Serikali ya India imeikabidhi Kenya vifaa vya matibabu vyenye thamani ya KSh83.4 milioni ili kusaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, wakati idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa nchini ikifikia wanane.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo, Jumatatu, Oktoba 19, 2026, katika ghala la Mamlaka ya Ugavi wa Dawa nchini (KEMSA) lililoko Embakasi, Nairobi.
Katibu Mkuu wa Idara ya Afya ya Umma, Mary Muthoni, alipokea msaada huo kutoka kwa Balozi Mkuu wa India nchini Kenya, Dkt. Adarsh Swaika, akisema vifaa hivyo vitasaidia kuwalinda wahudumu wa afya wanaohudumia wagonjwa wa Ebola.
Msaada huo unajumuisha mavazi 6,000 ya kujikinga na maambukizi (PPE), barakoa 30,000 za N95, vifaa 60 vya kusaidia kuchuja hewa wakati wa kupumua na zaidi ya vifaa 86,000 vya kusafirisha sampuli za wagonjwa kwa uchunguzi.
Pia kuna glavu, mavazi ya hospitali, vifaa vya kulinda uso, buti na vipimajoto vinavyotumia miale ya infrared.
Kwa mujibu wa Muthoni, vifaa hivyo vitasambazwa katika hospitali zinazotibu wagonjwa wa Ebola, vituo vya kuwatenga wagonjwa, timu za dharura na maeneo ya mipakani ambako wasafiri wanafanyiwa uchunguzi wa afya.
Msaada huo unakuja wakati Kenya ikiendelea kupambana na maambukizi ya aina ya Bundibugyo, baada ya kisa cha kwanza kuthibitishwa mapema mwezi huu kwa mgonjwa aliyekuwa amesafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kufikia Oktoba 18, Kenya ilikuwa imethibitisha visa vinane vya Ebola na kifo kimoja, huku baadhi ya walioambukizwa wakiwa wahudumu wa afya waliokuwa wakimhudumia mgonjwa wa kwanza.
Soma Visa vya Ebola Kenya vyafikia 8, Muhudumu wa Hospitali ya Nairobi aambukizwa
Wizara ya Afya imesisitiza kuwa juhudi za kutambua wagonjwa mapema, kuwatengea maeneo maalum na kuimarisha usafi na kinga hospitalini zinaendelea.
Serikali pia imewataka Wakenya kuwa watulivu lakini waangalifu, huku ikisisitiza umuhimu wa kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ili kuzuia maambukizi zaidi.