Inflation na kushuka kwa thamani ya shilingi kusikoeleweka; Serikali inachapisha fedha kisiri kugharamia shughuli za serikali na miradi mikubwa?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Wana JF, kuna neno nimepewa na mchumi maarufu hapa nchini. Nadhani wengi mmesikia maelezo yasiyoridhisha kuhusu kushuka thamani kwa shilingi japo ya hatua nyingi zilizochukuliwa na serikali ambazo kimsingi zinapaswa kuongeza thamani ya shilingi na kupunguza sana inflation.

Inachanganya kichwa kufikiria nini kinasababisha haya yote, maana ni kama yanapingana na kanuni za uchumi. Kwa kibano na udhibiti tulivyo navyo chini ya awamu ya tano, inflation ilitakiwa ipungue sana, na thamani ya shilingi kubaki stable. Lakini thamani imeendelea kushuka, na mwezi December inflation rate ilipanda kutoka 3.0% hadi 3.3%, japo wananchi hawana fedha mkononi na mzunguko wa fedha umepungua sana.

Sasa kuna tetesi kwamba huenda serikali ya Tanzania imekuwa ikichapisha kisiri fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli mbali mbali nchini ambazo zinahitaji fedha za ndani. Kuchapisha fedha ni jambo la kawaida, lakini huwa kunafanywa kwa mahesabu sana, kufidia fedha zilizoharibika na kiasi fulani kuongeza mzunguko. Lakini baadhi ya viongozi wa nchi wasiojua uchumi wamekuwa wakitoa amri kuchapisha fedha zaidi ya kiwango kinachotakiwa ili kuipa serikali fedha za ndani kuendesha shughuli zake. Kwa kifupi, badala ya serikali kutumia fedha za mapatao ya kodi nk, inachapisha fedha zake yenyewe.

Baadhi ya wachumi wetu wanaanza kuhisi huenda hili sasa linafanyika nchini kisiri. Binafsi sijui kama ni kweli litakuwa na athari gani nchini, ukizingatia kwamba mzunguko wa fedha umebanwa sana. Je linaaweza likawa si baya sana kwa kuwa kuna upungufu mkubwa wa fedha mikononi mwa watu?

Wenye uelewevu wa haya mabo tunaomba mtusaidie.
 
Inawezekana tukizingatia iyo theory,tungesema hoja kwamba mzunguko ni mkubwa lakini ni kinyume chake.
 
Synthesizer
Inflation ilikuwa 4.4% Mwaka jana November. Imepungua karibu 25%. Na ni inflation ya chini katika miaka ishirini iliyopita.
Kwa hiyo hakuna kitu kama hicho.

Katika kipindi hichohicho, RMB thamani yake imeongezeka by 2.2% only, na thamani ya Indian Rupee imeongezeka by 0.5% hii ni almost flat hasa ukizingatia hawa ni major trading partners wa Tanzania.

Tunaikuza sana hii inflation wakati hamna kitu kama hicho. Ni uongo.
 
Printing money creates a sense of nervousness amongst both economists and the general public. It immediately conjures up memories of hyperinflation in Weimar Germany in 1923 and Zimbabwe in more recent times.
If a government prints money faster than the growth of real output it reduces the value of money and this invariably causes inflation. Governments often resort to printing money when they cannot finance their borrowing by selling bonds. This hyperinflation can be extremely damaging to an economy.
 
Synthesizer
Inflation ilikuwa 4.4% Mwaka jana November. Imepungua karibu 25%. Na ni inflation ya chini katika miaka ishirini iliyopita.
Kwa hiyo hakuna kitu kama hicho.

Katika kipindi hichohicho, RMB thamani yake imeongezeka by 2.2% only, na thamani ya Indian Rupee imeongezeka by 0.5% hii ni almost flat hasa ukizingatia hawa ni major trading partners wa Tanzania.

Tunaikuza sana hii inflation wakati hamna kitu kama hicho. Ni uongo.
Good point Mkuu. Ila suala la ku-print hela inasemwa ni la hivi karibuni, haliendi nyuma zaidi ya mwaka. Kuna theory kwamba ilionekana halitatuathiri kwa kuwa tayari kuna udhibiti mkubwa sana wa fedha. Na pia eti kwa sababau kuwa matajiri wameamua kuhodhi (hoard) fedha!
 
Ngumu kumesa kwa kutumia theories za kawaida.
 
Ngoja niwe mpenzi msomaji,mtaambiwa mnakwamisha juhudi za Maendeleo
 
Mbona bank bado wanatoa ela zilizochakaa?? (a bit of professional joke)
====
Mleta mada naomba utufahamishe utaratibu rasmi unaotumiwa na Tanzania ku'print' fedha zake.
 
Inategemea nchi. Jambo la kawaida ni ku-print kiasi cha fedha zilizoharibiwa kwa kuchakaa au sababu nyingine. Pili wanaangalia uhitaji wa fedha nchini kuangalia waongeze kiasi gani (incremental money supply), kulingana na kukua kwa uchumi. Kwa mfano wanaweza kutumia GDP wakaamua wata-print 2% ya GDP. Na pia wanaweza kuamua ku-print kulingana na inflation rate iliyopo - yaani kama inflation iko juu sana basi si vema kuprint hela zaidi. Kwa hiyo BOT watakuwa wanatumia vigezo fulani kati ya hivi, au na zaidi.

Tatizo ni pale mkuu wa nchi zisizo na utawala wa sheria anatoa amri tu kwa Benki Kuu - chapisha manoti zaidi tukakamilishe miradi kwa fedha zetu!
 
Back
Top Bottom