Vyuo vikuu ni eneo la kuzalisha first class professionals. Sasa kwa huu mtazamo wako ni kama unasema sasa vyuo vikuu viwe na mtaala mmoja unaofanana kitu ambacho kikifanyika maana ya University haipo tena kwa maana ya kwamba hii itadidimiza ugunduzi na uzalishaji wa maarifa mapya kwa wanafunzi. Pili, kwa vyuo vingi, nafikiri mitihani ina michakato kuanzia ile ya ndani mpaka ya nje ambayo haitoi mwanya hata kidogo kwa mwalimu kumuonea mwanafunzi. Hoja hii ya kwamba waalimu wanawaonea ama kuwapendelea wanafunzi inatolewa na wanafunzi wenye udhaifu ama mapungufu fulani fulani. Mitihani ya vyuo vikuu hupitia michakato mingi, kuanzia kwa moderators, exerminers boards, watahini huru wa ndani na baadaye watahini huru kutoka nje ya nchi. Hawa wote huangalia ubora wa mtihani na usahihishaji wa mtihani wa mwanafunzi mmoja hadi mwingine. Kwa namna hii, hii hoja ya mwalimu kumkosesha mwanafunzi kwa sababu tu ana kisa naye hukosa nguvu kabisa.