Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza kuwa Novemba 04, 2026 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Mkoa wa Dodoma, pamoja na Madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ramadhani Kailima, imesema uchaguzi huo unafanyika kufuatia kuwepo kwa nafasi wazi za uongozi katika maeneo ya uchaguzi, na kwamba Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, baada ya Rais Samia Suluhu kumteua aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Deogratius John Ndejembi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uteuzi wake uliofanyika Agosti 26, 2026 na kuthibitishwa na Bunge Agosti 28, 2026.
Kailima kupitia taarifa hiyo amesema Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 57(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya 343 ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana juu ya uwepo wa nafasi wazi za madiwani 11 kwa Tanzania bara.
Amesema "Tumepokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuhusu uwepo wa nafasi wazi za madiwani 11 kwa Tanzania Bara. Nafasi hizo wazi zilitokana na vifo vya madiwani nane (08) kwa nyakati tofauti na madiwani watatu (03) kujiuzulu" hivyo tume imesema fomu za uteuzi kwa wagombea wa Ubunge Chamwino na Udiwani katika kata 11 zitatolewa kuanzia Oktoba 7 hadi 13, 2026, huku zoezi la uteuzi wa wagombea likifanyika Oktoba 13, 2026 ambapo baada ya uteuzi, kampeni za uchaguzi zitaanza Oktoba 14, 2026 na kuendelea hadi Novemba 03, 2026.
Tume imevikumbusha vyama vya siasa, wagombea na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Katiba, sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya Tume katika kipindi chote cha utekelezaji wa ratiba hiyo.
Soma pia