Ingekuwa heri JK uage sasa!!

Ingekuwa heri JK uage sasa!!

Kashaija

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2008
Posts
255
Reaction score
62
Ingekuwa heri JK uage sasa


MHESHIMIWA Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, salaam aleykum. Juma lililopita
niliwasiliana na Watanzania wote kwa njia hii ya makala.
Nilijaribu kuwachokonoa ili kupata mawazo yao juu yako.

Na kwa bahati nzuri nilikuwa nimeongea moja kwa moja na
Watanzania wote wakiwamo wasaidizi wako muhimu. Na ili
kuwahakikishia kwamba niliwalenga na wao pia niliamua
kuwataja kabisa pale niliposema, "Yote kwa yote ni
kwamba
kila mtu anajua sasa Rais Kikwete uwezo wake wa
kuliongoza
taifa na chama chake umepungua.

"Ninaamini ndani ya dhamiri yangu kwamba hata
wasaidizi wake, wakiwamo usalama wa taifa, mawaziri na
manaibu mawaziri, wanamtandao na wapambe wake, wabunge,
viongozi wenzake ndani ya chama, watendaji wake
serikalini
na wasaidizi wake wengineo wote wanajua hili".

Nilifanya hivyo kwa makusudi ili kupata maoni yao juu ya
hili. Nawatambua sana wasaidizi wako. Ni watu mahiri sana
kwa kulinda maslahi yao na ya wakubwa wao. Nilijua
watanijibu haraka haraka kwa kukanusha ukweli huo mdomoni
huku mioyoni mwao wakiutambua. Lakini hawakufanya hivyo.
Hii inathibitisha kwamba hata wao ukweli uliwagusa na
wamefikia mahali ambapo hawawezi kupingana nao.

Wa kwanza kabisa kuwasiliana nami ni kiongozi wa zamani wa
CCM katika mojawapo ya nafasi za uongozi ndani ya chama
ngazi ya kitaifa. Yeye alinipigia simu kabisa na
kujitambulisha kwa jina, nami nikamtambua kwa sauti
kwamba
ni yeye. Akanipongeza kwa kusema nimeandika vizuri sana na
kwa kweli maneno yake na sauti yake yalionyesha dhahiri
kukubaliana na ukweli niliouainisha.

Huyu ndiye akazidi kuthibitisha nilichokizungumza katika
aya hiyo hapo juu. Ukweli umewasuta ndani ya dhamira zao
na
kwa kweli umefika wakati ambao ukweli hauwezi kufichika
tena. Wengi sasa wanaogopa kukutetea hadharani
wasijeonekana vituko kwa kuupinga ukweli ulio wazi (naked
truth).

Mheshimiwa Rais, wasomaji walionitumia ujumbe mfupi wa
simu, walionipigia simu, walionitumia barua pepe na hata
waliozungumza nami uso kwa uso, wote wamenipongeza kwa
ujumbe uliokuwa wazi ukieleza ukweli halisi na kila mmoja
wao aliishia kusema 'atang'oka' 2010. Baada
ya
kutafakari ujumbe wa wasomaji na matukio yaliyoripotiwa
kwenye vyombo vya habari juma lililopita, nimeamua
kukuandikia waraka huu ili nikupatie ushauri makini
lakini
bure.

Msomaji mmoja, kwa mfano, aliongea kwa uchungu jinsi
ulivyojibu swali la mwanahabari kule Ufaransa.
Ulipokuuliza
kwa nini nchi yako ni maskini ukasema eti hata wewe
hujui.
Kwa maoni yake ilikuwa ni aibu kubwa kwa kiongozi wa nchi
kujibu hivyo tena mbele ya viongozi na wanahabari wa
kimataifa. Uliuonyesha ulimwengu kwamba nchi hii ni ya
ajabu na watu wake ni wa ajabu. Ni kama ulikuwa
unathibitisha kauli iliyopata kutolewa na mwandishi mmoja
kwamba Tanzania ni nchi pekee duniani inayoweza kukaa
miaka
10 bila rais na bado ikabaki na amani.

Kwa maoni yangu pia, rais wa nchi kusema hajui umaskini wa
wananchi wake unatokana na nini ni sawa na kusema nchi
haina kiongozi. Rais wa namna hiyo hawezi kuhangaika na
mipango ya kuiondoa nchi katika umaskini, maana hajui kwa
nini wananchi ni maskini. Anafikiri pengine ni
"wavivu tu
wa kufikiri" ama "fursa zipo ila kwa ujinga wao
hawataki
kuzitumia".

Rais wa namna hiyo hawezi kujua madhara ya ufisadi wa EPA,
Meremeta, Tangold, Kiwira, mikataba ya Richmond, IPTL na
jinsi inavyochangia umaskini wa watu wake. Hawezi kuona
ubaya wa rais na mke wake kujiingiza kwenye biashara kwa
kutumia ofisi, fursa na vyeo vyao vya Ikulu kuwanyonga
wananchi. Na kwa sababu hiyo hawezi kujihangaisha
kuyashughulikia madudu kama hayo kama unavyofanya wewe
hivi
sasa.

Rais wa namna hiyo atakuwa 'busy' na safari za nje
zisizo na kikomo, kukutana na marais wakubwa kama akina
George Bush tena wanapokutana Bush atampiga piga mabegani
rais kama huyo kama alivyofanya alipokuja hapa Dar es
Salaam, na tungetamani kupata tafsiri ya kitendo hicho
cha
George Bush, ambaye wafuatiliaji wanasema hata
mlipokutana
Japan alikupiga piga begani tena, kutoka kwa Salva
Rweyemamu yule mwandishi wa zamani aliyeisakama serikali
kwa kalamu yake, lakini baadaye akawa mwanakampeni wako
mahiri kwa kutumia kalamu hiyo hiyo na baadaye
ukamzawadia
ukurugenzi wa mawasiliano Ikulu.

