Inawezekana Vodacom wamegoma kuhusu mabando

Hadi wanapandisha vifurushi maana yake walipandishiwa kodi, sasa usikute serikali haijafuta kodi iliyopandisha zaidi ya kutoa matamshi ya kisiasa kuwa warudishe vifurushi.
 
Tulishaanza kummiss hayati maana kwa kauli yake moja tangu siku ile tu wangekuwa wameitikio wito. vinginevyo Vodacom wangelia sana kwa kujiumiza wenyewe kama angechungulia aseme mara ya pili. lakini kwa sasa wanamtest mama kuona nguvu yake iko wapi .
 
Hata halotel hawajashusha!
Hawa wanasiasa bwana, walitupiga changa la macho tu
Kampuni za simu zimegoma kutii agizo la serikali na waziri na TCRA yake wameufyata,
wabunge huko bungeni mpk sasa hawaoni Kama hili la bundle ni issue, wanapiga 300k kwa siku kwa kofokeana tu btn std 7 na profs.
Kila mtu akomae na hali yake.
 
Hata airtel wamegoma pia kurudisha
 
Kwani Tz kuna vodacom peke yake? Kuwa na line zote ikizungua moja unaweka nyingine.
 
Wanahisa wakubwa ni wanasiasa wakubwa wa chama tawala akiwemo Magufuli
 
Vodacom wanazingua sana tunaomba tcra wawafuatilie wanatoa mabando tofauti tofauti sana hata mimi nimebakia na vifurushi vya 3000 mb 500 kwa wiki dk 70, sijui wanajionaje. Tutawahama tu
 
Kiongozi mmoja alisikika kabla ya kufa "Mtanikumbuka"
 
Wamebadilisha vifurushi vya Chuo, University Bundle, wakati tulikuwa tunajiunga kwa pesa nyingi kila wiki

Wajinga sana hawa Vodacom, ni kuhamia tu Airtel mkuu
 
Mimi nilikuwa nanunua 1.2GB, dakika 100 voda to voda na dakika 50 mitandao yote kww 3000/= sasahivi wamebadilisha

Hawa wameigomea TCRA na ni wa kuwahama tu kwasababu bundle za tigo na Airtel zina unafuu mkubwa kwasasa Mkuu
 
Kwa minajir hii tunaweza kusema dharau za vodacom kwa serikal na TCRA ,siwez sema serikal haina meno ilaa hawa Voda wapo wanachokitafuta.
 
Hivi mfumo.wa bando ni wa lazima au takwa la kisheria?Ikitokea wakafuta tukaanza kutumia muda wa hewani kama kawaida ilivyokuwa Zamani tuna pa kulalamika au Cha kuwafanya(Naongelea Mitandao yote,Vodacom,Halotel,Airtel,Zantel,TTCL etc.)
 
Airtel nimeangalia vifurushi wako vizuri sana shida yao bado hawasikii malalamiko ya wateja wao kuwa mtandao wao unasumbua sana. ukiwaeleza unaambiwa badili yako kuwa 4G na simu yako iwe inasupport 4G network sasa kama hatuna fedha za kununua hizo simu tuachane na Airtel?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…