Inavyofikirika na wanaofikiri na namna isivyofikirika na wanaofikiri wanafikiri

Inavyofikirika na wanaofikiri na namna isivyofikirika na wanaofikiri wanafikiri

TozzyMay

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
482
Reaction score
1,787
Yaliyomo
A & B ==> wanadamu
C ==> Mungu
C katoa Sheria kwa A na B wapendane kama jinsi yeye anavyowapenda, ilihali wakipendana wasitendeane Ubaya.
Pia, C katoa ahadi ya Maisha ya Furaha ya Milele kwa asiye mdhambi Miongoni mwa A na B, na katoa ahadi ya Maisha ya Maumivu ya Milele kwenye Moto wa jehanam kwa mdhambi Miongoni mwa A na B.
Hivyo C ni Mwanzo na Mwisho .
-maana ya upendo inatoka kwa C
-maana ya hukumu inatoka kwa C

Ikitokea A Kaiba mali ya B, C atamhesabia dhambi A na B atahitajika amsamehe A Ili kutimiliza amri ya Upendo kutoka kwa C naye B akimsamehe A jina lake litaandikwa kwenye Kitabu cha watakaopata Ile ahadi ya Furaha ya Milele. Ila B naye asipomsamehe A, naye atahesabiwa mdhambi na C kama ilivyo kwa A ikiwa A naye hakutubu makosa yake.

Hivyo basi, kosa la B linaweza kumfanya A kuhesabiwa dhambi mbele ya C Pamoja na B mwenyewe.
A kwa kishindwa kutekeleza amri ya Upendo kupitia B, A atachomwa Moto wa milele wa Jehanam akiwa pamoja na B .
Pengine A Hajamsamehe B kwa kuwa B hakurudi kuomba Msamaha, ila inampelekea A kuhesabiwa mdhambi mbele ya C.

C ana Upendo mkamilifu kwa A na B ndiyo maana C akawaagiza A na B wapendane kama jinsi C anavyowapenda.
C humsamehe yule (A/B) anayekiri makosa yake Mbele zake.
Kaagiza A na B ,Kila mmoja asamehe 70×7 ila C hafanyi kusamehe 70×saba .

(<[Ingetokea C angelikuwa anasamehe saba×70 ,jehanam inayosadikika isingesadikika kuwepo]>)
 
Huyo C hayupo.

Na kama yupo basi hafai kabisa anastahili kufurushwa.
Lakini , kwanini C anasadakika kuwepo?
Halafu kwanini ,Kuna A na B wasadiki uwepo wa C?
Kuna A na B, wengi wanasadiki uwepo wa C.
Na wanadai C anawasaidia, kama sio C anayewasaidia basi wanasaidiwa na nani?
Sheria za C zinapinga uwepo wa C, deep thinking
 
Lakini , kwanini C anasadakika kuwepo?
Kusadiki unaweza kusadiki hata uongo.

Hata Vibwengo, Aliens👽 na Dragons husadikika kuwepo. Lakini kiuhalisia hawapo.

Sawasawa na Mungu, Husadikika yupo ila kiuhalisia hayupo.
Halafu kwanini ,Kuna A na B wasadiki uwepo wa C?
Kuna A na B, wengi wanasadiki uwepo wa C.
Kusadiki unaweza kusadiki hata uongo.

Na haijalishi ni watu wengi kiasi gani wanasadiki Mungu. Kama hakuna uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu. Mungu huyo ni dhana ya kufikirika tu.

Ni sawa na watu wengi wanavyo sadiki uwepo wa Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao, Kumbe kiuhalisia hawapo.
Na wanadai C anawasaidia, kama sio C anayewasaidia basi wanasaidiwa na nani?
Hakuna Mungu anaye saidia kitu chochote kile.

Kudai unaweza kudai hata uongo.

Lakini ili tuthibitishe hicho unacho "kidai" ni ukweli. Lazima uthibitishe na utoe ushahidi wenye uhakika.

Kwa hivyo, Thibitisha kwanza Mungu yupo. Kisha ndio useme anakusaidia.

Vinginevyo madai yako ni ya uongo.
Sheria za C zinapinga uwepo wa C, deep thinking
Hapo tayari sheria hizo zina thibitisha huyo C= Mungu. Hayupo.
 
Kweli ni hakika ya jambo.Kweli hii yawezasadikishwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu au watu na pia kizazi kimoja hadi kingine.Kupitia kusadiki werevu huweza kutumia ghiliba kufanikisha lengo lao.Mfano ni suala la Mungu:hakuna jamii iliyowahi ishi hapa duniani pasipo kuamini Mungu na binadamu amekuwa akisadiki miungu wengi kulingana na hitaji.Urasmishaji wa Mungu wa taifa enzi za nabii Eliya na kusadikishwa kizazi hadi kizazi ndiyo chanzo cha uwepo wa supreme deity(Mungu mkuu).Sisi wengine ni zao la ukengeufu na kujikuta tunasadiki katika mapokeo.
 
Je Kuna ukweli uliojificha kuhusu C
 
Fafanua maana ya huyo C.

Ni nani? Ni nini? Katoka wapi?
 
Back
Top Bottom