Inaumiza, inakatisha tamaa, ni unyanyasaji dhidi ya wanawake na rushwa

Inaumiza, inakatisha tamaa, ni unyanyasaji dhidi ya wanawake na rushwa

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
478
Reaction score
1,025
Mamlaka ya usafiri na uchukuzi fuatilieni hili swala, mama kama huyu kusafiri mikoa yote mzigo wake ukiwa sawa alafu ghafla anazuiliwa kwenye mzani wa mwisho inafikirisha sana.

Kuna mazingira ya ubovu wa mizani, UNYANYASAJI kwa mwanamke kwa kuzingatia majibu ya meneja kuwa "wewe ni mwanamke na hizi ni kazi za kiume tu" hii kauli peke yake inatosha ku justify the attitude of this manager towards women" kuwa hawathamini wala hawezi kuwa mwepesi kutatua changamoto zinazohusu wanawake ndani ya eneo lake kazi.

Rais anachagua mtu wa kuweza kumsaidia kazi kwa usawa, upendo na kuwajibika kwa mwanachi wa aina yoyote bila kujali, umri, jinsia, dini na hali zozote ikiwepo ulemavu.

Kiufupi huu meneja hatoshi kwenye iyo nafasi, ana mfumo dume, majigambo, kiburi na tabia ambayo hatasaidia kutekeleza majukumu alopewa na mwajiri wake hivyo kupelekea usumbufu, upotevu wa muda na unyanyasaji wa aina zote.

Soon tutasikia maelezo upande wa meneja ila kama kutakuwa na angalau nusu ya haya nayoeleza dereva kuwa kweli, hakika meneja hustahili kuwepo kwenye nafasi uliyopo.

Kama manager ulitilia shaka uzani wa gari ya dereva, ulitakiwa kuchukua karatasi zote kutoka kwenye mizani zote dereva alizovuka salama, wasiliana kupata uhakika wa documents hizi, ukijiridhisha zipo sawa, ulipaswa kuchunguza mizani yako kwa kuwa haiwezekani mizani zote zipime sawasawa alafu ya kwako pekee ndo iwe tofauti.

Ni concept ndogo tu ila sijui kwanini meneja ilikuwa ngumu kifikiria hivyo, zaidi ikawa rahisi tu kwako kuona jinsia ya dereva kuwa ni mwanamke na kuishia kumtukana na kumpotezea muda.

Hali hii haipo tu kwenye wizara ya uchukuzi, ila hii ndo hali halisi kwenye vitengo vingine vy serikali kwaiyo mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasani tunaomba uangalie tena swala la nidhamu katika utumishi wa umma. Mtangulizi wako alijitahidi sana katika swala la nidhamu katika utumishi wa umma na hii ni challenge kwako isikutie doa. RARA NAO MBERE, huna cha kupoteza, wewe ni Rais.

 
Back
Top Bottom