Mheshimiwa, watu wanashangaa hata kitendo cha serikali yako
kushindwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maji,
visivyokauka
tulivyonavyo hapa nchini na ardhi safi tena kubwa
inayofaa
kwa kilimo cha umwagiliaji kujihakikishia chakula cha
kutosha. Lakini badala yake unakwenda Italia kwa kutumia
mamilioni ya shilingi kuomba chakula kwa WFP.

Mheshimiwa Rais, si siri ni aibu kubwa. Mabilioni
yaliyopotea kwenye ufisadi yangetosha kuanzisha
'scheme' kubwa 13 za umwagiliaji kwenye mikoa 13
ya
nchi hii. Na hesabu zake ni rahisi mno wala huhitaji
kutumia shahada yako ya kwanza ya uchumi ambayo hata
hivyo
sijui kma umewahi kuitumia.

Chukua milioni 152 kwa siku kwa mwaka mmoja tu zilizolipwa
kwa Richmond/Dowans ambazo kwa siku 365 za mwaka ni
bilioni
55. Jumlisha bilioni 2,098 zilizolipwa kwa IPTL kwa miaka
minane tu kwa kuzingatia kauli ya aliyekuwa Naibu Waziri
wa
Nishati na Madini, William Ngeleja, bungeni Dodoma
Agosti6,
2007 kwamba kwa kipindi cha Julai 2005 hadi March 2006
peke
yake IPTL ililipwa jumla ya bilioni 262.3. Kwa vipindi
vinane tu kama hivyo kampuni hiyo imelipwa jumla ya
bilioni
2,098. Jumlisha bilioni 133 zilizoibwa kupitia EPA, kisha
juu yake ongeza bilioni zisizopungua 600 zilizopotea
kupitia ujenzi wa minara miwili pacha pale BoT. Halafu
umalizie na mabilioni yaliyopotea kupitia viufisadi
vingine
vingine kama ubinafsishaji wa TTCL, NBC, Kiwira, n.k
ambazo
nazo si chini ya 100.

Halafu chukua hiyo jumla inayofikia bilioni 2,986 bila
kuongeza bilioni ulizozitumia wewe kwa safari zako za nje
tangu uchaguliwe kuwa rais. Igawanye jumla hiyo kwa
gharama
za mradi mzima wa kupeleka maji Shinyanga ulioshikiwa
bango
na best yako ili aje kuonekana anafaa kuwa waziri mkuu wa
nchi hii. Utapata 13 ambazo ni scheme kubwa za
umwagiliaji
zenye thamani ya sh bilioni 225 kila moja.

Ina maana tungeweza kuwa na scheme kama hizo katika mikoa
13 inayoongoza kwa ardhi inayofaa kwa umwagiliaji. Njaa
ingetupata wapi. Hivi sasa dunia inapolia na kupanda kwa
bei za vyakula sisi tunaoita kilimo uti wa mgongo wa
uchumi
wetu tungekuwa matajiri kwa kuuza chakula.

Lakini hivi sasa eti serikali yako inapiga marufuku kuuza
chakula nje ya nchi, mkulima anayetegemea kuuza chakula
chake cha ziada ili apate matumizi yake mengine ikiwamo
kusomesha watoto unamwambi nini?

Mheshimiwa Rais, watu waliodunisha maisha ya Watanzania
kiasi hicho eti bado hutaki kuwachukulia hatua hadi leo.
Umeunda tume juu ya tume nyingine lakini mafisadi
wanaendelea kutesa. Ajabu zaidi chama unachokiongoza juma
lililopita, kimetangaza eti kumpa onyo kali aliyekuwa
naibu
meya wa Ilala na kumzuia kugombea cheo chochote zaidi ya
udiwani alionao, sababu eti ni kushiriki bomoabomoa ya
Tabata Dampo na kuisababishia hasara serikali ya sh
bilioni
1.8, kuwasababishia usumbufu wananchi wa Tabata Dampo na
kukiaibisha chama.

Gazeti hili likaiandika habari hiyo Jumatatu wiki hii, kwa
kichwa kilichosema; 'CCM yacharuka'. Naomba
kupingana moja kwa moja na maneno aliyoyatumia mwandishi
wa
habari hiyo. Kimsingi CCM haijacharuka. Bali ina mkakati
pengine unaosimamiwa na wewe mwenyewe mwenyekiti wako
kukisafisha chama. Msitudanganye kiasi hicho, kwamba mna
uchungu sana na pesa za serikali, mnawajali wananchi na
kulinda hadhi ya chama chenu.

Fikiria hasara za mabilioni ya serikali niliyoyataja hapo
juu, yote yamesababishwa na wana-CCM, fikiria Watanzania
milioni 40 wanaoteseka kwa ajili ya wana CCM na ukumbuke
jinsi hadhi, si tu ya chama unachokiongoza bali pia ya
serikali unayoiongoza ilivyoporomoka ndani ya mwaka
mmoja,
kwa ajili ya wana-CCM. Lakini hamjawakaripia wala
kuwafuta
uanachama kama mlivyofanya kwa Naibu Meya Yakubu.

Huu ni usanii ambao umeshajulikana kwa Watanzania.
Mheshimiwa Rais, juma lililopita umetoa kali nyingine ya
mwaka. Umewaasa Watanzania wavumilie shida wasikate
tamaa.
Hii nayo ni kauli nyingine ya mzaha kwa Watanzania kama
ile
ya kusema hujui umaskini wao unasababishwa na nini.

Natamani ungekuwa unasoma maoni ya wasomaji. Siku hizi
Tanzania Daima imeanzisha sehemu ya maoni ya wasomaji
wanaosoma gazeti hili, kwenye tovuti. Msomaji mmoja
aliposoma alisema hivi: "Kaka yetu usipate tabu wewe
sema
tu.

