Pre GE2025 Inawezekana tukapata KATIBA MPYA Mizengo Pinda akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM hawawezi kukupa katiba mpya na hata ikitokea wameamua basi itakuwa ni kwa maslahi ya chama chao na si vinginevyo...

Hiki chama ni cha mabavu na hakuna wa kukifanya lolote labda Mungu...
Ni chama cha hovyo sn lakini baada ya miaka 10 kitaeleweka maana watu wamechoshwa na ufisadi
 
TISS , Baraza kuu na wahusika wote ukweli ni kwamba 2025 tunahitaji Rais mpya hakuna wito Zaidi ya huo, Bibi hapana hapana hata kama anafaa kwa Dunia ya sasa umri wake hapana ikulu sio sehemu ya majaribio na bahati nasibu.
 
Kwenye hili. Ni muhimu kwa dola kuonesha yenyewe ni dola kweli. Maana unachosema kina ukweli kwa sehemu kubwa.

Sasa dola ya JMT si imeundwa na hao hao CCM kwa 100% kuanzia serikali kuu, bunge na mahakama...
 
Mizengo Pinda ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa ccm wanaopinga kabisa Katiba mpya, huyu ni mtu aliyepitwa na aakati ambaye hata rushwa hajawahi kuipiga vita.

Katiba Mpya italetwa kwa mashinikizo ya Wananchi wenyewe
 
CCM inapata kigugumizi kuleta katiba yenye kulinda rasilimali za nchi, katiba inayowapa nguvu wananchi kuchagua viongozi wawatakao na inayowawajibisha viongozi wanaohujumu nchi kwa maamauzi yao mabovu. CCM ni shetani.
 
Tulia kwanza. Usiongee ukiwa na hasira.
 
TISS imelinda umilele wa chama chetu ccm kushika Dola !Sasa yanawatokea puani!!

Yaani kama wangeandaa vyama mbadala mapema leo wangetuacha ccm na maugomvi yetu ya madaraka na kukimbilia chama kingine na kukipa Dola Ili kirekebishe taswira ya uchu,wizi,mauaji na kijicho vilivyomo ndani ya chama!

Leo wanakazi ya kuparuana wao kwa wao wakiwa wamegawanyika wakilinda wanaowaunga mkono ndani ya chama!!

Sarakasi za kutoana roho zinawatokea puani!!!wanachama hawaachiani maji mezani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…