Pele na D10S hujawaona, huo uhakika unautoa wapi? Bora ungesema una 'amini', halafu huu ni 'mpira wa miguu /football" sio mpira wa mgongo. Na hivi mbwembwe za kuuchezea mpira ndio zinamfanya mchezaji kuwa bora zaidi? Kama ni hivyo basi Okocha alikua bora kuliko Weah
Bila kuweka vigezo vya kutoa mwongozo wa kulinganisha na kutofautisha ubora wa mchezaji mmoja mmoja, kila mtu atakuja na mchezaji wake na kuandika ngonjera kama hizo zako.
Na ungetaka msaada wa kumsifia Dinho kwa mbwembwe, tambo, majigambo, ngonjera na danganya toto za kufa mtu, ungemuita huyu buluda,
Gang Chomba, maana huyu ukiwa karibu yake ukamsema vibaya Dinho, anaweza kukugeuza kitumbua