Sisi tumezoea shida, huna tofauti na Karume anayewaambia
Wazanzibari watazoea tu. Sasa sisi tumezoea na wewe
endelea
kula nchi maana mafuta si kazi yako. Wewe linda mtandao
wako
usisambaratike, maana inabidi uutumie kurudi madarakani
mwaka 2010." Haya si maoni ya mtu anayekuambia kwa
wema.
Huyu ana uchungu ndani ya moyo wake na kwa ujumla maneno
yake ni laana kwa serikali yako.

Mwingine akasema hivi: "...Kikwete suala la mafuta na
maisha magumu havimhusu kabisa. Ndiyo, si anatuonyesha
hivyo kwa kuwalinda mafisadi? Na sasa kapata kisingizio
cha
bei ya mafuta basi ndiyo itakuwa hadithi. Hivi
wadanganyika
wenzangu mnafikiri bei ya mafuta ikishuka (let's say)
hadi nusu, ndiyo maisha yatakuwa bora kwa kila
mdanganyika?
"Dhahabu imepanda sana bei katika soko la dunia. Kwa
nini vitu kama hivi vimeshindwa kufidia pengo la mafuta
yaliyopanda?

Watu wengine wanafananisha Bongo na Marekani - eti na
Marekani maisha yamepanda. Nyie ndugu zangu hebu acheni
mzaha! Wewe unakula humburg na pizza Macdonald halafu
unatuambia maisha yamepanda? "Chonde chonde jamani.

Natamani mngerudi huku mkapigika mkashindia kauzu ndiyo
mngejua watu wanaongea nini…" Ukurasa huu
hautatosha
kukupatia maoni ya kila msomaji, lakini natamani
ungejisomea mwenyewe habari hiyo kisha chini yake usome
maoni ya watu.

Wasaidizi wako wanaweza kukusaidia kutembelea
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/21/habari1
Mheshimiwa Rais ningekushauri jambo moja tu. Kukubali pia
ni uungwana wa aina yake na Watanzania wanapenda watu
waungwana.

Baada ya ziara yako ndefu mkoani Tanga, utakaporejea Ikulu
fanya jambo moja tu. Andaa hotuba yako ya mwezi bila
kumshirikisha msaidizi wako yeyote. Ita waandishi wa
habari
kana kwamba unakuja kujibu tu maswali watakayokuuliza
halafu
wakisha fika toa hotuba yako kabla hujaulizwa maswali.

Waeleze wanahabari na Watanzania kwa ujumla kwamba wakati
unachukua fomu za kugombea urais mwaka 2005 hukuijua
vizuri
sababu ya umaskini wa Watanzania. Waeleze kwamba wewe
ulidhani kazi uliyokuwa nayo ni kuwaita tu wawekezaji
uliokuwa umeshazoeana nao sana ukiwa waziri wa Mambo ya
Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, na kwamba wakishakuja
kuwekeza
tayari maisha bora kwa kila Mtanzania yanajipa.

Sema kwamba umekuja kugundua kuwa mambo sivyo yalivyo.
Umaskini wa Watanzania una uhusiano wa karibu mno na
utawala wa nchi. Na kwamba utawala wa nchi kwa miaka
mingi
umebaki kuwa mbovu hasa kupitia 'system'
iliyojengwa na
Chama chako Cha Mapinduzi ya kulindana viongozi, bila
kujali
madhara yanayosababishwa na viongozi mafisadi hapa nchini
na
hivyo hata malaika akiwa rais wa nchi hii kupitia CCM
hakuna
maendeleo yatakayopatikana.

Sema wazi wazi kwamba kama rais wa nchi hata kama ungekuwa
na dhamira ya kuikwamua nchi kutoka kwenye umaskini
unaosababishwa na uongozi mbovu, ungeshindwa kwa kuwa
kikulacho ki nguoni mwako. Maswahiba zako waliofanya juu
chini upate urais ndiyo hao hao mafisadi waliokubuhu hata
jina la mafisadi haliwafai tena. Nasikia wengine wameanza
kuwaita 'mafisidi'.

Na wewe huwezi kuwatupa wakati ungali ukikumbuka mchango
wao mwaka 2005. Kwa sababu hiyo, ili kulinda uhusiano
wako
nao na wakati huo huo kulinda heshima kupita kiasi
uliyopewa na watanzania, umeamua kuachia ngazi na hivyo
mwaka 2010 hutagombea tena.

Wapatie Watanzania nafasi ya kuanza kufikiria tangu sasa
chama kitakachowafaa kuongoza nchi hii hapo 2010,
kutokana
na sera zake kabla hawajafikiria ni nani atawafaa kuwa
rais wa nchi baada yako. Uhakika mmoja tu nakupatia kwamba
hutabaki ulivyo machoni mwa Watanzania.

Najua wapambe wako watakulaumu sana, maana kwa kung'oka
wewe utakuwa umewakosesha ulaji mkubwa. Lakini utakuwa
umejiweka katika nafasi nzuri ya kuwa shujaa mbele ya
Watanzania, kwa kutoboa ukweli na utapumzika kwa amani
baada ya miaka 10 ya kusaka urais na miaka mitano ya
kushutumiwa na Watanzania kwa kutotoa (not delivering)
kile
ulichotarajiwa.

Naamini pensheni itatosha, isipotosha utaongezea kilimo cha
kisasa. Fanya uamuzi sasa ama utakuja kujuta
utakapostaafu.
Watafanya kama walivyomfanyia Chiluba hadi
utashangaa.
Uamuzi ni wako Mheshimiwa Rais
 
..Kashaija unadhani huwa zinamfikia hizi habari au unategemea wale vijana wake ndio wampitishie??

