Inawezekana Mbowe ni gaidi, ila...

Inawezekana Mbowe ni gaidi, ila...

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Kuna ukweli umejificha inawezekana kabisa Mheshimiwa Mbowe ni gaidi tusubiri serikali ithibitishe au kumkuta na hatia, sio kutuambia alitaka kulipuwa vituo vya mafuta na sehemu zingine, bado hilo halipo sawa, maana gaidi ni watu wanne tu?

Ninavyosikia gaidi au magaidi huwa ni netiwaki kubwa sana au kundi au kikundi kikubwa na sio watu wanne, labda waseme ni jambazi na hapo wasibitishe ujambazi alioutekeleza.

Kuna mashambulizi ya ugaidi kusini mwa tanzania hatujaambiwa ni nani aliongoza au kikundi gani, hamna taarifa iliyokamilika, hali kadhalika mashambulizi ya Kibiti kati ya Polisi na wasiojulikana yalivuma, haikujulikana kiongozi alikuwa nani? Kiasi ya wananchi kuhesabu kuwa na mambo ya kisiasa za kiccm.

Marehemu Maali Seif na wenzake walikamatwa na kusota jela kwa kosa la kiccm la eti walipanga kufanya Mapinduzi.

Kule Zanzibar kutaka kuiondoa CCM madarakani unashitakiwa kwa kosa la kutaka kufanya mapinduzi. Huku Tanganyika kutaka kuiondoa CCM madarakani unashitakiwa kwa kosa la ugaidi.
 
harikazalika= Hali kadhalika

Kwa uandishi huu achana na habari za Mbowe
 
Mkuu upo nyuma ya wakati sanaa...nikuombe tuu.. usijaribu kufanya predictions za vitu usivyo na uhakika navyo.

Na, siyo kila mtu anauwezo wa kujadili mambo makubwa kama hayo kwa upeo wako?

Kwa upoe huo jadii vitu vidogo vdgo... zinakufaa sana
 
Kenya tuu hapo penye mashambulizi kabisa ya alshabab hawajatangaza kuna ugaidi.

Then hapa kwetu ambako hatuna hata bifu na makundi ya kigaidi tunampa statesman kesi mbaya ya ugaidi?

Halafu ukiangalia ushahidi wake mpaka la saba B asiye na akili anaziba masikio na macho asisikie wala kuona huo utopolo.
 
Kenya tuu hapo penye mashambulizi kabisa ya alshabab hawajatangaza kuna ugaidi.

Then hapa kwetu ambako hatuna hata bifu na makundi ya kigaidi tunampa statesman kesi mbaya ya ugaidi?

Halafu ukiangalia ushahidi wake mpaka la saba B asiye na akili anaziba masikio na macho asisikie wala kuona huo utopolo.
Hivi utopolo ni nini?
Mara Yanga utopolo
Mara ushahidi utopoto,
Sasa utopolo ni nini?
 
Gaidi sio lazima kikundi kikubwa, hata mtu mmoja unaweza kuwa gaidi. Kivipi! Unaweza kupewa mafunzo makali huko nje na ukaja kujumuika na wananchi lakini ni gaidi.
 
Back
Top Bottom