Inauma sana wakuu, kijana amenikata ngwala hadharani

Inauma sana wakuu, kijana amenikata ngwala hadharani

Mi nakushauri mkuu mvizie tu akirudi likizo, shuleni atakuaibisha tena.
Sawa mkuu...
tapatalk_jpeg_1568211858235.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abee mkuu, tangawizi ni nyingi ila chai ilikua poa nimecheka mara mweleka,ngwala in front of your son, mara zigo la fimbo limepelekwa jikoni dah tafrani[emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio mkweo huyo ananifanyia uhuni mbele ya wanafunzi wenzake, maana pia suruali ya kaunda suti ilipasuka kwa nyuma kwasababu ya tambo za mbio
 
Ndio mkweo huyo ananifanyia uhuni mbele ya wanafunzi wenzake, maana pia suruali ya kaunda suti ilipasuka kwa nyuma kwasababu ya tambo za mbio
Hapo sasa ndo pa kumpa makonde km mike tyson, otherwise anakugeuza delicious 🤣🤣🤣
 
Kwanza naomba niwaonye wakubwa wenzangu, ili kurahisisha maisha kuna wakati tunapaswa kupuuza baadhi ya mambo ili tujifanyie wepesi.

Naomba nifupishe simulizi.

Leo nilifunga safari kwenda shule fulani kutoa discipline kwa kijana huku nikiwa nimeambatana na fungu moja la bakora (vijana wanaita mzigo wa kuni).

Kama kawaida nikifika shuleni na nikapokewa mfuko wangu nilio bebea nguo zangu, na ule mzigo mwingine kama mnakumbuka watoto pia wakauopokea huku wakishangilia na sikuuona tena (kumbe walizipeleka zile fimbo jikoni na kusema kwamba baba yake na fulani katuletea na zawadi ya kuni).

Basi nikapitiliza hadi ofisi ya mkuu pale, nilipo ingia na kijana akawa amefika tayari maana kidogo pale shule wanafunzi wapo so active kuhabarishana taarifa.

Bila kuchelewa nikaanza kutoa mashtaka yangu mbele ya mkuu pale sasa kijana alipo sikia nikamuona kama anasimama na akataka kukimbia, basi nikataka kumkata ngwala na nikakosea nika kanyaga kamba ya kiatu kumbe nilisahau kuifunga vizuri, wakuu nilikula mweleka right on front of my son.

Hapa nilisimama na nikaanza kujipangusa, basi kijana akasogea na kunipa pole, mzee nikaona usintanie badala ya kuitikia nikanyenyua teke na akalikwepa nikapita na stuli ya ugoko dahhhh.

Hapa ikabidi kijana akimbie nje, na mimi nikaona isiwe tabu maana bado sijazeeka sana, wacha nimkimbize, kijana alinikata chenga mbele ya kundi la wanafunzi katika kumkimbiza wakuu... Nilikula mweleka na nikaangukia upande wa kitambi hadi kidogo suruali ya kaunda niliovaa ikatatuka kwa nyuma kidogo.

Wakuu, kwa leo naomba niishie hapa, haya mambo ya kuwafuatilia vijana wenye damu inachemka zaidi sio sawa, kuanzia Leo nimejifunza na ninawashauri wazee wenzangu kwamba hakuna jambo jema kama mzazi kuongea na mwanae katika kila jambo pasipo kujalisha ugumu ama uzito wa situation husika, na wazazi tupunguze matumizi ya nguvu iliyopita kiasi katika kuwa nyoosha vijana wetu.

Mungu awabariki sana, mimi na familia yangu tunawatakia usiku mwema na amani tele.

Kutoka mkaka mkimyaa, mpolee bin mtaratibu hadi mkaka muongeaji na mchekeshaji.

Mia...(nimekukumbushia enzi zako...100!).

Matata the K.
 
Back
Top Bottom