Nadhani next term watanzania hawataangalia sura ya mtu katika kuchagua raisi...
 
Naomba kudiffer. Pamoja na yote uliyoeleza ni ya kweli, mimi binafsi yangu toka moyoni nisingependa Rais wetu mpendwa, na handsome boy Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ajiuzulu sasa. Mbona 2010 sio mbali.

Kama kawaida baada ya Kubenea kusema wana CCM wenye uchungu wa dhati na nchi hii wanapanga mkakati wa kumuengua JK asiwe mgombea wa CCM 2010 ili kuinusuru nchi, hoja hiyo imetafsiriwa kama Uhaini.

Na wenye mkakati huo wamesha uabandon baada ya kujulikana hivyo JK ndiye mgombea wa CCM 2010.

Huu ndio wakati wa watanzania kumjulisha wamechoka na sasa watasema basi inatosha.

Tatizo ninaloliona hapa ni ile kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyere kuwa kiongozi bora ni lazima atatoka CCM.

Hivi hawa wapinzani waliopo wako tayari kuunganisha nguvu wamsimamishe John Memosa Cheyo?.
Makamo awe yoyote ila waziri mkuu Zitto Kabwe.Wakipanga safu nzuri, wananchi watawaamini na CCM itapumzika kwa amani na Mtukufu mpendwa wetu, Mhe. JK kipenzi cha watu, atajumuika na watu wake. Tena itakuwa afadhali angalau kile kijiwe chetu cha
Saigon kitachangamka tena.
 
..Kashaija unadhani huwa zinamfikia hizi habari au unategemea wale vijana wake ndio wampitishie??

Nadhani next term watanzania hawataangalia sura ya mtu katika kuchagua raisi...

Uchaguzi wa sura umeigharimu Tanzania almost miaka 5 ya ubabaishaji natumaini watajifunza in a hard way kutokana na kosa hili. Ninamwomba Mungu alinisuru Taifa tupate Rais mwenye uchungu na nchi na anayejua analofanya in 2010.
 
Naomba kudiffer. Pamoja na yote uliyoeleza ni ya kweli, mimi binafsi yangu toka moyoni nisingependa Rais wetu mpendwa, na handsome boy Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ajiuzulu sasa. Mbona 2010 sio mbali.

Kama kawaida baada ya Kubenea kusema wana CCM wenye uchungu wa dhati na nchi hii wanapanga mkakati wa kumuengua JK asiwe mgombea wa CCM 2010 ili kuinusuru nchi, hoja hiyo imetafsiriwa kama Uhaini.

Na wenye mkakati huo wamesha uabandon baada ya kujulikana hivyo JK ndiye mgombea wa CCM 2010.

Huu ndio wakati wa watanzania kumjulisha wamechoka na sasa watasema basi inatosha.

Tatizo ninaloliona hapa ni ile kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyere kuwa kiongozi bora ni lazima atatoka CCM.

Hivi hawa wapinzani waliopo wako tayari kuunganisha nguvu wamsimamishe John Memosa Cheyo?.
Makamo awe yoyote ila waziri mkuu Zitto Kabwe.Wakipanga safu nzuri, wananchi watawaamini na CCM itapumzika kwa amani na Mtukufu mpendwa wetu, Mhe. JK kipenzi cha watu, atajumuika na watu wake. Tena itakuwa afadhali angalau kile kijiwe chetu cha
Saigon kitachangamka tena.


Pasco huwatakii mema wapinzani,, ooops vyama mbadala. Si wamsimamishe Mtikila.
 
Hivi hawa wapinzani waliopo wako tayari kuunganisha nguvu wamsimamishe John Memosa Cheyo?.
.

Cheyo? Huyu si ndiye yule aliyekwapua mihela ya Waswazi? Awe rais?
 
Ingekuwa heri JK uage sasa

MHESHIMIWA Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, salaam aleykum. Juma lililopita niliwasiliana na Watanzania wote kwa njia hii ya makala. Nilijaribu kuwachokonoa ili kupata mawazo yao juu yako.

Na kwa bahati nzuri nilikuwa nimeongea moja kwa moja na Watanzania wote wakiwamo wasaidizi wako muhimu. Na ili kuwahakikishia kwamba niliwalenga na wao pia niliamua kuwataja kabisa pale niliposema, "Yote kwa yote ni kwamba kila mtu anajua sasa Rais Kikwete uwezo wake wa kuliongoza taifa na chama chake umepungua.

"Ninaamini ndani ya dhamiri yangu kwamba hata wasaidizi wake, wakiwamo usalama wa taifa, mawaziri na manaibu mawaziri, wanamtandao na wapambe wake, wabunge, viongozi wenzake ndani ya chama, watendaji wake serikalini na wasaidizi wake wengineo wote wanajua hili".

Nilifanya hivyo kwa makusudi ili kupata maoni yao juu ya hili. Nawatambua sana wasaidizi wako. Ni watu mahiri sana kwa kulinda maslahi yao na ya wakubwa wao. Nilijua watanijibu haraka haraka kwa kukanusha ukweli huo mdomoni huku mioyoni mwao wakiutambua. Lakini hawakufanya hivyo. Hii inathibitisha kwamba hata wao ukweli uliwagusa na wamefikia mahali ambapo hawawezi kupingana nao.

Wa kwanza kabisa kuwasiliana nami ni kiongozi wa zamani wa CCM katika mojawapo ya nafasi za uongozi ndani ya chama ngazi ya kitaifa. Yeye alinipigia simu kabisa na kujitambulisha kwa jina, nami nikamtambua kwa sauti kwamba ni yeye. Akanipongeza kwa kusema nimeandika vizuri sana na kwa kweli maneno yake na sauti yake yalionyesha dhahiri kukubaliana na ukweli niliouainisha.

