GE2025 INEC yapitisha vyama 17 kuwania Urais Oktoba 29, 2025

GE2025 INEC yapitisha vyama 17 kuwania Urais Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Vingine Mbona ni kama Cooperative Union au Saccos fulani hivi?...African farmers kweli?...daaah!
 
Kinachofanywa na Msajili na INEC kinasadifu uhalisia wa watanzania wengi.
  • Wengi ni wanafiki;
  • Wengi ni wapuuza;
  • Chiki zimewajaa;
  • Hodari wa kusema tuu;
 
Siku si nyingi hawa wanaofanya maigizo watasimama kizimbani wakipigwa mvua kwa huu usanii wanaotufanyia leo.

Hiyo tarehe 26 Oktoba wote tusijitokeze kwenda kuhalalisha huu upumbavu.
 
Marehemu Shehe Yahya alishawahi kutabiri kuwa akitoka Rais Kikwete atakuja Rais atakayetwala kwa muda mfupi(Magufuli)na baada ya hapo atatokea Rais mwanamke na baada ya hapo upinzani watachukua nchi!
Imethibitika Rais Samia hana ushawishi wowote kuanzia ndani ya chama chake hadi kwa wananchi wote kwa ujumla. Rais Samia licha ya kuwa makamu wa rais kwa miaka 5 anaonekana hajui matatizo ya watanzania na wala hajui watanzania wanataka nini. Serikali ya Rais Samia kila kukicha inajitenga na wananchi wanyonge kwa kuwapatia huduma mbovu sana kwenye kila nyanja. Rais Samia hajui kukemea rushwa na ufisadi. Hajui umuhimu wa viwanda kwa watanzania .
Kutokana na ulegelege huu ikitokea kwenye uchaguzi mkuu akawekwa Rais Samia na Tundu Lisu basi utabiri wa shehe Yahya unatimia asubuhi na mapema kwa Rais Samia kushindwa vibaya sana kwenye sanduku la kura na Tundu Lisu wa chama cha upinzani kuibuka mshindi na kushika dola.
 
Urejeshaji fomu za kugombea urais umekamilika leo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), ambapo mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, alizuiwa kuingia kutokana na kukosa vigezo.

Kwa mujibu wa kanuni za chama hicho, mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa awe mwanachama aliyehudumu ndani ya chama kwa angalau siku 30 kabla ya uteuzi, jambo ambalo Mpina alishindwa kutimiza.

Mpina, ambaye aliwasili saa 6:40 mchana akiwa na mgombea mwenza wake, alizuiwa getini na maafisa wa Tume na kuambiwa wasubiri nje. Hata hivyo, hadi mwisho wa siku, yeye pamoja na wafuasi wake hawakuruhusiwa kuingia ndani kurejesha fomu hizo.

Awali, ACT-Wazalendo walieleza matumaini ya kurejesha fomu hizo ili kujiandaa kuanza kampeni rasmi katika maeneo mbalimbali nchini, lakini walikumbana na kikwazo hicho.

Wagombea wa Vyama VingineMgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwa na mgombea mwenza wake Dk. Emmanuel Nchimbi, walifanikiwa kurejesha fomu zao kwa mujibu wa ratiba ya Tume.

Mbali na CCM, vyama vingine vilivyorejesha fomu ni: NRA, AAFP, Chama Makini, NLD, UPDP, ADA TADEA, UMD, TLP, CCK, CHAUMMA, DP, SAU, CUF, ADC, UDP, NCCR-Mageuzi na UMD.

Wagombea wa Urais Tanzania 2025

1. Chama Cha Mapinduzi (CCM)
  • Samia Suluhu Hassan - Mgombea Urais
  • Emmanuel Nchimbi – Mgombea mwenza
2. National Reconstruction Alliance (NRA)
  • Hassan Kisabya Almas - Mgombea Urais
  • Hamis Hassan - Mgombea mwenza
3. Alliance for African Farmers Party (AAFP)
  • Kunje Ngombare Mwiru – Mgombea Urais
  • Chumu Abdallah Juma – Mgombea mwenza
4. Chama cha Maarifa, Kilimo na Nishati (MAKINI)
  • Coaster Kibonde – Mgombea urais
  • Aziza Haji Suleiman – Mgombea mwenza
5. National League for Democracy (NLD)
  • Doyo Hassan Doyo – Mgombea urais
  • Chausiku Khatibu Mohamed – Mgombea mwenza
6. United People’s Democratic Party (UPDP)
  • Twalib Ibrahim Kadege – Mgombea Urais
  • Abdalla Mohamed Khamis – Mgombea mwenza
7. Chama Cha African Democratic Alliance Party (ADA TADEA)
  • George Bussungu – Mgombea Urais
  • Ali Issa Makame - Mgombea mwenza
8. Chama Cha Union for Multiparty Democracy (UMD)
  • Mwajuma Noty Mirambo – Mgombea Urais
  • Mashavu Alawi - Mgombea mwenza
9. Chama cha Tanzania Labour Party (TLP)
  • Yustas Rwamugira – Mgombea Urais
  • Aman Seleman Mzee - Mgombea mwenza
10. Chama cha Kijamii cha (CCK)
  • David Daud Mwaijele – Mgombea Urais
  • Masoud Ali Abdalla - Mgombea mwenza
11. Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)
  • Salum Mwalimu – Mgombea Urais
  • Devotha Minja - Mgombea mwenza
12. Chama cha Democratic Party (DP)
  • Abdul Mluya – Mgombea Urais
  • Abrahman Khatib - Mgombea mwenza
13. Chama cha Sauti ya Umma (SAU)
  • Majalio Paul Kyara – Mgombea Urais
  • Satia Mussa Bebwa - Mgombea mwenza
14. Chama cha Wananchi (CUF)
  • Gombo Gombo – Mgombea Urais
  • Husna Mohamed Abdalla - Mgombea mwenza
15. Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC)
  • Wilson Elias Mulumbe – Mgombea Urais
  • Shoka Khamis Juma - Mgombea mwenza
16. Chama cha United Democratic Party (UDP)
  • Saum Rashid – Mgombea Urais
  • Juma Hamis - Mgombea mwenza
17. Chama cha National Convention for Construction and Reform – Mageuzi (NCCR-MAGEUZI)
  • Haji Ambar Khamis – Mgombea Urais
  • Dkt. Eveline Wilbard Munisi - Mgombea mwenza

Chanzo: Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
Hii nchi inawasomi wapo kwenye nyadhifa mbalimbali ikiwemo INEC ila mambo yanayofanyika unabaki kushika kichwa.
 
Back
Top Bottom