Inauma sana, wezi walaaniwe. Wamenirudisha nyuma sana

ASA 1

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2017
Posts
234
Reaction score
568
Habari waungwana!!

Mimi ni kijana niliyehitimu elimu ya juu. Kutokana na changamoto za ajira niliamua kujiajiri kwa kufungua biashara Mpesa (Tigo, Airtel nk) kwa kutumia kiasi kidogo cha pesa nilichojiwekea kutoka katika boom langu.

Baada ya muda mtaji wangu ulikuwa. Nikaamua kuanzisha biashara nyingine huku ofisi ya mwanzo nikamuweka mdada apige kazi.

Basi baada ya kipindi kupita mdada alitapeliwa kiasi kadhaa cha mtaji. Kwa kuwa ofisi mpya ilikuwa inaenda vizuri nikaamua nichikue mtaji uliobaki nichanganye nibaki na biashara moja ile mpya na kuachana na Mpesa.

Siku moja kabla ya tukio nilifungasha mzigo wa kufa mtu kulingana na mtaji wangu. Nikabakisha pesa kidogo tu kwa ajili kunisogeza siku mbili tatu huku nikiwa nasukuma mzigo mpya.

Siku hiyo nilifunga ofisi mapema kwa kuwa nilikuwa sijisikii fresh. Kesho yake asubuhi naingia ofisini, laahaula!! Sikuamini kile macho yangu yanaona.

Wezi walitaifisha kila kitu daah, walinifanya kuwa masikini ghafla. Mtaji wote umeenda, sijui nitaupataje sasa. Nimebaki natangatanga tu, hustle za kutembeza bahasha bado zimebuma.

Vibarua naishia kuvitazama tu bila channel hakuna kugusa. Hali imekuwa tete,njaa imeniganda.

Hebu nipeni mawazo kidogo nipenye wapi pengine nitapata ahueni kutoka kwenye kuchanganyikiwa huku. Nina imani siku moja nitasimama tena.

Hakika wezi walaaniwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Wakoritho : Mlango 10
13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
ASA 1,

Mungu ana mpango wa kukupeleka mbele na mbali zaidi.
Mtumaini na kumtegemea yeye tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…