Huyu ndiye akazidi kuthibitisha nilichokizungumza katika aya hiyo hapo juu. Ukweli umewasuta ndani ya dhamira zao na kwa kweli umefika wakati ambao ukweli hauwezi kufichika tena. Wengi sasa wanaogopa kukutetea hadharani wasijeonekana vituko kwa kuupinga ukweli ulio wazi (naked truth).

Mheshimiwa Rais, wasomaji walionitumia ujumbe mfupi wa simu, walionipigia simu, walionitumia barua pepe na hata waliozungumza nami uso kwa uso, wote wamenipongeza kwa ujumbe uliokuwa wazi ukieleza ukweli halisi na kila mmoja wao aliishia kusema 'atang'oka' 2010. Baada ya kutafakari ujumbe wa wasomaji na matukio yaliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari juma lililopita, nimeamua kukuandikia waraka huu ili nikupatie ushauri makini lakini bure.

Msomaji mmoja, kwa mfano, aliongea kwa uchungu jinsi ulivyojibu swali la mwanahabari kule Ufaransa. Ulipokuuliza kwa nini nchi yako ni maskini ukasema eti hata wewe hujui. Kwa maoni yake ilikuwa ni aibu kubwa kwa kiongozi wa nchi kujibu hivyo tena mbele ya viongozi na wanahabari wa kimataifa. Uliuonyesha ulimwengu kwamba nchi hii ni ya ajabu na watu wake ni wa ajabu. Ni kama ulikuwa unathibitisha kauli iliyopata kutolewa na mwandishi mmoja kwamba Tanzania ni nchi pekee duniani inayoweza kukaa miaka 10 bila rais na bado ikabaki na amani.

Kwa maoni yangu pia, rais wa nchi kusema hajui umaskini wa wananchi wake unatokana na nini ni sawa na kusema nchi haina kiongozi. Rais wa namna hiyo hawezi kuhangaika na mipango ya kuiondoa nchi katika umaskini, maana hajui kwa nini wananchi ni maskini. Anafikiri pengine ni "wavivu tu wa kufikiri" ama "fursa zipo ila kwa ujinga wao hawataki kuzitumia".

Rais wa namna hiyo hawezi kujua madhara ya ufisadi wa EPA, Meremeta, Tangold, Kiwira, mikataba ya Richmond, IPTL na jinsi inavyochangia umaskini wa watu wake. Hawezi kuona ubaya wa rais na mke wake kujiingiza kwenye biashara kwa kutumia ofisi, fursa na vyeo vyao vya Ikulu kuwanyonga wananchi. Na kwa sababu hiyo hawezi kujihangaisha kuyashughulikia madudu kama hayo kama unavyofanya wewe hivi sasa.

Rais wa namna hiyo atakuwa 'busy' na safari za nje zisizo na kikomo, kukutana na marais wakubwa kama akina George Bush tena wanapokutana Bush atampiga piga mabegani rais kama huyo kama alivyofanya alipokuja hapa Dar es Salaam, na tungetamani kupata tafsiri ya kitendo hicho cha George Bush, ambaye wafuatiliaji wanasema hata mlipokutana Japan alikupiga piga begani tena, kutoka kwa Salva Rweyemamu yule mwandishi wa zamani aliyeisakama serikali kwa kalamu yake, lakini baadaye akawa mwanakampeni wako mahiri kwa kutumia kalamu hiyo hiyo na baadaye ukamzawadia ukurugenzi wa mawasiliano Ikulu.

Mheshimiwa, watu wanashangaa hata kitendo cha serikali yako kushindwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maji, visivyokauka tulivyonavyo hapa nchini na ardhi safi tena kubwa inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kujihakikishia chakula cha kutosha. Lakini badala yake unakwenda Italia kwa kutumia mamilioni ya shilingi kuomba chakula kwa WFP.

Mheshimiwa Rais, si siri ni aibu kubwa. Mabilioni yaliyopotea kwenye ufisadi yangetosha kuanzisha 'scheme' kubwa 13 za umwagiliaji kwenye mikoa 13 ya nchi hii. Na hesabu zake ni rahisi mno wala huhitaji kutumia shahada yako ya kwanza ya uchumi ambayo hata hivyo sijui kma umewahi kuitumia.

Chukua milioni 152 kwa siku kwa mwaka mmoja tu zilizolipwa kwa Richmond/Dowans ambazo kwa siku 365 za mwaka ni bilioni 55. Jumlisha milioni 2,098 zilizolipwa kwa IPTL kwa miaka minane tu kwa kuzingatia kauli ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, bungeni Dodoma Agosti 6, 2007 kwamba kwa kipindi cha Julai 2005 hadi March 2006 peke yake IPTL ililipwa jumla ya bilioni 262.3. Kwa vipindi vinane tu kama hivyo kampuni hiyo imelipwa jumla ya bilioni 2,098. Jumlisha bilioni 133 zilizoibwa kupitia EPA, kisha juu yake ongeza bilioni zisizopungua 600 zilizopotea kupitia ujenzi wa minara miwili pacha pale BoT. Halafu umalizie na mabilioni yaliyopotea kupitia viufisadi vingine vingine kama ubinafsishaji wa TTCL, NBC, Kiwira, n.k ambazo nazo si chini ya 100.

Halafu chukua hiyo jumla inayofikia bilioni 2,986 bila kuongeza bilioni ulizozitumia wewe kwa safari zako za nje tangu uchaguliwe kuwa rais. Igawanye jumla hiyo kwa gharama za mradi mzima wa kupeleka maji Shinyanga ulioshikiwa bango na best yako ili aje kuonekana anafaa kuwa waziri mkuu wa nchi hii. Utapata 13 ambazo ni scheme kubwa za
umwagiliaji zenye thamani ya sh bilioni 225 kila moja.

