Inaumiza sana kusoma chuo kikuu na kupata degree ila haitumiki kukubadilishia maisha, umri unaenda na maisha yako yanazidi kuwa magumu

Inaumiza sana kusoma chuo kikuu na kupata degree ila haitumiki kukubadilishia maisha, umri unaenda na maisha yako yanazidi kuwa magumu

MELEKAHE

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2023
Posts
1,340
Reaction score
5,588
Nimeona hii interview ya huyu muhitimu inatrend mitandaoni imeniumiza sana kwa kweli

1724346080352.png
Hujafa hujaumbika! Kijana Noel Swai, mkazi wa Bunju A jijini Dar es Salaam amekuwa mtu wa kutoa machozi kila siku kutokana na maisha magumu anayoyapitia baada ya kupata ajali mbaya ya bodaboda, miaka sita iliyopita.

Ajali hiyo ilisababisha nyonga yake kuondolewa na kuwekwa ya bandia ambayo nayo tayari imeshavunjika muda mrefu anahitaji kutolewa.

Akizungumza na Global TV, Noel ambaye ni msomi wa Chuo cha Ardhi mwenye shahada ya Sayansi ya Mazingira, anasema kuwa hajawahi kuitumia digrii yake ambayo aliisoma ili aikomboe familia yake ambayo iko kwenye umasikini mkubwa.

Ili kuondoa nyonga ya bandia aliyowekewa ambayo nayo imevunjika, Noel amesema inahitajika shilingi milioni moja ambayo hana huku familia yake ikiendelea kuteseka kwa umaskini mkubwa.

Kama umeguswa na habari ya Noel, unaweza kumchangia chochote kupitia namba yake ya simu

Nilipopata ajali marafiki wote walinikimbia
Hujafa hujaumbika! Kijana Noel Swai, mkazi wa Bunju A jijini Dar es Salaam amekuwa mtu wa kutoa machozi kila siku kutokana na maisha magumu anayoyapitia baada ya kupata ajali mbaya ya bodaboda, miaka sita iliyopita ambapo anaeleza kuwa marafiki zake wote wamemkimbia.

Ajali hiyo ilisababisha nyonga yake kuondolewa na kuwekwa ya bandia ambayo nayo tayari imeshavunjika muda mrefu anahitaji kutolewa.

Akizungumza na Global TV, Noel ambaye ni msomi wa Chuo cha Ardhi mwenye shahada ya Sayansi ya Mazingira, anasema kuwa hajawahi kuitumia digrii yake ambayo aliisoma ili aikomboe familia yake ambayo iko kwenye umasikini mkubwa.

Ili kuondoa nyonga ya bandia aliyowekewa ambayo nayo imevunjika, Noel amesema inahitajika shilingi milioni moja ambayo hana huku familia yake ikiendelea kuteseka kwa umaskini mkubwa.

Kama umeguswa na habari ya Noel, unaweza kumchangia chochote kupitia namba yake ya simu
 
Nimeona hii interview ya huyu muhitimu inatrend mitandaoni imeniumiza sana kwa kweli

View attachment 3076648
Nani aliwaambia mwende kusoma chuo kikuu! Nchi hii imejaa kukariri! Mtaani ukifungua duka la nguo wote wanafungua duka la nguo! Ukiuza samaki wote wataanza kuuza samaki! Ukifanya biashara ya kufyatua matofari kila mtu matofari! Sasa wamekariri kusoma mpaka chuo kikuu wakidhani ndo watatoboa! Sio kila mwanafunzi wa sekondari ni lazima mpaka ufike chuo! Mnajipotezea muda! Makazini kumejaa graduate mbumbumbu wezi na mafisadi wa mali za umma hakuna ubunifu! Hatuna elimu ya kujitambua ndo maana vijana graduate wako mtaani wanazurula! Jitathimini kwanza na hesabu gharama kabla ya kujenga ukuta! Kalaghabao!
 
Jaman msiongee tu Kwa mihemko,omba yasikukute mtu wangu.haya mambo ni reality iliopo katik maish yanayotuzunguk.imagin unwekez nguvu kubwa juu ya jamb flan ukitegemea matokeo mazur zen unakuja ku-fail.co pow wakuu.hii ndo inaitw"msuli tembo matokeo sungura"
 
Ujue ukiwaza sijui digrii yangu sijaifanyia kazi, utachelewa sana, digrii zenyewe ni Mult purpose, unakuta mtu amesomea account lakn ndani yake kulikuwa na course ya entrepreneur, na mpaka leo anasubiri ajiliwe awe accountant hapo lazima mkwamo uwepo, Kwangu Elimu ni uwezo wa kugeuza changamoto kuwa fursa, na ndio aliyesoma anategemewa afanye hivyo, changamoto tunakariri madesa ili tusipate supp, vyuoni wakat wa field huwa kuna option ya kufanya project kama umekosa sehemu ya kufanyia field lakini kiukweli ilitakiwa tufanye hizo project ili kuyajua mazingira yetu hiyo inaamisha udadisi
 
Nani aliwaambia mwende kusoma chuo kikuu! Nchi hii imejaa kukariri! Mtaani ukifungua duka la nguo wote wanafungua duka la nguo! Ukiuza samaki wote wataanza kuuza samaki! Ukifanya biashara ya kufyatua matofari kila mtu matofari! Sasa wamekariri kusoma mpaka chuo kikuu wakidhani ndo watatoboa! Sio kila mwanafunzi wa sekondari ni lazima mpaka ufike chuo! Mnajipotezea muda! Makazini kumejaa graduate mbumbumbu wezi na mafisadi wa mali za umma hakuna ubunifu! Hatuna elimu ya kujitambua ndo maana vijana graduate wako mtaani wanazurula! Jitathimini kwanza na hesabu gharama kabla ya kujenga ukuta! Kalaghabao!
Dhana nzima ya kusoma mpaka university kiukweli siyo ili uajiriwe na serikali, kwa sababu serikali zote duniani hazina huo uwezo wa kuajiri wananchi wake wootee. Elimu mpaka chuo kikuu lengo lake kubwa ni kukupa uwezo mkubwa wa kufanya mipango yako ya maisha iwe ni kilimo, ufugaji,biashara etc...mfano nimeenda huko Katavi vijijini kabisa unakuta jinsi jamii inavyolima kizamani, lishe duni pamoja na kwamba wanalima nk nk Mtu aliyeelimika ana uwezo mkubwa wa kulima kisasa, kufuga kusasa, kutafuta masoko mitandaoni etc...Msomi wanaweza kuungana na kufungua biashara za kisomi kama hawa wenye JF, kufungua zahanati,maabara, kutengeneza websites etc etc. Mwisho hata nchi zenye raia wengi waliosoma wanajielewa na kujitambua na siyo rahisi kuburuzwa hovyo na viongozi wasiowajibika .
 
Back
Top Bottom