Inflammatory ya tumboni chanzo chake nini?

magange

Member
Joined
May 30, 2015
Posts
65
Reaction score
15
Amani iwe kwenu wapendwa. Nimesumbuliwa na tatizo la tumbo kwa muda mrefu huku nikienda hospitali tofauti bila bila kupata matibabu ya moja kwa moja. Hivi karibuni nilifanya uchunguzi tena ndio ikagundulika kuwa nina tatizo linaloitwa CHRONIC INFLAMMATORY. Je tatizo hili linasababishwa na nini na matibabu yake ni nini? Maana dawa nitumiazo mpaka niambiwe niache na Dr na ni baada ya kupewa masharti ya kuacha baadhi ya vyakula. Naomba msaada wenu wapendwa.
 
Mkuu hakuna tatizo kama hilo katika Medical, hiyo ni General Term kuelezea Severenity ya tatizo na siyo tatizo lenyewe.

Kamuulize tena daktari tatizo lako ni lipi.
 
Mkuu hakuna tatizo kama hilo katika Medical, hiyo ni General Term kuelezea Severenity ya tatizo na siyo tatizo lenyewe.

Kamuulize tena daktari tatizo lako ni lipi.

au labda anamaanisha Inflammatory Bowel Diseases kama Ulcerative Colitis na Chrohns disease...
 
au labda anamaanisha Inflammatory Bowel Diseases kama Ulcerative Colitis na Chrohns disease...

Asante kwa ushirikiano wenu. Katika cheti cha majibu nilichopewa kimeandika chronic inflammatory ila katika dawa nizitumiazo dosage yake ni katika kipengele cha Inflammatory bowel. Hicho cheti ndicho kimenipelekea kusema nina chronic inflammatory
 
ilitakiwa uzitaje dawa ndipo itajulikana ndugu.
 
Dawa nizitumiazo zinaitwa SULFASALAZINE TABLETS 500Mg

dah! pole sana mkuu... najua shida unayopitia...

hizo dawa ni kwa ajili ya inflammation huwa zinatumika kwa watu wa Rheumatoid Arthritis, Ulcerative Colitis na Chrohns disease hizo ni autoimmune diseases...

ulifanya vipimo gani?! ulipiga Colonoscopy au Barium Enema kwa hilo tatizo lako?!

Hizo dawa zinakuwa zinapunguza inflammation kwa hospital kutibu hilo tatizo ni issue, kwa ulcerative colitis kutibu hilo tatizo ni kwa surgery wanakata ile sehemu ya colon iliyo athirika halafu wanaunga au unatolewa colon yote...

Chrohns ni iko challenge sana challenge kuitibu, kwa hospital wanasema no cure kwa hayo magonjwa wanaita idiopathic yaani unknown causes...

dawa hizo ni kwa ajili ya kupunguza inflammation na kupunguza attack ili uweze ku maintain remission kwa kipindi kirefu...

kwa ulcerative colitis, hospital cure ni kwa surgery
Darren Fletcher aliyekuwa mchezaji wa Manchester alikuwa na hilo tatizo yeye alipona kwa surgery...

lakini kuna jamaa mmoja hapa jf anaitwa Deception nilisoma sehemu akasema autoimmune disease zinatibika kwa tiba mbadala labda aje atueleze ni kwa namna gani autoimmune kama hizo zinatibika namna gani?!
 
Last edited by a moderator:

Asante Mkuu kwa udadavuzi wa kina!!!!! Vipi kuhusu Gastric Esophageal Reflux Desease (GERD) je inasababishwa na nini na matibabu yake huwa ni nani??
 
Last edited by a moderator:
 
Pole sana kwa uvimbe ulikuwa nao tumboni usiotibika Mahospitalini ukishindwa kupona hospitali nione mimi ninaweza kukutibia na ukapo ukihitaji mimi nikutibie bonyeza hapa.Mawasiliano
 
Asante mpendwa kwa ushirikiano wako na Mungu akubariki. Kipimo nilichopima ni COLONOSCOPY. Swali linakuja kwamba wanapotoa hiyo colon inakuwaje( mtu anaishi baada ya kutolewa )?
Mtu anaishi baada ya kutolewa, wataalamu wanajua namna gani ya kufanya ila unaweza ukapitia maelezo hapa chini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…