Ina maana tungeweza kuwa na scheme kama hizo katika mikoa 13 inayoongoza kwa ardhi inayofaa kwa umwagiliaji. Njaa ingetupata wapi. Hivi sasa dunia inapolia na kupanda kwa bei za vyakula sisi tunaoita kilimo uti wa mgongo wa uchumi wetu tungekuwa matajiri kwa kuuza chakula.

Lakini hivi sasa eti serikali yako inapiga marufuku kuuza chakula nje ya nchi, mkulima anayetegemea kuuza chakula chake cha ziada ili apate matumizi yake mengine ikiwamo kusomesha watoto unamwambi nini?

Mheshimiwa Rais, watu waliodunisha maisha ya Watanzania kiasi hicho eti bado hutaki kuwachukulia hatua hadi leo. Umeunda tume juu ya tume nyingine lakini mafisadi wanaendelea kutesa. Ajabu zaidi chama unachokiongoza juma lililopita, kimetangaza eti kumpa onyo kali aliyekuwa naibu meya wa Ilala na kumzuia kugombea cheo chochote zaidi ya udiwani alionao, sababu eti ni kushiriki bomoabomoa ya Tabata Dampo na kuisababishia hasara serikali ya sh bilioni 1.8, kuwasababishia usumbufu wananchi wa Tabata Dampo na kukiaibisha chama.

Gazeti hili likaiandika habari hiyo Jumatatu wiki hii, kwa kichwa kilichosema; 'CCM yacharuka'. Naomba kupingana moja kwa moja na maneno aliyoyatumia mwandishi wa habari hiyo. Kimsingi CCM haijacharuka. Bali ina mkakati pengine unaosimamiwa na wewe mwenyewe mwenyekiti wako kukisafisha chama. Msitudanganye kiasi hicho, kwamba mna uchungu sana na pesa za serikali, mnawajali wananchi na kulinda hadhi ya chama chenu.

Fikiria hasara za mabilioni ya serikali niliyoyataja hapo juu, yote yamesababishwa na wana-CCM, fikiria Watanzania milioni 40 wanaoteseka kwa ajili ya wana CCM na ukumbuke jinsi hadhi, si tu ya chama unachokiongoza bali pia ya serikali unayoiongoza ilivyoporomoka ndani ya mwaka mmoja, kwa ajili ya wana-CCM. Lakini hamjawakaripia wala kuwafuta uanachama kama mlivyofanya kwa Naibu Meya Yakubu.

Huu ni usanii ambao umeshajulikana kwa Watanzania. Mheshimiwa Rais, juma lililopita umetoa kali nyingine ya mwaka. Umewaasa Watanzania wavumilie shida wasikate tamaa. Hii nayo ni kauli nyingine ya mzaha kwa Watanzania kama ile ya kusema hujui umaskini wao unasababishwa na nini.

Natamani ungekuwa unasoma maoni ya wasomaji. Siku hizi Tanzania Daima imeanzisha sehemu ya maoni ya wasomaji wanaosoma gazeti hili, kwenye tovuti. Msomaji mmoja aliposoma alisema hivi: "Kaka yetu usipate tabu wewe sema tu.

Sisi tumezoea shida, huna tofauti na Karume anayewaambia Wazanzibari watazoea tu. Sasa sisi tumezoea na wewe endelea kula nchi maana mafuta si kazi yako. Wewe linda mtandao wako usisambaratike, maana inabidi uutumie kurudi madarakani mwaka 2010." Haya si maoni ya mtu anayekuambia kwa wema. Huyu ana uchungu ndani ya moyo wake na kwa ujumla maneno yake ni laana kwa serikali yako.

Mwingine akasema hivi: "...Kikwete suala la mafuta na maisha magumu havimhusu kabisa. Ndiyo, si anatuonyesha hivyo kwa kuwalinda mafisadi? Na sasa kapata kisingizio cha bei ya mafuta basi ndiyo itakuwa hadithi. Hivi wadanganyika wenzangu mnafikiri bei ya mafuta ikishuka (let's say) hadi nusu, ndiyo maisha yatakuwa bora kwa kila mdanganyika? "Dhahabu imepanda sana bei katika soko la dunia. Kwa nini vitu kama hivi vimeshindwa kufidia pengo la mafuta yaliyopanda?

Watu wengine wanafananisha Bongo na Marekani - eti na Marekani maisha yamepanda. Nyie ndugu zangu hebu acheni mzaha! Wewe unakula humburg na pizza Macdonald halafu unatuambia maisha yamepanda? "Chonde chonde jamani.

Natamani mngerudi huku mkapigika mkashindia kauzu ndiyo mngejua watu wanaongea nini…" Ukurasa huu hautatosha kukupatia maoni ya kila msomaji, lakini natamani ungejisomea mwenyewe habari hiyo kisha chini yake usome maoni ya watu.

Wasaidizi wako wanaweza kukusaidia kutembelea url]http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/21/habari1[/url]. Mheshimiwa Rais ningekushauri jambo moja tu. Kukubali pia ni uungwana wa aina yake na Watanzania wanapenda watu waungwana.

Baada ya ziara yako ndefu mkoani Tanga, utakaporejea Ikulu fanya jambo moja tu. Andaa hotuba yako ya mwezi bila kumshirikisha msaidizi wako yeyote. Ita waandishi wa habari kana kwamba unakuja kujibu tu maswali watakayokuuliza halafu wakisha fika toa hotuba yako kabla hujaulizwa maswali.

Waeleze wanahabari na Watanzania kwa ujumla kwamba wakati unachukua fomu za kugombea urais mwaka 2005 hukuijua vizuri sababu ya umaskini wa Watanzania. Waeleze kwamba wewe ulidhani kazi uliyokuwa nayo ni kuwaita tu wawekezaji uliokuwa umeshazoeana nao sana ukiwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na kwamba wakishakuja kuwekeza tayari maisha bora kwa kila Mtanzania yanajipa.

