Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dennis Bergkamp vs Everton
akiwa na miaka 36 ya kuzaliwa
Morrison vs Simba ( 08/03/2020 )
Maradona world cup 1986 Argentina vs England.
Ana sifa ,alikuwa na uwezo wa kumfunga kipa akiwa mbali bado akamfuata na kumpiga chenga
♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
Mchezo wa soka ni mchezo unaohitaji, team work ili ufanikiwe, lakini Mara kadhaa hutokea kwamba mchezaji fulani akacheza kwa jitihada sana kuliko wenzake na kusababisha ushindi. Ifuatayo ni baadhi ya Individual performance bora ziliwahi kutokew kwenye mpira. (Kwa mtazamo wangu)
Usisahau kuweka na za kwako
8. Andrey Arshavin vs Liverpool
Wakati huo Liverpool alikua na ndoto za kuchukua ubingwa wa england akichukuana na Man U, lakini kumbe Arshavin alikua na lake kichwani. Arshavin alitupia goli nne peke yake.
7. Canavaro vs German
Inatajwa mechi bora kuliko zote za World Cup 2006, wakati wenyeji German chini ya kocha wao Klinsman wakitaka kubakiza kombe nyumbani, Canavaro akiongoza ngome yake vizuri na kuhimili mashambulizi yote ya Ujermani. Mechi ikiisha kwa Italy kushinda goli 2-0 na kutinga fainali
Mechi hii ndio iliyosababisha apewe tuzo ya Balon O dor baadaye, nadhani ndio beki pekee duniani kuwa mchezaji bora wa dunia.
6. Gareth Bale Vs Inter Milan
Kuna watu wawili hawatakaa waisahau hii mechi. Moja ni Bale mwenyewe maana mechi hii ya Uefa ndio iliyomtambulisha kwenye ulimwengu wa soka na kumfanya awe mtu mwingine kabisa. Na mwingime ni Maicon beki wa kulia bora kabisa akiwa anamuweka Dani Alves benchi kwenye team ya taifa ya Brazil. kwenye hii mechi maicon alidhalilishwa mno na Bale na ndio ukawa mwanzo wa mwisho wa Maicon. Bale akifunga hat trick.
5. Ronaldo De Lima vs Man U
Nadhani ilikua mechi ya nusu fainali au robo final ya UEFA, mechi ya kwanza Real alishinda 2-1 nadhani (sina uhakika) baada ya mechi fergie akihojiwa akasema anaomba Mungu Raul asiwepo mechi ya marudiano, nadhini maombi yake yakasikilizwa, Raul akaumwa na kidole tumbo mechi ya marudiano Old Trafford. Ronaldo alipiga Hat trick japo Man alishinda 4-3, ila Ronaldo aliupiga mwingi sana. Hata hivyo Man U walitolewa kwenye aggregate.
4 Xavi Hernandez vs Real Madrid
Nadhani kila mtu anamjua huyu maestro kwa kupiga pasi na kumiliki mpira, Fergie siku moja aliwahi kutania kuwa katika maisha yake yote amewahi kumuona xavi amepoteza pasi Mara mbili tu. Siku hiyo Madrid walidhalilika katika uwanja wao wa Bernabeu kwa kupigwa kipigo cha goli 6 - 2, na xavi akia -assist goli NNE kati ya sita.
3. Roy Keane Vs Juventus
Hii mechi ndio iliyompa U-Legend Roy Keane, mechi ya kwanza ya nusu fainali ya UEFA 1999 ilichezwa Old Trafford na ilitoka 1-1, watu wengi ikiwemo mm niliamini kuwa Man u ni nje. katika uwanja wa Dele Alp mjini Turin mpaka half time Juve alikua anaongoza goli 2-0, huku Kean akipewa kadi ya njano, na akijua kwa kadi hyo hawezi kucheza final, akaamua kufungulia mabomba yote. Siku hyo aliwakalisha chini Zizou, Edgar Davis na Didier Deschchamp pale katikati,kwa wale wanaofahamu shughuli ya huo utatu atanielewa namaanisha nini. Man U walienda na kushinda 3-2 na kuingia final.
