GE2025 INEC yavitaka Vyombo vya Habari kuomba vibali vya kuripoti Uchaguzi Mkuu 2025

GE2025 INEC yavitaka Vyombo vya Habari kuomba vibali vya kuripoti Uchaguzi Mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kwa kuzingatia kifungu cha 26 cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatoa mwaliko kwa vyombo vya habari vyenye nia ya kuchapisha au kutangaza habari wakati wa kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo.


Chombo cha Habari kinachohitaji kuomba kibali kinapaswa kuwa na sifa au vigezo vifuatavyo:
(i) kiwe kimesajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya Mwaka 2016; na
(ii) kihakikishe kuwa waandishi wake wamethibitishwa na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari na wana Press Cards zilizotolewa na Bodi hiyo.


Maombi yawasilishwe kupitia mfumo wa usajili Accreditation Management System (AMS) unaopatikana kupitia kiunganishi (link) AMS

snapins-ai_3713529037361525349.jpeg
 
wavifunge vyote ibaki TBC Tu lakini NO REFORMS NO ELECTION huu ndiyo msimamo wa wenye akili wale wa matiki waendelee kutumia cables zao zilizounganishwa hapo NEC
 
Back
Top Bottom