leefrankne
Member
- May 8, 2025
- 7
- 5
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, leo tarehe 31 Agosti, 2025 imekaa na kujadili rufaa kuhusu uteuzi wa wagombea Ubunge katika Jamhuri ya Muungano na Udiwani kwa Tanzania Bara zilizowasilishwa Tume kwa ajili ya uamuzi.
=============
KUHUSU UAMUZI WA RUFAA DHIDI YA UAMUZI WA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KWA PINGAMIZI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO NA UDIWANI KWA TANZANIA BARA
Dodoma, Tarehe 31 Agosti, 2025
Kwa mujibu wa kifungu cha 53 na 65 vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, baada ya uteuzi kufanyika, wagombea Ubunge na Udiwani wanaruhusiwa kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi.
Kifungu cha 53(6) na 65(7) vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 vikisomwa pamoja na kanuni ya 29(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025 vinaeleza kuwa, mgombea yeyote ambaye hakuridhika na uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi kuhusu uhalali wa pingamizi lililowekwa anaweza kukata rufaa kwa Tume ndani ya saa ishirini na nne tangu uamuzi ulipotolewa. Tume inaweza kukataa au kukubali rufaa husika wakati wa kufanya uamuzi.
Kwa kuzingatia masharti ya vifungu tajwa vya Sheria, hadi kufikia tarehe 31 Agosti, 2025 zimepokelewa rufaa 33, kati ya rufaa hizo, rufaa 13 zimefanyiwa uamuzi na Tume, ambapo kati yake rufaa nane (08) ni za kupinga uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kuhusu Ubunge na rufaa tano (05) ni kupinga uamuzi kuhusu Udiwani.