GE2025 INEC yawaonya CCM Kigoma mjini, 'Msiharibu uchaguzi'

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Its Tesha

Senior Member
Joined
Oct 6, 2025
Posts
168
Reaction score
608
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kupitia kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini, David Rwazo, imetoa onyo kali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kigoma baada ya Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Jimbo hilo kubaini vitendo kadhaa vinavyokiuka maadili ya uchaguzi vinavyofanywa na baadhi ya wanachama na wagombea wa chama hicho katika eneo hilo.

Katika barua yake rasmi iliyotumwa tarehe 16 Oktoba 2025 kwenda kwa Katibu wa CCM Kigoma ambayo Jambo TV imeiona, Rwazo amesema Kamati hiyo katika kikao chake cha Oktoba 15, 2025, ilibaini vitendo visivyofaa vinavyohusishwa na CCM, vikiwemo kung’oa na kuchana mabango ya chama cha ACT Wazalendo, kufanya mikutano nje ya ratiba, kutumia lugha zisizo na staha dhidi ya mgombea wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kata ya Rubuga, na kuingilia misafara ya vyama vingine.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya wanachama wa CCM wamekuwa wakifunika mabango ya ACT Wazalendo katika maeneo ya wazi, hususan eneo la ‘roundabout’ Mwanga, jambo ambalo limeelezwa kuwa ni ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi.

Msimamizi huyo wa Uchaguzi pia amelaani tukio la mgombea udiwani kupitia CCM katika kata ya Katubuka, Daniel Rumenyela, kumtolea lugha za matusi Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa ngazi ya kata, akisema kitendo hicho kisirudiwe tena.

“Kwa mujibu wa Kanuni ya 4.1(g) ya Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ina wajibu wa kukemea vitendo vyenye vinaweza kuharibu uchaguzi vinavyoweza kufanywa na viongozi wa vyama vya siasa, wagombea, wanachama, serikali na watendaji na vyombo vyake”, imeeleza taarifa hiyo.

Rwazo amesema, ikiwa CCM au wagombea wake wataendelea na vitendo hivyo, Tume haitasita kuzuia mikutano yao ya kampeni itakayosalia katika jimbo hilo.

Amehitimisha kwa kulitaka Jeshi la Polisi kuendelea kufuatilia kwa karibu shughuli za kampeni na kuchukua hatua stahiki pale kanuni za maadili zinapokiukwa, sambamba na kuwataka wadau wote wa uchaguzi kuhakikisha kampeni zinafanyika kwa amani, heshima na utii wa sheria.
1760724695361.png
 
Hizo ni porojo tu kwa ccm
 
Ukiona hivyo, unue wameelekezwa na CCM kusema hivyo, kwa sababu Kigoma CCM wameamua kumpa ubunge Zito ili kuwahaaa punguani wa akili waamini kuwa kulikiwa na uchaguzi.
 
Back
Top Bottom