Inawezekanaje mwanamke aliyetolewa kizazi akapata mimba!?

blogger

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2012
Posts
12,112
Reaction score
15,060
Ni kwa Mwamposa hapa jamani. Yuko live. Dada anatoa ushuhuda anasema alitolewa kizazi Ila baada ya kuchukua mafuta ya upako kwa Mwamposa akapata Mimba.

Eee Mungu nisaidie Imani na Mimi!?๐Ÿค”๐Ÿค”๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„

Kwenu madaktari wa JF...
 
Comrade, usiwaamshe wajinga kutoka kwenye ujinga wao. Waache waendelee kuibiwa. Na uzuri jamaa kwa sasa hali peke yake!

Si umeona kule Arusha ametoa pikipiki za msaada? Unafikiri hela ya kununulia hizo pikipiki anatoa wapi? Ni kwenye hayo mafuta, maji, sabuni, na ufongo wenye upako!
 
Ni kwa Mwamposa hapa jamani. Yuko live. Dada anatoa ushuhuda anasema alitolewa kizazi Ila baada ya kuchukua mafuta ya upako kwa Mwamposa akapata Mimba.

Eee Mungu nisaidie Imani na Mimi!?๐Ÿค”๐Ÿค”๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿ™„

Kwenu madaktari wa JF...

Kutolewa kizazi (hysterectomy) humaanisha kwamba ule mji ambao mimba hupandikiza na kukua kwa miezi tisa (9) haupo. Kwa hiyo uwezekano wa kubeba mimba baada ya kizazi kutolewa haupo kisayansi.

Naheshimu imani za watu lakini nafikiri ukimhoji mhusika huenda hakutolewa kizazi, labda alifanyiwa upasuaji mwingine wa mfuko wa kizazi na siyo kutolewa kizazi.
 
Yep. Hii hoja yako ๐Ÿ‘† ๐Ÿ‘† ina mashiko. Itawafanya wadau watake kujua:
1. Anayedai katolewa kizazi ana uhakika kweli alitolewa kizazi au alisafishwa kizazi au ni nini hasa alichafanyiwa? Hii ni pamoja na elimu yake juu ya mambo ya magonjwa au changamoto za kizazi na tiba zake.
2. Anadai kapata mimba. Je, anauhakika ni mimba au ni uvimbe mahali kilipokuwepo kizazi ambacho anadai kiliondolewa? Madai yamethibitishwa na ni mimba ya miezi mingapi?
3. Haiwezekani huyo kala kolabo na matapeli ili kuwarubuni akina mama wateja waongezeke kwa Mtume halafu wakatoe ya kujimaliza???
(Tukumbuke biashara ni pamoja na matangazo).
 
Kwa mwamposa kila kitu kinawezekana mimi niliweka mafuta lita moja kwenye pikipiki yangu kisha kwenye tank la mafuta nikabandika picha ya mwamposa ni mwaka na nusu sasa ile lita moja haijawihi kuisha
 
Hivi Serikali inanufaika na nini kwa hawa manabii fekero?

Haya makanisa yanakwangua vijisenti vya watu masikini wajinga na desperate people wenye shida mbali mbali.

Serikali pigeni stop huu utapeli kwenye haya makanisa. Yanawapumbaza watu na kuwazidishia Umasikini. ๐Ÿ˜Ž

-Kaveli-
 
Well said!๐Ÿ™
 
Back
Top Bottom