Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewateua makada 17 kutoka kwenye vyama mbalimbali vya siasa kuwania ubunge wa Isimani mkoani Iringa ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, William Lukuvi, aliyefariki Machi 25, 2026.
Watiania walioteuliwa na INEC ni pamoja na Emannuela Mtatifikolo (CCM), Farida Mwapungu (Demokrasia Makini), Asha Chuma (UPDP), Fidelis Mtikile (Sau), Hadija Makawa (Ada-Tadea), Protas Mgimbila (CCK), Zavely Seleleka (UDP), Berbard Mwingila (DP) na Burton Chitenga (NCCR Mageuzi).
Wengine ni Christina Mbaunga (NRA), Mark Mhemela (AAFP), Nassim Upete (CUF), Mwaka Mgimwa (TLP), Asma Othern (UMD), Maimuna Lumato (ADC), Daudi Masasi (Chaumma) pamoja na Subira Kalolo (NLD).
Ushindani huo unatajwa kuwa miongoni mwa chaguzi ndogo zenye mvuto wa kisiasa kutokana na idadi kubwa ya wagombea watakaoshiriki huku kila chama kuteka imani ya wananchi wa Isimani ili kushinda nafasi hiyo muhimu ya uwakilishi bungeni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 11, 2026 mkoani Iringa, msimamizi wa uchaguzi wa INEC katika jimbo hilo, Caroline Otieno amesema kukamilika kwa hatua ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi kumeashiria mwanzo rasmi wa mchakato wa kampeni kwa wagombea waliokidhi masharti ya uchaguzi.
Chanzo: Mwananchi