Uchaguzi 2020 Inawezekanaje miundo mbinu iliyojengwa na pesa za watanzania wote, ionekane kuwa imejengwa na CCM pekee?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Turufu kubwa inayotumiwa na wanaCCM, ili Rais Magufuli apewe tena miaka mingine 5 ya kutawala nchi hii, ni kuwa Rais huyo amejenga reli ya SGR, amejenga mafly overs, amejenga mabarabara ya lami, anajenga bwawa la umeme katika mto wa Rufiji

Nimekuwa nikijiuliza ni kwanini juhudi zinazofanywa na watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, sifa zote achukue mtu mmoja, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ndiye Rais wetu Magufuli?

Kwa kuwa siyo siri tena, kuwa turufu kubwa wanayotumia wanaccm kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, ni ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali inayoendelea nchini, utadhani kuwa pesa ya kugharimia miundo mbinu hiyo, anatoa toka mifukoni mwake, yeye Rais Magufuli!

Hata serikali ya makaburu wa Afrika Kusini, walijenga miundo mbinu ambayo ndiyo inayongoza kwa ubora wake humu barani Afrika. Hata hivyo wananchi wa nchi hiyo, waliamua kumchagua mzalendo mweusi, Shujaa Nelson Mandela kuwa Rais wao na kuwapiga chini makaburu weupe ambao ndiyo waliokuwa wakijidai kuwa miundo mbinu hiyo imejengwa na wao.

Vile vile inajulikana kuwa pesa yote ya walipa kodi wa nchi hii, ya wanaccm na wanaChadema, zinakusanywa kwa pamoja na kuwekwa kwenye Hazina ya Taifa na ndiyo hizo zinazojenga, hiyo miundo mbinu, ambayo wanaccm "wanajimwambafai" kuwa wamejenga wao!

Wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu ni lazima watanzania tusikubali kulaghaiwa kwa hizo propaganda nyepesi kuwa eti miundo mbinu yote nchi hii imejengwa na wanaccm!

Hebu tusikilize sera za kila mgombea na wananchi tuchague kiongozi ambaye tunaamini ndiye atakayetuvusha kama Taifa, katika umoja wetu na kudumisha utulivu wa nchi hii.

Tusichague kiongozi ambaye tunamuona dhahiri kuwa analibomoa kwa kasi kubwa Taifa hili umoja wetu na kuleta chuki ndani ya jamii ya watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Bhana wee acha tuu, Hawa ni wabakaji Kama wabakaji wengine
 
CCM inatumia rasilimali za umma kujinufaisha, tulidhuhudia TBC wakirusha live mikutano yote ya ccm, lakini ya upinzani wanakimbia, lazima tubadilishe hali hii, vyama vyote vina haki sawa
Hivi kwa mfano hiki kipindi kinachoitwa kishindo cha awamu ya tano, kinachoendeshwa na televisheni ya Taifa ya TBC, kina maana gani, kama siyo kutaka kutuaminisha watanzania kuwa maendeleo yote ya Tanzania, yanatokana na yeye pekee Rais Magufuli?
 
Turufu kubwa inayotumiwa na wanaCCM, ili Rais Magufuli apewe tena miaka mingine 5 ya kutawala nchi hii, ni kuwa Rais huyo amejenga reli ya SGR, amejenga mafly overs, amejenga mabarabara ya lami, anajenga bwawa la umeme katika mto wa Rufiji

Nimekuwa nikijiuliza ni kwanini juhudi zinazofanywa na watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, sifa zote achukue mtu mmoja, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ndiye Rais wetu Magufuli?

Kwa kuwa siyo siri tena, kuwa turufu kubwa wanayotumia wanaccm kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, ni ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali inayoendelea nchini, utadhani kuwa pesa ya kugharimia miundo mbinu hiyo, anatoa toka mifukoni mwake, yeye Rais Magufuli!

Hata serikali ya makaburu wa Afrika Kusini, walijenga miundo mbinu ambayo ndiyo inayongoza kwa ubora wake humu barani Afrika. Hata hivyo wananchi wa nchi hiyo, waliamua kumchagua mzalendo mweusi, Shujaa Nelson Mandela kuwa Rais wao na kuwapiga chini makaburu weupe ambao ndiyo waliokuwa wakijidai kuwa miundo mbinu hiyo imejengwa na wao.

