Inawezekana tukawa tumenunua VAR kwaajili ya urembo

Nchi hii janjajanja na blaa blaa zimetawala, huoni uwanja wa mkapa toka ufungwe kwa marekebisho unatimiza mwaka na ushehe hakuna kitu cha kuonyesha kuna ukarabati wa maana, Zanzibar uwanja wa aman imewachukua miezi 8 tu kuukarabati na kuwa na muonekano safi na wakisasa🚮🚮🚮
 
K
Kwani tumenunua kwa hela zetu hiyo VAR? Sio kwamba ililetwa kama msaada na majaribio.
 
Hahahahaha, kelele zenu mashabiki za kutaka VAR ndio iliyopelekea watu waombe bajeti wapige hela , ila msihofu uwanja ukikamilika itafungwa bado uko ktk marekebisho.....

NB : aliyekula kala
 
Wameenda training nje ya nchi, subiria warud watakaa chumbani kwao
 
K
Kwani tumenunua kwa hela zetu hiyo VAR? Sio kwamba ililetwa kama msaada na majaribio.
 
Fifa hawacheleweshi mambo, hapa itakuwa tumepigwa tena kama ilivyoada.
hapana kupigwa,kwanza hizo var zimenunuliwa na azam sio tff,na zimenunuliwa ujerumani kwa specifications za fifa ,wakati tunasubiri kibali cha fifa mafunzo yanaendelea na fifa watakuja kukagua wao hapa tanzania ndio watatoa kibali
 
Kwa matumizi ya msimu ujao wa ligi?
 
V.A.R haitumiki kama unavyotumia simu yako, inahitaji vibali kutoka kwa wenye mpira wao pamoja na wataalam wa kuiendesha
 
V.A.R haitumiki kama unavyotumia simu yako, inahitaji vibali kutoka kwa wenye mpira wao pamoja na wataalam wa kuiendesha
Ndio umeandika kitu gani? Tokea iletwe hadi sasa imepita miezi mingapi? Kama kufatilia vibali tokea kipindi kile mpaka sasa ingekuwa wameshapata na hao wataalam kama wangepeleka mafunzo mpaka sasa wangekuwa wameshahitimu. Hapo ni usanii tu
 
Ulikuwa mbele ya muda
 
Msimu unaisha bila hata kutumika V.A.R hata mechi moja, haya si ni matumizi mabaya ya fedha? TFF wameshindwa hata kutoa ufafanuzi kama tatizo ni nini hakuna wa kutumia, au imenunuliwa mbovu au haikununuliwa kabisa? Hii nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…