Inawezekana ndege kutumia dakika 5 kutoka Dar-Dodoma?

Habari zenu wakuu,

Kuna kitu najiulizaga nakosa majibu kwakweli yaani dunia imefikia level ambayo kila kitu washamaliza kabisa, and ndo mwisho unakaribia?

Mimi hapa nilikuwa najiuliza swali dogo kabisa kuna ndege inatoka Dar mpaka Dodoma kwa dakika tano (5) ndio 5 na kuna gari inatembea kilometer 500km/h hapa sijajuliuza kuhusu nasa,roboti sophia, etc

Hebu twende kwa hesabu ndogo tu dakika moja ni sawa na sekunde 60 dakika tano ina sekunde 300 kutoka Dar mpaka Dodoma kuna kilometer 444km

Kwa hiyo hapo ukigawanya utapata 1.5km per sec kwa sekunde yaani kwa sekunde moja tu chombo kinatembea 1.5km inashangaza na kumbuka hizi ndege ni za zamani sio za kisasa sasa najiuliza hizi za kisasa inakuaje

Gari linakimbika 500km/h daaah

60*500 =30000sec = 0.0166km per sec daaah.

Dunia inashangaza
Kupaa na kutua ndege hutumia dakika nyingi, lakini hasa kwenye kujiandaa kutua. Ili ndege itue kwa usalama inahitaji dkk kama 20 hivi, ili kupunguza mwendo na kupambana na hali ya hewa ya mahali husika. Kwa hio haiwezekani katika mazingira ya kawaida ndege itumie dkk 5 toka Dar mpaka Dodoma.
 
Unajichanganya, Dar-Dom kwa barabara ni km 444 lakini kwa anayetumia anga itakuwa kama 2/3 ya hizo au pungufu. Ndege ya abiria aina ya Concorde (now grounded), ilikuwa inatembea mpaka speed ya 2179 km/hr, Jeshi la Marekani wapo kwenye hatua za mwisho kutoa hypersonic jet yenye speed ya 6100 km/hr. Yale ma-space shuttle likishatulia angani, lina speed mpaka 39,897km/hr.
Kazi kwako kudadavua.
Corcode ilikuwa ndege ya kifaransa waliacha kubebea a abiria baada kupata ajali
 
Lakini pia ilikuwa na matumizi makubwa ya mafuta. Hilo lingine la kiufundi lingeweza kurekebishwa.
 
Ile ajali ilikuwa ya ajabu kwenye uchunguzi waliabaini wakati kwenye kiwanja cha ndege Paris ndege ya shirika lingine inatoa ilidondosha kibati kidogo ambacho kilikuja kukanyagwa na ndege ya corcode muda huo ikapelekea tairi kupasuka la kwenye upande wa tank la mafuta so wakati inapaa ndege ilikuwa inawaka tayari ila kwa vile ilikuwa kwenye speed kubwa rubani alitafuta sehemu zuri ya kuimwaga watu wote walikufa na kuwatambua watu ilibini watumie DNA testing mpaka leo zinatumika kwa ajili ya kubebea mizigo tuu
 
Habari zenu wakuu,

Kuna kitu najiulizaga nakosa majibu kwakweli yaani dunia imefikia level ambayo kila kitu washamaliza kabisa, and ndo mwisho unakaribia?

Mimi hapa nilikuwa najiuliza swali dogo kabisa kuna ndege inatoka Dar mpaka Dodoma kwa dakika tano (5) ndio 5 na kuna gari inatembea kilometer 500km/h hapa sijajuliuza kuhusu nasa,roboti sophia, etc

Hebu twende kwa hesabu ndogo tu dakika moja ni sawa na sekunde 60 dakika tano ina sekunde 300 kutoka Dar mpaka Dodoma kuna kilometer 444km

Kwa hiyo hapo ukigawanya utapata 1.5km per sec kwa sekunde yaani kwa sekunde moja tu chombo kinatembea 1.5km inashangaza na kumbuka hizi ndege ni za zamani sio za kisasa sasa najiuliza hizi za kisasa inakuaje

Gari linakimbika 500km/h daaah

60*500 =30000sec = 0.0166km per sec daaah.

Dunia inashangaza
Dakika tano kuingia anga ya ddma au kutua uwanja waddma? Hivo no vitu viwili tofauti ndege kutua inatjmia dakika 15 hadi 30, kulingana na ubora wa uwanja
 
Unajichanganya, Dar-Dom kwa barabara ni km 444 lakini kwa anayetumia anga itakuwa kama 2/3 ya hizo au pungufu. Ndege ya abiria aina ya Concorde (now grounded), ilikuwa inatembea mpaka speed ya 2179 km/hr, Jeshi la Marekani wapo kwenye hatua za mwisho kutoa hypersonic jet yenye speed ya 6100 km/hr. Yale ma-space shuttle likishatulia angani, lina speed mpaka 39,897km/hr.
Kazi kwako kudadavua.
Sikumbuki vizuri ila nadhani Curiosity Rover iliyopelekwa kwenye sayari ya Pluto ilikuwa inakimbia kwa kasi kubwa zaidi ya hizi ulizozitaja hapa, na ilipokuwa njiani baada ya kuingia kwenye eneo la Kuiper Belt, ilikuwa acckerated zaidi kna kupelekea spidi yake kuongezeka zaidi
 
Back
Top Bottom