Vile vile inajulikana kuwa pesa yote ya walipa kodi wa nchi hii, ya wanaccm na wanaChadema, zinakusanywa kwa pamoja na kuwekwa kwenye Hazina ya Taifa na ndiyo hizo zinazojenga, hiyo miundo mbinu, ambayo wanaccm "wanajimwambafai" kuwa wamejenga wao!

Wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu ni lazima watanzania tusikubali kulaghaiwa kwa hizo propaganda nyepesi kuwa eti miundo mbinu yote nchi hii imejengwa na wanaccm!

Hebu tusikilize sera za kila mgombea na wananchi tuchague kiongozi ambaye tunaamini ndiye atakayetuvusha kama Taifa, katika umoja wetu na kudumisha utulivu wa nchi hii.

Tusichague kiongozi ambaye tunamuona dhahiri kuwa analibomoa kwa kasi kubwa Taifa hili umoja wetu na kuleta chuki ndani ya jamii ya watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
CCM ni wakora, wamepora viwanja vyote vya serikali mikoani vilivyoachwa na mkoloni na vilivyojengwa na na wananchi kwahiyo usishangae, na ili kujilinda inatumia sheria kandamizi ya uchochezi.
 
Hiki chama kimechakaa......

Kwa kuwa kimeshika madaraka tokea miaka ya 60, kwa hiyo hivi sasa kimeshachoka, kinabidi kipumzishwe kwa kutumia sanduku la kura, hapo kwenye uchaguzi mkuu, baadaye mwaka huu
 
Hoja ya msingi ni kwamba ametumia kodi ya watanzania wote vizuri au kwa ufanisi zaidi ya ilivyokuwa mwanzo (Sina uthibitisho wa kitafiti hapa, ila kuna vitu vinaonekana, wengine waweza kuweka).
Wagombea wengine wanatakiwa kushawishi wananchi kuwa wanaweza kukusanya Kodi na mapato mengine kwa ufanisi zaidi ili kuleta maendeleo endelevu zaidi.
 
lebabu11
Tunachoona hakijakaa sawa, ni kwa huyu Rais tuliyenaye kujiona kuwa apewe sifa yeye pekee, kwa kutengeneza miundo mbinu hiyo, wakati ni kodi za wananchi wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, ndiyo tuliotengeneza miundo mbinu hiyo
 
Hoja nyingine aisee zinashangaza Sana. Unashangaa hilo eti Tanzania sifa anapewa rais mbona huko nchi nyingine husemi mana nchi zote duniani Marais wanao fanya vizuri ndio husifiwa kwa kuleta maendeleo Ila akisifiwa wa Tanzania tu inakuwa nongwa.
Eti ni katumia kodi za wananchi kwani katika hizo nchi nyingine huko hao Marais wanajenga kwa pesa zao mfukoni? Mbona awamu nyingine zilishindwa kujenga hiyo miundombinu au walikuwa hawakusanyi kodi?

Kwa mfano ikitokea Lissu kashinda uchaguzi na kuwa Rais kisha akanunu meli za masafa marefu Cargo na kuzidi kuimarisha bandari, akajenga SGR hadi Mpakani na Zambia, mahospital, mashule n.k je hapo tutamsifia nani kwa hiyo kazi?

Mtu kapewa dhamana ya kuongoza taifa kakaa ofisini kwa miaka mitano akijenga nchi kwa mipango yake pamoja na Ilani ya chama chake sasa eti leo hutaki asifiwe yeye Kama sio Chuki binafsi kumbe ni nini sasa?

Halafu ccm ndio chama kilicho madarakani kwasasa hivyo Ilani inayo tumika kujenga nchi ni ya ccm sasa ni ajabu kushangaa kwanini ccm isifiwe au kuwa na nguvu.

Mbona ikifanya madudu huwa tunaisema ni serikali ya ccm ndio imeharibu Ila ikifanya mazuri hutaki tuseme ni serikali ya ccm.

Mana chama chochote kitakacho ingia madarakani kitakuwa hivo hivo, hoja Kama hizi mkienda nazo kwenye uchaguzi alafu mkawaambie wananchi wa Kigoma walio jengewa barabara nzuri kabisa ya lami Kigoma- Nyakanazi mjue kabisa mnakwenda kushindwa vibaya Sana.
 
Hamueleweki nyie juzi hapa mmeanzisha nyuzi lukuki mkimsifia JK na mkapa kwa maendeleo waliyoyafanya hamkukumbuka ni kodi zenu?
Yani ukweli ni kwamba serikali hii inamapungufu yake mengi sana tu Lakini kinachoonekana Kuna Chuki kubwa sana kwa watu wachache dhidi ya serikali bila kujali kipi hasa wanakisimamia juu ya hoja zao kipi wanapinga na kipi wanakubaliana nacho.
 
