leo nimejifunza na ninawashauri wazee wenzangu kwamba hakuna jambo jema kama mzazi kuongea na mwanae katika kila jambo pasipo kujalisha ugumu ama uzito wa situation husika, na wazazi tupunguze matumizi ya nguvu iliyopita kiasi katika kuwa nyoosha vijana wetu.

Mungu awabariki sana, mimi na familia yangu tunawatakia usiku mwema na amani tele.
Ulivaa kaunda suti kama ya Musiba mzee? 😂 😂 😂 😂

Pole sana,kama naiona hiyo suruali ilivyotatuka kwa nyuma..!
 
Back
Top Bottom