Sema kwamba umekuja kugundua kuwa mambo sivyo yalivyo. Umaskini wa Watanzania una uhusiano wa karibu mno na utawala wa nchi. Na kwamba utawala wa nchi kwa miaka mingi umebaki kuwa mbovu hasa kupitia 'system' iliyojengwa na Chama chako Cha Mapinduzi ya kulindana viongozi, bila kujali madhara yanayosababishwa na viongozi mafisadi hapa nchini na hivyo hata malaika akiwa rais wa nchi hii kupitia CCM hakuna maendeleo yatakayopatikana.

Sema wazi wazi kwamba kama rais wa nchi hata kama ungekuwa na dhamira ya kuikwamua nchi kutoka kwenye umaskini unaosababishwa na uongozi mbovu, ungeshindwa kwa kuwa kikulacho ki nguoni mwako. Maswahiba zako waliofanya juu chini upate urais ndiyo hao hao mafisadi waliokubuhu hata jina la mafisadi haliwafai tena. Nasikia wengine wameanza kuwaita 'mafisadi'.

Na wewe huwezi kuwatupa wakati ungali ukikumbuka mchango wao mwaka 2005. Kwa sababu hiyo, ili kulinda uhusiano wako nao na wakati huo huo kulinda heshima kupita kiasi uliyopewa na watanzania, umeamua kuachia ngazi na hivyo mwaka 2010 hutagombea tena.

Wapatie Watanzania nafasi ya kuanza kufikiria tangu sasa chama kitakachowafaa kuongoza nchi hii hapo 2010, kutokana na sera zake kabla hawajafikiria ni nani atawafaa kuwa rais wa nchi baada yako. Uhakika mmoja tu nakupatia kwamba hutabaki ulivyo machoni mwa Watanzania.

Najua wapambe wako watakulaumu sana, maana kwa kung'oka wewe utakuwa umewakosesha ulaji mkubwa. Lakini utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri ya kuwa shujaa mbele ya Watanzania, kwa kutoboa ukweli na utapumzika kwa amani baada ya miaka 10 ya kusaka urais na miaka mitano ya kushutumiwa na Watanzania kwa kutotoa (not delivering) kile ulichotarajiwa.

Naamini pensheni itatosha, isipotosha utaongezea kilimo cha kisasa. Fanya uamuzi sasa ama utakuja kujuta utakapostaafu. Watafanya kama alivyomfanyia Chiluba hadi utashangaa. Uamuzi ni wako Mheshimiwa Rais


Umesema ndugu yangu na sina la kuongezea. Kama kweli Mwalimu alikuwa anawatandika watu viboko, hapa kifimbo kingepata ajira ya uhakika. Na mimi nasema wakati wa JK kuondoka ni sasa, ameshindwa kazi, period.
 
Yes Cheyo ndiye the only opposition leader mwenye presidential personality kama wapinzani wakiungana kumsimamisha. JK chali 2010.

Ni cheyo ambaye anacomand respect ya wote hata wanasisiem waliochoka na udhaifu wa CCM watampa kura zao.

Aliyoyafanya Swazi siyajui ila alisaidia sana Watanzania waliofika huko. Yeye na Mwizarubi walijitolea nyumba zao kuwa makao ya kufikia Watanzaia wote bila ubaguzi.

The truth jamaa ana roho nzuri na anabishana kwa hoja na sio kwa jazba.

Hebu nipatie mpinzani mwingine yoyote atakayeweza kusimama na JK akambwaga?.

Naweza nikakupa madhaifu ya wengine wote kama ukuhitaji. Nakiri upinzani una viongozi wengi wazuri swali la kujiuliza ni je wanachagulika?.
 
Kama wasaidizi wa raisi hawamwambii kinachoendelea watoto wake je? Will some one invite them to join this forum if they still havent! Someone better inform daddy dearest that there's some serious socio-political movement going on in cyberspace. A political party in the making perhaps....
 
Ingekuwa heri JK uage sasa!!

Ni matumizi mabaya ya maneno (misuse of phrase). Huyu jamaa alipofikia hawezi tena kusikia lugha ya namna hii; ya kumpapasa na kutekenya tekenya! Sana sana atalala usingizi wa pono! Lugha anayotakiwa kusikia ni moja tu,.... siyo maneno wala kelele ....bali vitendo. Kumwondoa pale mahali kwa kutumia nguvu ya wale waliompa hiyo nafasi, nukta. Haya mambo mengine ni kujifariji na kufurahisha baraza/kijiwe tu!
 
Yes Cheyo ndiye the only opposition leader mwenye presidential personality kama wapinzani wakiungana kumsimamisha. JK chali 2010.

Ni cheyo ambaye anacomand respect ya wote hata wanasisiem waliochoka na udhaifu wa CCM watampa kura zao.

Aliyoyafanya Swazi siyajui ila alisaidia sana Watanzania waliofika huko. Yeye na Mwizarubi walijitolea nyumba zao kuwa makao ya kufikia Watanzaia wote bila ubaguzi.

The truth jamaa ana roho nzuri na anabishana kwa hoja na sio kwa jazba.

Hebu nipatie mpinzani mwingine yoyote atakayeweza kusimama na JK akambwaga?.

Naweza nikakupa madhaifu ya wengine wote kama ukuhitaji. Nakiri upinzani una viongozi wengi wazuri swali la kujiuliza ni je wanachagulika?.