Hoja ya msingi ni kwamba ametumia kodi ya watanzania wote vizuri au kwa ufanisi zaidi ya ilivyokuwa mwanzo (Sina uthibitisho wa kitafiti hapa, ila kuna vitu vinaonekana, wengine waweza kuweka).
Wagombea wengine wanatakiwa kushawishi wananchi kuwa wanaweza kukusanya Kodi na mapato mengine kwa ufanisi zaidi ili kuleta maendeleo endelevu zaidi.
Hiki ndicho walitakiwa kufanya mkuu na si kupinga ovyo, kodi ni zetu sawa sasa je ni nani tumempa dhamana ya kuzisimamia hizo kodi? Kwani tangu tupate Uhuru hatukuwa tunakusanya kodi mbona hiyo miundombinu haikujengwa?
Waje na mipango mipya watuambie watafanya nini ili kuleta maendeleo zaidi ya haya tunayo yaona kuliko kuja na hoja kama hizi zisizo na mashiko.

mfano, Wami pele wanajengewa daraja kubwa kabisa litakalo ondoa shida waliokuwa wanapata kutokana na lile daraja la zamani hivi wale watu pale uende kuwapelekea hoja kama hii unadhani watakuelewa wale?
 
Magu kaingia kipindi smartphone sio jambo la anasa bali kila mtu ana uwezo wa kuimiliki ndio maana mnaona kila anachokifanya na wapambe wanapata urahisi kwa kupigia debe kila akifanyacho.
Umekosea kusema imejengwa na CCM, sema inaonekanaje imejengwa na Magufuli? Maana hata CCM wanamshangaa
 
Turufu kubwa inayotumiwa na wanaCCM, ili Rais Magufuli apewe tena miaka mingine 5 ya kutawala nchi hii, ni kuwa Rais huyo amejenga reli ya SGR, amejenga mafly overs, amejenga mabarabara ya lami, anajenga bwawa la umeme katika mto wa Rufiji

Nimekuwa nikijiuliza ni kwanini juhudi zinazofanywa na watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, sifa zote achukue mtu mmoja, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ndiye Rais wetu Magufuli?

Kwa kuwa siyo siri tena, kuwa turufu kubwa wanayotumia wanaccm kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, ni ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali inayoendelea nchini, utadhani kuwa pesa ya kugharimia miundo mbinu hiyo, anatoa toka mifukoni mwake, yeye Rais Magufuli!

Hata serikali ya makaburu wa Afrika Kusini, walijenga miundo mbinu ambayo ndiyo inayongoza kwa ubora wake humu barani Afrika. Hata hivyo wananchi wa nchi hiyo, waliamua kumchagua mzalendo mweusi, Shujaa Nelson Mandela kuwa Rais wao na kuwapiga chini makaburu weupe ambao ndiyo waliokuwa wakijidai kuwa miundo mbinu hiyo imejengwa na wao.

Vile vile inajulikana kuwa pesa yote ya walipa kodi wa nchi hii, ya wanaccm na wanaChadema, zinakusanywa kwa pamoja na kuwekwa kwenye Hazina ya Taifa na ndiyo hizo zinazojenga, hiyo miundo mbinu, ambayo wanaccm "wanajimwambafai" kuwa wamejenga wao!

Wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu ni lazima watanzania tusikubali kulaghaiwa kwa hizo propaganda nyepesi kuwa eti miundo mbinu yote nchi hii imejengwa na wanaccm!

Hebu tusikilize sera za kila mgombea na wananchi tuchague kiongozi ambaye tunaamini ndiye atakayetuvusha kama Taifa, katika umoja wetu na kudumisha utulivu wa nchi hii.

Tusichague kiongozi ambaye tunamuona dhahiri kuwa analibomoa kwa kasi kubwa Taifa hili umoja wetu na kuleta chuki ndani ya jamii ya watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
Hivyo vyote vinajengwa kwa kodi zetu sote na wala siyo hisani ya CCM. Hata daraja LA Kigamboni ambalo limejengwa kwa fedha za NSSF halafu hawa kwa ulofa wao watasema wamejenga wao.Hawa jamaa mshipa wa aibu hawanaga.
Tunahitaji Sera za kumkomboa Mtanzania katika Lindi LA umaskini,maradhi na ujinga ambavyo ni maadui wa asili.
Tusifanye makosa,CDM kupitia Mh.Lissu anatosha.
 
