Inawezekana Ole Sabaya "anaonewa" kweli

Inawezekana Ole Sabaya "anaonewa" kweli

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Kama Taifa kuna vitu tunadharau sana na mara nyingi vime Tu cost Sana na kwa sababu hatutaki kabisa kuvitazama na kuvifanyia kazi, pengine vitaendelea kutu cost sana.

Magonjwa ya akili ni jambo moja Taifa hili hatutaki kabisa kukaa chini na kuweka mipango ya kusaidia 'wagonjwa' wetu
Na kuzuia wengine wasiyapate.

Matokeo yake wagonjwa tunawapa vyeo vikubwa, wanadhuru watu na hata kujidhuru wenyewe. Ikitokea mgonjwa mmoja tumemkamata na kumuadhibu, basi tunafurahi na kuona tumemaliza.

Hatutaki kabisa kukaa chini na kujiuliza huyu mgonjwa ilikuwaje akapata hiki cheo?

Tufanyaje wagonjwa wengine wapate matibabu sahihi badala ya kuwapa vyeo wanakuja kudhuru watu na wao wenyewe?

Mtu mwenye akili ya kawaida hawezi kuwa DC halafu akabeba walinzi binafsi kumsaidia kupora hela watu na kubaka wanawake.
Huyu hata akihukumiwa miaka 50.

Akasema 'tumemuonea' inawezekana kweli tumemuonea.

Hasa kama wagonjwa wenzake bado tunaishi nao na hatutaki kuwapa tiba.
 
Ni kweli ana onewa, kwa madhambi aliyofanya alikuwa sio wakufungwa miaka 30 ambayo kimsingi ni hukumu ya tozi aliyempa mimba dent

Jitu ambalo limepora mali za watu, limefanya ukatili kwa kuumiza watu lilipaswa lipigwe kifungo cha maisha
 
Umeandika kitu kikubwa sana lakini wachache sana watakuelewa mkuu. Binafsi nimekupata vema, na kusema ukweli Maofsini wagonjwa wa akili ni wengi sana, yaani unakuta kiongozi anafanya kitu unabaki unajiuliza huyu kweli yuko timamu!
 
Sabaya ni daraja tu la Mh. Mbowe kuelekea kifungo cha maisha kisha yeye (Sabaya) kutoka kwa msamaha wa Rais. hiii yote ni mipango ili Serikali ilitoe lawamani kwa mataifa.

Kwa yaliyotokea leo, mpango uliopo ni wa Mbowe kufungwa kifungo cha Maisha kitakachopelekea CDM kufutwa. tuwe tayari watanzania.
 
Mimi nimekuelewa vzr tu. Ila sasa inakuwaje unajua kabisa huyu anaugonjwa wa akili ukampa jukumu aongoze wazima?

Hivi kwenye kundi la vipofu na viziwi ni nani atapewa uongozi wa kuwavusha wenzao kwenye mto. Sina maana hiyo na sitengui kauli.

Madaraka ya kujuana haya ndiyo madhara yake, kisa n mtoto wa aliyekusaidia ww ukaitwa fulani basi unamteua tu hata kama hana ueledi.

Ninaimani mbuzi ndio wanaoharibu msafara wa ng'ombe!
 
Mbowe anafungwa lakini hii serikali ikipinduliwa tusije kumlaumu yeyote

Sabaya alitakiwa kweli kupimwa akili Kama yupo sawa mentally.

Ila amefungwa kimtego ili kumfunga Mbowe kwa upande wa pili na kuiua chadema.

Nafikiri Ni wakati Sasa wa Tundu Lissu kurudi na kuonyesha uongozi.
 
Sabaya ni daraja tu la Mh. Mbowe kuelekea kifungo cha maisha kisha yeye (Sabaya) kutoka kwa msamaha wa Rais. hiii yote ni mipango ili Serikali ilitoe lawamani kwa mataifa.

Kwa yaliyotokea leo, mpango uliopo ni wa Mbowe kufungwa kifungo cha Maisha kitakachopelekea CDM kufutwa. tuwe tayari watanzania.
Hujui mambo yalivyo kaa kimya
 
we unafikiri kupandiswa cheo kwa jaji huyo ilikuwa ni bahati mbaya? nyie CCM mnafikiri watanzania wote ni mazuzu?
Mmmh kwa hio kule kuupiga mwingi kwa jopo la mawakili wa Mbowe ni hola!
 
Sio kila MTU ni ccm bro
We Baba Jayaron, CCM ni dude kubwa mno, lipo kila pahala, ukitaka kuhakikisha hilo we kamuulize Mh. Membe, Polepole, Nape, January,Bushiru, Lowassa, Sumaye.. yaliyowakuta, kila mmoja kwa style yake.

Bila katiba mpya kupambana na CCM ni kazi nzito saana na ndiyo maana tunasema afungwe Mbowe asifungwe ni lazima kupambania Katiba tu.
 
Tanzania Sasa Kuna wagonjwa wa akili wengi ila tu basi watu wanapuuza Hilo tatizo kuanzia serikalini, kwenye mahusiano Kuna wagonjwa wengine vile tu tuna ignore hivo vitu hata aliyeenda zake chako ni chako alikuwa mgonjwa wa akili chakushangaza akawa na cheo kikubwa.
N. B kabla ya cheo kutolewa waweke na kipengele Cha kupita viongozi mental health zao kwanza
 
Back
Top Bottom