GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Mtu mmoja alishawahi kuniambia kuwa alipokuwa akiishi Marekani yeye na familia yake alipokuwa masomoni, hakuwa akisumbuka kununua baadhi ya vitu vya ndani kama sofa, TV, n.k. Alichokuwa akifanya ni kwenda kunakotupwa vitu vilivyokwishatumika na kuvihamishia nyumbani kwake.
Kwamba, ni kawaida kwa Marekani kukuta vitu vizuri vimetupwa, ambavyo vingefikishwa hapa Tanzania, vingeweza kuwa "mali". Magari, sofa, TV, laptop, n.k. ni kawaida kutupwa huko, wamiliki wake wanapokuwa wamezichoka.
Kama hayo ni kweli, kwa nini Watanzania wasiende kujikusanyia huko "mali" za bure na kuja kuziuza?