Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Pamoja na mapungufu yake mengi, ninachomkubali Mizengo Pinda ni uumini wake kwenye Katiba Mpya. Nilishawahi muangalia akitoa maoni TBC akiwa mjumbe wa kikosi cha kutazama hali ya demokrasia nchini na kusema kweli aliunga mkono suala la Katiba Mpya.
Pamoja na mapungufu yake mengi ,ninachomkubali Mizengo Pinda ni pale aliposimama waziwazi kupinga kurejeshwa kwa Bashite CCM kwa hoja kuwa huyu mtu ana mapungufu mengi.
Pamoja na mapungufu yake mengi, Pinda ni mkweli sana. Na ana tabia ya kushauri ukweli kwenye ukweli.
Hakuna ubishi kuwa kisiasa Kinana ndo Legend wa siasa za Tanzania. Sidhani kama kuna mtu anamuweza huyu mtu. Ufahamu wake kwa siasa za ndani na nje ya nchi sidhani kama kuna mwana CCM anayemfikia kwenye hili.
Ni ukweli pia kuwa Kinana amezeeka, na anazeeka kila siku. Kwa umri wake ni kumuonea kumuweka kwenye siasa za purukushani. Alishawahi omba kupumzika huko nyuma na sasa inasemwa ameomba. Aachwe apumzike kwa kuwa kweli amechoka kutokana na kufanya kazi sana.
Vyovyote vile, hofu yangu kubwa sio vita ndani ya CCM bali ni namna nchi yetu itaweza pata Katiba Mpya na bora chini ya CCM hii ya sasa ambao ni power mongers!
Hofu yangu Lord denning ni makundi hasimu ya CCM ambayo kusema kweli nia yao ni kukamata dola kwa maslahi yao na wala sio kuibadilisha hii nchi iwe na maendeleo ya kweli! Sasa kuna kundi linaweza kutupa Katiba Mpya na iliyo bora?
Ukiangalia kwenye mitandao, utagundua hizi tumbua tumbua, toa huyu weka yule zinafanyika kama sehemu ya power struggle tu. Hazina maana yeyote kwa nchi na wananchi. Na hii ni ishara kuwa akilini mwa hawa watu ni madaraka tu!
Napenda kumaliza kwa kusema, vyovyote vile, the future of Tanzania is not promising. TISS watusaidie tupate Katiba Mpya na bora haraka sana!