Inawezekanaje masoko ya Lebanon yenye matatizo mengi hivi yana tiles ila yetu hayana!

Inawezekanaje masoko ya Lebanon yenye matatizo mengi hivi yana tiles ila yetu hayana!

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Hii nchi ya Lebanon kila siku naisikia iko vitani na Waisraeli au migogoro ya siasa za ndani kwa ndani kati yao wenyewe ila nimeshangaa masoko yao yana tiles!

Sisi tunashindwaje kuweka hata zege tu bila tiles kwa soko muhimu kama la Mabibo??
Masoko yote yalitakiwa yawekwe pavement blocks.
 
Tufikie mahali tukubali ukweli, na ukweli huu utatuweka huru! kwamba waafrika hatuwezi kujitawala, na hata serikali tunazounda na viongozi wake wapo kwa maslahi binafsi na si dhamira ya kuyakomboa mataifa yao kiuchumi na kufukuza umaskini.
 
Hii nchi ya Lebanon kila siku naisikia iko vitani na Waisraeli au migogoro ya siasa za ndani kwa ndani kati yao wenyewe ila nimeshangaa masoko yao yana tiles!
View attachment 3099323
Sisi tunashindwaje kuweka hata zege tu bila tiles kwa soko muhimu kama la Mabibo??
Masoko yote yalitakiwa yawekwe pavement blocks.
Wakati magufuli anajenga masoko ya kisasa mulimwona mwehu
 
Tufikie mahali tukubali ukweli, na ukweli huu utatuweka huru! kwamba waafrika hatuwezi kujitawala, na hata serikali tunazounda na viongozi wake wapo kwa maslahi binafsi na si dhamira ya kuyakomboa mataifa yao kiuchumi na kufukuza umaskini.
Mbona magufuli alikuwa na motive ya kujenga masoko ya kisasa Tanzania nzima?
 
Usafi wa mtu unaaza ndani ya mtu, ni vigumu kuwa na gulio safi wakati getho unalokaa imeshindikana kutoa buibui juu ya paa. 🤔🤔
 
Pamoja na kwamba wapo vitani lakini wanatuzidi.sisi masoko yote mabaya tu.mfano soko la buguruni,manzese wanaita mahakama ya ndizi kama hujazoea unaweza kutapika lakini viongozi hawaoni hata aibu kuyajenga upya pamoja na kukusanya ushauri Kila siku miaka na miaka.
 
Tufikie mahali tukubali ukweli, na ukweli huu utatuweka huru! kwamba waafrika hatuwezi kujitawala, na hata serikali tunazounda na viongozi wake wapo kwa maslahi binafsi na si dhamira ya kuyakomboa mataifa yao kiuchumi na kufukuza umaskini.
Tuishie Hapa
 
Rasilimali ya kwanza na ya muhimu zaidi ni akili.
 
Hii nchi ya Lebanon kila siku naisikia iko vitani na Waisraeli au migogoro ya siasa za ndani kwa ndani kati yao wenyewe ila nimeshangaa masoko yao yana tiles!
View attachment 3099323
Sisi tunashindwaje kuweka hata zege tu bila tiles kwa soko muhimu kama la Mabibo??
Masoko yote yalitakiwa yawekwe pavement blocks.
kwa wasiojua, hezbollah kwa kuogopa kunaswa na israel, waliamua kutokutumia simu hizi za kawaida. ukitumia simu myahudi anakuona ulipo na unachokifanya kwenye simu na unaoongea nao na anakufuata na bom pale ulipo. wakaamua kununua "pagers" ambazo zinasemekana hazina network. kumbe myahudi ana uwezo kuhack hizo pagers, akasubiri kwanza wafuasi wa hezbollah wanunue na kuzitumia, wamekuwa wakizitumia kwa mafanikio. siku ya siku walipojisahau, israel akabonyeza kitufe kume zile pagers mle ndani kuna explosives, kuna namna unafanya zinalipuka.

watu wengine walikuwa sokoni kama huyo ananunua vitu, kitufe kilipobonyezwa akalipukiwa. sawa na wewe ulipukiwe na simu yako. wengi waliweka mfukoni, vikiliupka vimefyeka nyeti zao zote na testicles, kilio kikubwa huko lebanon hezbollah wengi hawana nyeti. karibia watu 4000 hadi sasa waliokua wanatumia, wengine wamelipukiwa usoni wakati wanasoma msg, wengine waliweka mfuko wambele nyeti hawana, wengine waliweka nyuma hawana makalio, wengine wamefyekwa matumbo, vifua kila mtu analia kilio chake. teknolojia imefika mbali sana. mwarabu ambaye hajawahi kuunda hata mkojo wa ngamia, anategemea kila kitu kwa mzungu kuanzia simu, bunduki, pagers, internet kila kitu, toka kwa makafiri, anaamini atakuwa salama akipambana na hao makafiri wa kizungu. kimewaramba. poleni sana.
 
Back
Top Bottom