Indonesia: Kila mwaka katika Kisiwa cha Sulawesi wafu hufukuliwa, kubadilishwa nguo, kuvutishwa sigara n.k, kama ishara ya kudumisha mapenzi kwao

Indonesia: Kila mwaka katika Kisiwa cha Sulawesi wafu hufukuliwa, kubadilishwa nguo, kuvutishwa sigara n.k, kama ishara ya kudumisha mapenzi kwao

Pascal_TZA

Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
27
Reaction score
76
Kila mwaka huko kaitika Kisiwa cha Sulawesi, Tana Toraja, Indonesia, wafu hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo na kuwatembeza Kijini hapo, watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila ya ajabu inayoiitwa Ma’nene ambayo wanaamini mtu akifa bado yuko nao kwa hiyo inawalizimu kufanya mambo hayo kama kuwabadilisha nguo.

Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia, idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.

Mzizi wa imani ya utamaduni wa Manine ni kwamba “mapenzi kati ya binaadamu na wanafamilia hayawezi kuisha kamwe hata baada ya kifo”.



 
Sisi ni wamavumbini na mavumbini tutarudi, na kwa kutowarudisha mavumbini maiti wetu tunamkosea sana Mwenyezi Mungu.
 
Haya mambo hata kama ni mila.ila kusumbua wafu sio kuzuri
 
Back
Top Bottom