CCM inatumia rasilimali za umma kujinufaisha, tulidhuhudia TBC wakirusha live mikutano yote ya ccm, lakini ya upinzani wanakimbia, lazima tubadilishe hali hii, vyama vyote vina haki sawa
Baada ya kuzima Chanel Huru katika vingamuzi na kuibakiza hiyo TBC waliyoipora toka kuwa chombo cha umma na kuwa Mali ya CCM Mpya/Jiwe.Chombo kinachoendeshwa kwa kodi za Watanzania kinapotumika kukiuka miiko ya Uhuru wa habari na vyombo Huru vya habari huku tcra wakitumika kuzima chombo chochote wasichopendaezwa nacho.
 
TUKIACHA USHABIKI WA KISIASA
Kiongozi wa juu wa Chama aliyeko madarakani kipindi flani, NDIYE anaweza kusukuma mambo yatendeke na kwa kiasi gani
Mf: China miaka yoote iliongozwa na maraisi wazuri tu ILA alipo ingia Mao Tse Tung (mwaka 1945) ndiye aliyeleta mabadiliko makubwa ya Uchumi yanayoifanya china itishie Dunia Nzima
Tanzania kwa mfano imewaliwa na Maraisi wengi; ila Alipo ingia huyu amesukuma maendeleo kwa kiasi kikubwa naweza kusema zaidi ya mara mbili ya walio pita.
Sisemi kuwa waliopita hawajafanya kitu: Iko hivi, Raisi mmoja anaweza kujenga shule 35, mwingine ajenge 200. au mwingine anaweza kujenga Hospitali (vituo vya afya 50: Mwingine ajengine aingie ajenge 250; na miundo mbinu nk
Hivyo yule aliyeweza kusimamia na kupunguza ubadhirifu hivyo kutekeleza miradi mingi kwa kipindi chake; ndio hujivunia chama chake na sio hapa TZ ni utaratibu wa DUNIA NZIMA
China baada ya kuondoka mwenyekiti wa zidumu fikra ilifanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na lugha ili iingie kwenye dunia ya sasa.
 
Turufu kubwa inayotumiwa na wanaCCM, ili Rais Magufuli apewe tena miaka mingine 5 ya kutawala nchi hii, ni kuwa Rais huyo amejenga reli ya SGR, amejenga mafly overs, amejenga mabarabara ya lami, anajenga bwawa la umeme katika mto wa Rufiji

Nimekuwa nikijiuliza ni kwanini juhudi zinazofanywa na watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, sifa zote achukue mtu mmoja, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ndiye Rais wetu Magufuli?

Kwa kuwa siyo siri tena, kuwa turufu kubwa wanayotumia wanaccm kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, ni ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali inayoendelea nchini, utadhani kuwa pesa ya kugharimia miundo mbinu hiyo, anatoa toka mifukoni mwake, yeye Rais Magufuli!

Hata serikali ya makaburu wa Afrika Kusini, walijenga miundo mbinu ambayo ndiyo inayongoza kwa ubora wake humu barani Afrika. Hata hivyo wananchi wa nchi hiyo, waliamua kumchagua mzalendo mweusi, Shujaa Nelson Mandela kuwa Rais wao na kuwapiga chini makaburu weupe ambao ndiyo waliokuwa wakijidai kuwa miundo mbinu hiyo imejengwa na wao.

Vile vile inajulikana kuwa pesa yote ya walipa kodi wa nchi hii, ya wanaccm na wanaChadema, zinakusanywa kwa pamoja na kuwekwa kwenye Hazina ya Taifa na ndiyo hizo zinazojenga, hiyo miundo mbinu, ambayo wanaccm "wanajimwambafai" kuwa wamejenga wao!

Wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu ni lazima watanzania tusikubali kulaghaiwa kwa hizo propaganda nyepesi kuwa eti miundo mbinu yote nchi hii imejengwa na wanaccm!

Hebu tusikilize sera za kila mgombea na wananchi tuchague kiongozi ambaye tunaamini ndiye atakayetuvusha kama Taifa, katika umoja wetu na kudumisha utulivu wa nchi hii.

Tusichague kiongozi ambaye tunamuona dhahiri kuwa analibomoa kwa kasi kubwa Taifa hili umoja wetu na kuleta chuki ndani ya jamii ya watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
Tatizo ni kukosa mme ndio maana unakuwa na hoja za kipuuzi. Ina maana hujui nini maana ya chama tawala?
 
Back
Top Bottom