Ingawa sijawaona Pele na Maradona, ila nina uhakika hawamfikii Gaucho

Ingawa sijawaona Pele na Maradona, ila nina uhakika hawamfikii Gaucho

Upo sahihi, tactical skills kadiri siku zinavyokwenda zinazidi kuwa juu na kila erA ina top aces, Pele na Maradona walikuwa wa Kwanza kuleta mabadiliko ya ufundi wa mpira ndiyo maana their legacy well appreciated tho hawakua na ushindani kama wa leo hii
 
Pele na D10S hujawaona, huo uhakika unautoa wapi? Bora ungesema una 'amini', halafu huu ni 'mpira wa miguu /football" sio mpira wa mgongo. Na hivi mbwembwe za kuuchezea mpira ndio zinamfanya mchezaji kuwa bora zaidi? Kama ni hivyo basi Okocha alikua bora kuliko Weah
Bila kuweka vigezo vya kutoa mwongozo wa kulinganisha na kutofautisha ubora wa mchezaji mmoja mmoja, kila mtu atakuja na mchezaji wake na kuandika ngonjera kama hizo zako.
Na ungetaka msaada wa kumsifia Dinho kwa mbwembwe, tambo, majigambo, ngonjera na danganya toto za kufa mtu, ungemuita huyu buluda, Gang Chomba, maana huyu ukiwa karibu yake ukamsema vibaya Dinho, anaweza kukugeuza kitumbua

ha ha ha hivi Gang Chomba? Sipati picha anavyojisikia kuhusu Ac Milan yake.
 
Last edited by a moderator:
Messi na Gaucho ni naona Messi ni moto wa kuotea mbali.
Ronaldinho usimweke kabisa Level ya Maradona hata Pele.
Nilikuwa naangalia Clip za Maradona majuzi nikagundua kuwa huyu jamaa alikuwa anacheza mpira ambao leo Messi ndo anaucheza.
Hapigi chenga bila sababu za msingi wala hakai na mpira mda mrefu.
Maradona sio mtu wa kucheza na Jukwaa ila ni mtu wa kucheza mpira haswaa, ni kama leo tunavyomuona Messi.
Ronaldinho anacheza na Jukwaa harafu Show nyingi ndani ya Uwanja ndo maana hata mashabiki wake wakiangalia mpira wanataka kila mara mpira apewe Ronaldinho ili waone atafanya kituko gani, hii ni tofauti na Messi, Pele na Maradona na hata na Cristiano Ronaldo.
Ronaldo ana maslahi binafsi ktk Ulimwengu wa Soka na si ktk Timu yake.
 
MFUKUZI

Mkuu pongezi kwa kutoa ufafanuzi.

Huwa nashangaa kwa nini watu hupenda kuwalinganisha wachezaji ambao aidha wanacheza nafasi tofauti au walicheza kipindi tofauti?

Hao waliotajwa hapo juu wote ni GREAT PLAYERS, na kama suala ni kulinganisha great players kwa nini watu hawawataji kina Alfredo Di Stefano, Ferenc Puskas, Bobby Charton, Johan Cruyff, Franz Beckenbauer, Eusebio, Zico, Romario, Michel Platini, George Weah, Ruud Gullit, Marco Van Basten, Zinedine Zidane, Gheorge Hagi, Enzo Scifo, Hristo Stoichkov na wengineo?

Kama mtu unampenda mmoja wapo haina tatizo lakini kila siku oh mara Messi bora kuliko CR7 and vice versa, mara Gaucho ni bora kuliko Messi na CR7, mara Messi bora kuliko Pele n.k ...

Ni mambo ya kitoto.
 
Last edited by a moderator:
Sahau kina pele na maradona Ronaldinho ni kitu kingine,weka mbali takataka kama messi na christiano.Kwenye historia ya mpira ushawahi kumwona nani bonge la shuti katuliza kwa mgongo na ikakaa?

Kama hujawaona umefikiaje tamati yako?
 
Pele na D10S hujawaona, huo uhakika unautoa wapi? Bora ungesema una 'amini', halafu huu ni 'mpira wa miguu /football" sio mpira wa mgongo. Na hivi mbwembwe za kuuchezea mpira ndio zinamfanya mchezaji kuwa bora zaidi? Kama ni hivyo basi Okocha alikua bora kuliko Weah
Bila kuweka vigezo vya kutoa mwongozo wa kulinganisha na kutofautisha ubora wa mchezaji mmoja mmoja, kila mtu atakuja na mchezaji wake na kuandika ngonjera kama hizo zako.
Na ungetaka msaada wa kumsifia Dinho kwa mbwembwe, tambo, majigambo, ngonjera na danganya toto za kufa mtu, ungemuita huyu buluda, Gang Chomba, maana huyu ukiwa karibu yake ukamsema vibaya Dinho, anaweza kukugeuza kitumbua

uzuri wa dinho alikuwa ana udundi sio mbwembwe kama unavyoziita unaleta ladha kumtazama pia alikuwa anasaidia timu yake kumbuka aliipa barca mataji ya kutosha na yy mwenyewe kawa mchezaji bora wa dunia mara2 Halafu akatajwa tena ndio mchezaji bora wa muongo mmoja una chakupinga kuhusu dinho?
 
