Unajua ushabiki uko wa aina nyingi... Kuna mtu anashabikia ujuzi binafsi wa mchezaji, mwingine anashabikia jitihada binafsi za mchezaji... na mwingine udambwiudambi wa mchezaji kwake sio deal ila mchezaji kaisaidiaje timu kufikia malengo... Sasa tuwachambue..
Pele> Mfalme wa soka anaishi: Huyu jamaa ni balaa,, labda tufe wote then wazaliwe wengine ndiyo atokee kama yeye... Kwanza fikiria amecheza kipindi hicho black au waafrika tulikuwa hatuthaminiwi kama watu,.. wazungu walikuwa wanatudharau na kutuona kama hazijatimia.. Lakini huyu mwanaume aliwaonyesha kazi.. piga goli kama mvua,, japo hakuwa mtu wa udambwi sana lakini aliamini kuisaidia timu yake kwa kufunga magoli ndiko kitu muhimu katika maisha yake ya soko..
Maradona> Huyu jamaa yuko vizuri mno kwenye kuchezea mpira (ball dancer).. Ufupi wake na kasi ulimsaidia sana kutesa mijitu yenye miraba minne ya Ulaya... Japo alikuwa na kapaji na kuisaidia timu yake lakini hakujitambua kapewa kipaji na mungu ili akifanyie nini.. Uvutaji madawa na ulevi vilimfanya ashindwe kuvunja rekodi za Pele...
Ronaldinho Gaucho>.. Huyu jamaa ni kizazi kipya cha soka. vyenga vya hatari, dribbling za kutosha, nguvu na kumiliki mpira huyu jamaa utampenda.. Tatizo la dunia ya sasa watu wanaweka rekodi kwa maana umefunga magoli mangapi, assist ngapi na umenyanyua kwapa mara ngapi... sio vyenga, cjui kazu, tobo.. no, huo mpia sasa hivi hakuna.. Ulikuwepo enzi ya Maradona.... Japo kabeba vikombe kadhaa kwa timu zake, Barcelona na Brazil lakini historia za wachezaji wa zamani wa timu hizo zinamficha asionekane..
Messi>.Sasa kwa mpira wa kisasa huyu ndiyo mwenyewe... Waswahili wanasema kila kizazi na nabii wake.. Kwenye mpira wa leo huyu jamaa ni nabii wetu. Kumbuka mpira wa sasa unaunganisha style zote hizo za juu na kuziweka pamoja.. Messi anajua kuuchezea mpira, vyenga vipo, anajua nini timu yake inataka ndiyo maana huwa hajing'ang'nizi kufunga hata kama hayuko kwenye nafasi.. Lakini muhimu kuliko yote ni determination ya kuvunja record za dunia na huwezi kuzivunja kama huna discipline ya kwako mwenyewe pamoja na timu kwa ujumla.. Ukitaka kuamini angalia timu nzima ya Barcelona yaani kila mchezaji jicho kwa Messi na kila mmoja anafurahia mafanikio ya huyu dogo.. Aombe kwa Mungu aendelee kuwa na maisha marefu ya soka may be, just may be anaweza akafikisha magoli 1000 kama si kuvunja kabisa rekodi ya Pele.. Ana miaka 27 mungu akimjalia acheze miaka saba mingine katika kiwango hiki tutakuwa tunazungumzia mengine...
CR7> Anaujua.. Mchezaji mwenye kaliba zote za soka la kisasa... kasi, nguvu na chenga zake za break ni balaa.. Unajicho lenye lenzi kali sana ya goli liliko.. Kachukua ufundi kidogo wa maradona na umakini wa Pele.. Ila tatizo kwa CR7 ni kama Nabii asiyekuwa na kizazi. kwa maana gani..? kumbuka kuwa CR7 alianza kutamba kipindi wafalme wengine wanatawala.. Amemkuta Ronaldo mwenyewe, alimkuta Zinedine Zidane mbaya zaidi alimkuta Ronaldinho Gaucho yuko moto vibaya sana...!! Ingekuwa ngumu kwake kutamba mbele wa miamba hao.. Sasa hao jamaa enzi zao zilivyoisha bahati mbaya tena kwake, kizazi kipya cha soka kinaibuka, makao makuu Katalunya.. Anakutana na kina Messi wananjaa ya kufa mtu.. tatizo jingine akaenda Real Madrid ambao ni mahasimu wa Barcelona... Kwa misimu kama mitatu mfululizo Madrid wameteseka sana kwa Barcelona.. Hicho ndicho kinachomficha CR7 awe nyuma ya hao vigogo wa soka waliowahi kutokea duniani..
Hizi tuzo za FIFA wakati mwingine ni mbwembwe tu.. Ila record zinabaki kama msahafu.
Kama una swali uliza, kama una ya kuongeza uongeza!!