Elythrobacter
Member
- Sep 29, 2020
- 47
- 94
Nimepitia masharti niliyosaini katika mkataba wa kuomba mpoto wa kufadhiri masomo yangu ya elimu ya juu,kati yangu na Bodi ya mikopo (HESLB) nimegundua sikuelewa na hata kama ningeelewa ningesaini tu, kwa sababu ya uhitaji niliokuwa nao.
Lakini kuna masharti magumu sana hasa ukizingatia hatujui kama tutapata ajira. Moja ya masharti yaliyonifanya niandike hapa ni haya hapa;
2.16 Mkopo huu utatozwa asilimia sita au asilimia nyingine itakayopangwa na bodi kwa mwaka kama garama ya kuhifadhi dhamani ya fedha (value retention fee) zitakazokopeshwa na asilimia moja ambayo ni gharama ya usimamizi wa mkopo (administrative fee) ambazo zitalipwa pamoja na marejesho ya mkopo.
2.17 Bodi itatoza asilimia 10% ya mkopo kwa mwaka kama adhabu ya kuchelewa kurejesha mkopo katika muda uliowekwa na bodi.
Najiuliza haya maswali:
- Hivi muda uliowekwa na bodi wa kurejesha mkopo ni miaka mingapi?
- Na ikitokea umestaafu hujarudisha mkopo wote inakuwaje?
- Ikitokea sijapata ajira kabisa katika maisha yangu niwa machinga tu au mkulima? Ntakamatwa na kesi ya madai?
- Je, wale walopata ajira nje ya nchi wanarejeshaje mkopo?