Last edited by a moderator:
Gaucho alishawahi kutangazwa man of the match wakati hajacheza, tena alikuwa jukwaani kabisa , namkubali sana huyu jamaa
 
kwa show game gaucho yuko poa lakini hajadumu kwenye game bana..
Jay Jay Okocha alikuwa na show-game na kuleta impact kwenye timu na amedumu kwa kipindi kirefu, sema tu ni mwafrika ndio maana historia yake imefutika kwa kipindi kifupi

Dinho made Barca...hilo uliweke akilini
 
Ubora na umaarufu wa mchezaji ni kuwezesha timu yake kuchukua ubingwa na pia kuwezesha timu yake ya taifa kuchukua ubingwa wa dunia ndivyo Pele na Maredona walivyofanya. Huyo unayemtaja nini amefanya kwa timu ya taifa lake kuwezesha kuchukua kombe la dunia? Usipime kwa mtazamo wako ila angalia macho ya wengi pamoja na jopo la vyombo vya habari na wataalamu wa mchezo huo kwa vigezo vyenye mizani ya ukweli si ushabiki wa kile moyo ukipenda.

ulikuwapo wapi kuangalia kombe la Dunia mwaka 2002?
au Dada alikuwa hajaolewa mjini bado so wewe ulikuwa kijijini bado?
 
Mwaka 1961, Pele alitangazwa na rais wa Brazil kipindi hiko kama 'Hazina ya taifa'
Jiulize kwanini? Naungana na jamaa aliesema labda dunia yote tufe wazaliwe wengine

Pele ni habar nyingine kwenye mpira
 
Mwaka 1961, Pele alitangazwa na rais wa Brazil kipindi hiko kama 'Hazina ya taifa'
Jiulize kwanini? Naungana na jamaa aliesema labda dunia yote tufe wazaliwe wengine

Pele ni habar nyingine kwenye mpira

Nasikia kipindi cha Pele hakukuwa na Offside, mshambuliaji akivizia anajifungia tuu.
 
ulikuwapo wapi kuangalia kombe la Dunia mwaka 2002?
au Dada alikuwa hajaolewa mjini bado so wewe ulikuwa kijijini bado?

Messi>.Sasa kwa mpira wa kisasa huyu ndiyo mwenyewe... Waswahili wanasema kila kizazi na nabii wake.. Kwenye mpira wa leo huyu jamaa ni nabii wetu. Kumbuka mpira wa sasa unaunganisha style zote hizo za juu na kuziweka pamoja.. Messi anajua kuuchezea mpira, vyenga vipo, anajua nini timu yake inataka ndiyo maana huwa hajing'ang'nizi kufunga hata kama hayuko kwenye nafasi.. Lakini muhimu kuliko yote ni determination ya kuvunja record za dunia na huwezi kuzivunja kama huna discipline ya kwako mwenyewe pamoja na timu kwa ujumla.. Ukitaka kuamini angalia timu nzima ya Barcelona yaani kila mchezaji jicho kwa Messi na kila mmoja anafurahia mafanikio ya huyu dogo.. Aombe kwa Mungu aendelee kuwa na maisha marefu ya soka may be, just may be anaweza akafikisha magoli 1000 kama si kuvunja kabisa rekodi ya Pele.. Ana miaka 27 mungu akimjalia acheze miaka saba mingine katika kiwango hiki tutakuwa tunazungumzia mengine...

Bora ungeongelea huyu Messi wa kutoka nchi ya Maradona anayechezea Bac ambaye ameshafikisha kiwango cha kuvunja rekodi ya Pele wiki iliyopita wakati bado umri unadai sana kimchezo kwa kupachika mabao ndiye habari ya mujini. Achana na ushabiki pamoja na hoja ya nguvu, ukitumia nguvu ya hoja kama sisi tunaongea kwa data yakhe huna sababu ya kupimwa kwa kikutokacho mdomoni mwako na kukuchafua kuliko kikuingiacho.
 
hakuna mchezaji anayeweza kufika level za gaucho naumia sana kuona alikiwa pik kwa muda mfupi ila hao wote mnaowataja kwa dinho hawanusi
 
Sahau kina pele na maradona Ronaldinho ni kitu kingine,weka mbali takataka kama messi na christiano.Kwenye historia ya mpira ushawahi kumwona nani bonge la shuti katuliza kwa mgongo na ikakaa?

Gaucho is the greatest player of all the times and indeed is second to none
 
Sijawahi waona maradona na pele. Kwenye kizazi changu naukubali mpira wa ronaldinho. Cr7 ni mchezaji anajituma sana.
 
Back
Top Bottom