Pre GE2025 INEC watoa elimu kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ili kuliweka tayari Jeshi la Polisi wakati wa mchakato wa Uchaguzi

Pre GE2025 INEC watoa elimu kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ili kuliweka tayari Jeshi la Polisi wakati wa mchakato wa Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Mambo yanazidi kuiva..

====

Screenshot_20241112_235819_Instagram.jpg

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika kuhakikisha inatoa Elimu ya Mpiga Kura kwa makundi mbalimbali katika jamii, Novemba, 2024 imetoa elimu hiyo kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) nchini katika mafunzo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo ya siku moja kuhusu Sheria na Kanuni zinazoiongoza Tume, Mkurugenzi wa INEC, Bw. Kailima Ramadhani amesema

"Kimsingi hawa ndio wasimamizi wa sheria ngazi ya Wilaya kutoka Jeshi la Polisi, hivyo tumewapitisha katika Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na.2 ya Mwaka 2024 na Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 ili iwawezeshe kuzitafsiri vyema hizi sheria na zitawawezesha katika usimamizi bora wa majukumu
yao bila kuleta mtafaruku kati ya chama cha siasa au na wananchi kiujumla".

Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji amesema lengo la mafunzo hayo ni kuliweka tayari Jeshi la Polisi wakati wa mchakato wa uchaguzi na huku akibainisha kuwa Jeshi hilo ndio wasimamizi wa sheria na walinzi wa raia na mali zao.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Dodoma: Jeshi La Polisi lapigwa msasa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu namna bora ya kuendesha Uchaguzi Mkuu 2025

Orkonerei Radio
 
Wasimamizi wa CCM wakiwa kambini mafunzo namna ya kuiba kura na kuibakisha CCM madarakani.... Hiyo ndio habari ulitakiwa uandike.
 
Back
Top Bottom