Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Wana JF, kuna neno nimepewa na mchumi maarufu hapa nchini. Nadhani wengi mmesikia maelezo yasiyoridhisha kuhusu kushuka thamani kwa shilingi japo ya hatua nyingi zilizochukuliwa na serikali ambazo kimsingi zinapaswa kuongeza thamani ya shilingi na kupunguza sana inflation.
Inachanganya kichwa kufikiria nini kinasababisha haya yote, maana ni kama yanapingana na kanuni za uchumi. Kwa kibano na udhibiti tulivyo navyo chini ya awamu ya tano, inflation ilitakiwa ipungue sana, na thamani ya shilingi kubaki stable. Lakini thamani imeendelea kushuka, na mwezi December inflation rate ilipanda kutoka 3.0% hadi 3.3%, japo wananchi hawana fedha mkononi na mzunguko wa fedha umepungua sana.
Sasa kuna tetesi kwamba huenda serikali ya Tanzania imekuwa ikichapisha kisiri fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli mbali mbali nchini ambazo zinahitaji fedha za ndani. Kuchapisha fedha ni jambo la kawaida, lakini huwa kunafanywa kwa mahesabu sana, kufidia fedha zilizoharibika na kiasi fulani kuongeza mzunguko. Lakini baadhi ya viongozi wa nchi wasiojua uchumi wamekuwa wakitoa amri kuchapisha fedha zaidi ya kiwango kinachotakiwa ili kuipa serikali fedha za ndani kuendesha shughuli zake. Kwa kifupi, badala ya serikali kutumia fedha za mapatao ya kodi nk, inachapisha fedha zake yenyewe.
Baadhi ya wachumi wetu wanaanza kuhisi huenda hili sasa linafanyika nchini kisiri. Binafsi sijui kama ni kweli litakuwa na athari gani nchini, ukizingatia kwamba mzunguko wa fedha umebanwa sana. Je linaaweza likawa si baya sana kwa kuwa kuna upungufu mkubwa wa fedha mikononi mwa watu?
Wenye uelewevu wa haya mabo tunaomba mtusaidie.