Hii ya kuwasaidia watu na kuwa na roho nzuri si kigezo cha kumpa urais. Hata Don Corleone aliwasaidia sana marafiki zake na kuonekana kuwa mwenye roho nzuri lakini alikuwa ni Mafia tu. Cheyo alikwapua mihela ya Waswazi na hata alipopata ubunge Waswazi walitushangaa sana Watanzania. Kwa Tanzania tunachohitaji sasa hivi si personalities. Tunachohitaji ni vision na baada ya hapo ndipo tuangalie ni nani anayeweza kutusaidia kuifikia hiyo vision. Haya ya personalities ndiyo yaliyotugandisha na akina Mrema na chama chake na Cheyo na chama chake.
 
Nyere alishase,a ikulu hakuna uzuri pale si sehemu ya kujipaka poda wala perfume mlidhan anaota hao sasa mabrazameni wenu!!!!!
Jk&lowassa wanashindwa hata kuangaliana kwa uchafu wao@@@@@@@@@@

wait lowasa atakapotajwa kuwa waziri##$#$#$

eeeeeeeeeeeeeehhhhhhhhhhhhhh

babay face wetu mnatisha babukubwa!!!!!!!!!!
 
QUOTE=Jasusi;310833]Hii ya kuwasaidia watu na kuwa na roho nzuri si kigezo cha kumpa urais. Hata Don Corleone aliwasaidia sana marafiki zake na kuonekana kuwa mwenye roho nzuri lakini alikuwa ni Mafia tu. Cheyo alikwapua mihela ya Waswazi na hata alipopata ubunge Waswazi walitushangaa sana Watanzania. Kwa Tanzania tunachohitaji sasa hivi si personalities. Tunachohitaji ni vision na baada ya hapo ndipo tuangalie ni nani anayeweza kutusaidia kuifikia hiyo vision. Haya ya personalities ndiyo yaliyotugandisha na akina Mrema na chama chake na Cheyo na chama chake.[/QUOTE]

Kwa wakati huu uliobakia kabla ya 2010. Huu sio muda wa kugroom new leader. Aliyoyafanya Swazi has nothing to do with with Tanzania. Hoja yangu hapa ni... Kama sio yeye nani?. Lipumba?, Mrema?, Mbowe?, Zito?, Dr.Slaa?, Mbatia?, Mtikila?. Makaidi?, Chipaka? Au nani anauzika, anachagulika na ana Presidential Personality?. Kwa taarifa tuu, JK hana Presidential Pesonality ila ni handsome boy mwenye haiba ya kupendwa na watu. His smiles doesen't reflect integrity. We need a man of integrity kama Obama.
Tuletee majina ya watu sio kuishia na kina Don, pamoja na Umafia wao, wao ndio wafadhili wakuu wa kanisa Katoliki ndiyo dini yenye wafuasi wengi zaidi duniani. Bulusconi ni Don na alikuwa PM itakuwa Cheyo.

Mbona JK kaupata kwa ufadhili wa pesa za ufisadi? Itakuwa Cheyo?.
 
Kwa wakati huu uliobakia kabla ya 2010. Huu sio muda wa kugroom new leader. Aliyoyafanya Swazi has nothing to do with with Tanzania. Hoja yangu hapa ni... Kama sio yeye nani?. Lipumba?, Mrema?, Mbowe?, Zito?, Dr.Slaa?, Mbatia?, Mtikila?. Makaidi?, Chipaka? Au nani anauzika, anachagulika na ana Presidential Personality?. Kwa taarifa tuu, JK hana Presidential Pesonality ila ni handsome boy mwenye haiba ya kupendwa na watu. His smiles doesen't reflect integrity. We need a man of integrity kama Obama.
Tuletee majina ya watu sio kuishia na kina Don, pamoja na Umafia wao, wao ndio wafadhili wakuu wa kanisa Katoliki ndiyo dini yenye wafuasi wengi zaidi duniani. Bulusconi ni Don na alikuwa PM itakuwa Cheyo.

Mbona JK kaupata kwa ufadhili wa pesa za ufisadi? Itakuwa Cheyo?.[/quote]
Pasco,
Naona hujanielewa ndugu yangu. Tanzania ya sasa haitafuti au haihitaji mkombozi as in personality. Tunachohitaji Watanzania ni ukombozi. Ndio maana nimesema kwanza tu-identify vision itakayotuletea ukombozi na baada ya hapo ndipo tusema katika visheni hii ni nani aliye na uwezo wa kutuongoza. Wewe umekazania personalities mimi nimepanua uwanja kidogo. Najua kuna Watanzania wengi tu wenye uwezo. Nakubali kabisa kuwa tunahitaji mtu mwenye integrity lakini hawezi kuifanya kazi hiyo peke yake. Kwa hiyo kama unataka majina mimi huko hunikuti. Tuzungumzie vision itakayotuondoa kwenye matatizo tuliyo nayo and then we can identify who among us is dedicated and can help lead to the promised land. For your info I also know Cheyo more than you can imagine.
 
Haya tena tunarudi kule kule.. tunatafuta KUIGA!... jamani kiongozi wetu apatikane kulingana na sisi wenyewe ktk mazingira haya magumu tuliyokuwa nayo..
Hawa ma Don mnaozungumzia tunao kina Rostam na tumeyaona matokeo yake iweje tufikirie kuwa ma Don nchini wanaweza kuwa sawa na Marekani wakati watu na mazingira yetu hayafanani?...
Mimi namtaka Dikteta mmoja mwana mapinduzi kama Chavez wa kibongo bongo!
Nani mweye Ubavu huo hata sijui, lakini tunahitaji dikteta mwenye kuweka maslahi ya Taifa mbele dhidi ya propaganda zote za kifisadi iwe toka ndani ama nchi za nje!
 
Watu wa karibu wa rais hawamwambii ukweli,wanachokifanya ni kumpa moyo tu.Mnakumbuka alisema KELELE ZA CHURA HAZIMZUII MWENYE NYUMBA KUPATA USINGIZI.
 
Back
Top Bottom