2. Rolaldinho vs Real Madrid
Ni Mara chache sana mashabiki kumshabikia mchezaji wa team pinzani hasa ikizingatiwa ni Derb ya Madrid na Barcelona. Ronaldinho alikiwasha mno siku hiyo nadhani Michael Salgado na Sergio Ramos walilala na viatu. Kwenye mechi hiyo alipiga goli mbili kali sana Barca ikishinda 3-0, wakati anatoka mashabiki wa Madrid walisimama kumpigia makofi.
1. Zinadine Zidane vs Brazil
Nusu fainal nyingine matata sana ya world cup 2006, Brazil ikiwa na mastaa kibao kama Ronaldinho, Ronaldo de Lina, Kaka, Adriano nk. Zizou aliwakalisha wote chini, akicheza ile staili yake maarufu kama hataki vile aliwapiga kanzu, vyenga, pasi za visigino nk. mastaa wote wa Brazil walikubali kuwa zizou ni maestro wa eneo la kiungo. Na pia ndio aliyepiga pasi ya goli kwa Thiery Henry. Kwenye hiyo mechi hakuna chochote cha maana cha kukumbukwa zaidi ya care free performance ya Zizou.
Kwa msaada wa mtandao wa give me sport.
Ana sifa ,alikuwa na uwezo wa kumfunga kipa akiwa mbali bado akamfuata na kumpiga chenga
♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
Hii ndio kali na bora ya muda wote
Sent from my iPhone using Tapatalk
Messi vs Arsenal; Messi Vs Real Madrid; Messi vs Bayern Munich; Messi vs Juvetus; Messi Vs Brazil...Messi Messi.....
Thierry Henry vs Inter Milan
Hii game ilinipa mchuchu wa Diploma kipindi hicho.
Nakumbuka game 1 Arsenal alikuwa amekufa 3 kwa 0 kwenye makundi Highbury.
Sasa game ya pili inaanza, nikamwambia mdau mmoja kwamba hii game Inter atakufa, ukumbi mzima wakawa wananizomea kwa kuangalia game ya kwanza na hii Vieira hakuwepo, nilizomewa sana, sasa mimi nikawaambia tusubiri tuone.
Jamaa anayeonesha mpira tukakubaliana kwamba Arsenal akifungwa namlipa 20,000 na siangalii tena mpira kwenye ukumbi wake na akishinda nitaangalia mpira bure mpaka msimu uishe.
Sasa wa kumpa aishike hiyo 20,000 ndo nikamchagua dada mrembo tulikuwa tumekaa viti vinafatana.
Kikichotokea yule dada akawa ananionea huruma goli la kwanza liliporudi, Thierry akafanya maajabu yake, na ile twenty nikamwachia yule dada kwamba iwe kiingilio chake cha kuwa anakuja kumwangalia Thierry.
Ndo tukawa tumeanzia hapo.
Ile game ilikuwa ni [emoji91]
Kuna goli hilo, kuna goli like kawatungua tottenham kakimbia na mali toka golini kwao, kuna goli against madrid, kuna goli aliwafunga liver akamgaragaza jammie carragher.
Kwangu he is the best nyuma ya de lima.
Pamoja na kuwa sikuwa mshabiki wa Arsenal, chogo nilikuwa namwelewa sana.
Nilianza kumwona world cup anaingia kama sub anavaa 12 (France 98 WC), babu Wenger alivyomsajili nilifurahi sana, na nimeangalia games nyingi za Thierry.
Alikuwa ana style yake ya kuutuliza mpira, anapanda juu halafu anashuka nao. Na kuna ile ya kukimbia na mpira kwenye chaki akifika karibu na kibendera ndo anarudi ndani.