Inawezekana Mbeya City ni tabia yao!

Truth Matters

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
2,302
Reaction score
4,603
Ukiachia mbali kuboronga kwa referee wa mchezo wa jana kati ya Mbeya city na Yanga. Nimeshtushwa na ujasiri wa kiwango cha 'nuclear' ulioneshwa na Mbeya City

Hakika sijawahi hata kudhania kuwa timu tena ya VPL inaweza kufanya uhuni ule wa kuchomekea mchezji kinyemela. Na zaidi haiwezekani kuwa ni bahati mbaya!

Inawezekana wameshafanya sana huko nyuma ila waliweza 'get away with it'!
Nadhani TFF watapata tabu kupata sheria ya kuamua swala hili, sijui kama lipo kwenye sheria na kanuni!
Hongera Mbeya City kwa ubunifu wa kijinga!
 
Aiseee hiii yao n kali sana
Na n kama wanakua wamepanga mwanzo kabsa ya game kuanza
Wakiwa vyumban mwao
 
Ikiwa mwizi hatakamatwa, huyo tunamuita mtfutaji.
Kwa vile hizo zama zingime hawakukamatwa, it's ok. Lkn kwa kuwa sasa wamekamatwa, imekula kwao.
 
Adhabu ya kwanza kabisa inabidi washushwe daraja
 
Siku hizi huku mjini kuna technology kaka watu hawabahatishi!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kweli ushamba mzigo. Kama mtu hata masuala ya teknolojia tu hajua........ Mkuu ukombozi wa fikra bado sana Tz
 
Mi siamini bado,msajigwa tu aone?,yaani referee na mareferee wasaidizi wasione,wachezaji wa Yanga wasione
 
Mi siamini bado,msajigwa tu aone?,yaani referee na mareferee wasaidizi wasione,wachezaji wa Yanga wasione
Mkuu nadhani hukuwepo uwanjani, walioanza kuona ni mashabiki wa Yanga waliokuwa jukwaani ambao walianza kupiga kelele na miruzi kuonyesha Mbeya City wanafanya uhuni wa kizamani, na hapo ndipo Msajigwa naye akaanza kupaza sauti....

Okay yote kwa yote ni teknolojia tu, video zinaonyesha hivyo, sasa hatuna sababu ya kuhoji tena nani kaona au nani hajaona.

Katika hili tuweke ushabiki pembeni, tusimamie Haki na Ukweli.
 
Inamaana aliyeona ninnsajigwa tuu..hii ni kama hadithi za kutungwa
Hata ye mwenyewe kasema alipaniki kwa ile droo ila hana uhakika zaidi kama walikuwa wamezidi, mpaka anatia aibu kwa maelezo yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…